CCM mnaogopa nini kuwatumia Polisi kuvuruga vikao vya vyama?

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
POLISI WAVAMIA KIKAO CHA CHADEMA NA KUAMURU MBUNGE KUONDOKA

Mbunge wa viti maalum CHADEMA mkoa wa Mwanza (Mh Sussane Massele) akiwa anaendelea na ziara yake ya ujenzi wa chama mkoani Mwanza. Leo tarehe 5/1/2017 akiwa kata ya Malya iliyopo jimbo la Sumve ambayo inajiandaa na uchaguzi Mdogo wa udiwani. Na Sussane Maselle akiwa kiongozi wa timu ya kampeni katika kata hiyo leo alikuwa akifanya kikao cha ndani kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa kampeni katika Kata hiyo. Kikao hicho kilijumuisha kamati tendaji ya jimbo, kata na wanachama waalikwa
Ghafla jeshi la Polisi lilivamia kikao hicho na kuamuru Mbunge kuondoka eneo la tukio kwa madai kuwa hali ya kiusalama siyo nzuri
Mh mbunge aliwahoji lakini akataka kujua hiyo taarifa ya hali ya usalama kutokuwa nzuri jeshi la polisi wameitoa wapi? Ndipo alipoondoka na msafara wake hadi kwa mkuu wa Polisi wilaya ya kwimba ili apate ufafanuzi zaidi
Mkuu wa polisi alisema alipigiwa simu kuwa kuna kikundi cha watu kinataka kufanya vurugu kwenye kikao cha Mbunge. Hivyo akatuma vijana wake eneo la tukio. Baada ya Maelezo hayo Mh Mbunge aliuliza je jeshi la polisi linapopata taarifa ya kikundi fulani kutaka kufanya fujo kwenye kikao, jukumu lao ni kufukuza watu kwenye kikao au ni kulinda usalama ili kikundi hicho kisitekeleze malengo yake?
Baada ya mahojiano hayo Mh Mbunge alibaini kuwa ni hujuma na yeye msafara wake walirudi Mwanza kujipanga zaidi na kutoa tamko

Hivyo ofisi ya Mbunge inalahani kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi pia inatoa tamko na kulitaka jeshi la polisi litekeleze majukumu yake ya kulinda amani na usalama kwa misingi ya kidemokrasia
Pia ofisi ya Mbunge inapenda kuwambia wanachama wa CHADEMA, wapenzi na Watanzania wot kuwa Mh Mbunge hatorudi nyuma katika mapambano haya ya kutafuta kweli na haki. Na hii ni dalili nzuri kuwa kata ya Malya inaenda kuchukuliwa na Chadema kwani wananchi wamekwishaamua na yeye anaendelea na vikao vya ndani na mikutano kuakikisha ushindi unapatikana

Imetolewa leo
Na ofisi ya Mbunge viti maalum CHADEMA mkoa wa Mwanza
Fesali Majura
Katibu wa Mbunge
 
Tumeshasema kuwa hatutaki mikutano ya kisiasa HAPA KAZI TU.hamsikii sasa hamna namna nyingine tutawatawatawanyisha tu.
 
Wanaogopa kivuli hao!rudisheni kura za Lowasa bila hivyo ni juu kwa juu mpaka mseme poo.tangu lini policcm awe na huruma mbunge wa chadema akifanyiwa vurugu na kikundi ? Km co maigizo ya amboni mnarudia tu ! Wananchi wamesha jua mbinu na uovu wenu kuliko mnavyo fikiri.hampati wajinga tena,muda huo ulishapita.na hali ya uelewa wa watu imeongezeka,ss mnavuruga mikusanyiko ya cdm kwa kujua hamkubaliki na mikusanyiko yenu itakua dhoofu bin hali.
 
CCM waoga kama kunguru wanajua Jecha hawezi kujigawa maeneo yote hayo kuwaokoa inabidi kitengo maalum cha Mwigulu Nchemba kiingie front kufanya mafekechee kuokoa jahazi maji yamewafika utosini.
 
Inasikitisha sana mambo kama haya yanafanyika nchini mwetu.. Sikuwahi kufikiri kama tutafika huko.. Siasa ni ajira , demokrasia ni afya kwa Taifa.. Nimemiss Bunge live, Choppa za Kina Slaa, Mipasho ya Kina Lipumba.. "Where is Our Democracy Heading"
 
Yaani polisi wamepata taarifa kuna kikundi cha wahuni kinapanga kuvamia mkutano wa ndani mahali fulani...nilitegemea polisi wangejipanga strategically ili wapate kuwanasa wahuni hao. Ina maana polisi ya Tanzania ni waoga hivi?
 
Watuambie kama nchi hii kwa sasa ni ya kijeshi? Haki zetu haziwezi kuporwa na yeyote bali zitacheleweshwa tu.Polisi mjue unapomtesa mtanzania wa Malya na wewe baba yako dada yako kaka yako sehemu nyingine ya nchi hii wakati huo huo ananyanyashwa na jeshi lako.Hakika usiku umesonga sana mchana unakaribia.
 
Back
Top Bottom