Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,315
- 38,454
CCM mnakera sana, yaani kila jambo mnalolifanya hata kama ni ovu nyie huona ni sawa tu kwa kuwa mnalifanya nyie. Mfumo wa vyama vingi ulipoingia chama chenu hakikufuata hatua ambazo vyama vingine vimepitia, badala yake kikajisajili cha kwanza na ndiyo ule msemo wenu maarufu wa "CCM Nambari One" ulipoanzia.
Baada ya Uchaguzi wa mwaka 1995 Chama chenu kikaanza kujimilikisha mali za Umma na kuzifanya zenu. Mlijimilikisha viwanja vya michezo, shule, Majengo, viwanda, mashamba na kila kitu mlichoweza. Na bado mkaona sawa.
Mlipogundua kwamba CCM al manusra iangushwe na NCCR-Mageuzi kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 kwa sababu vyama vilipewa ruzuku ya Uchaguzi,mkabadili sheria na kutoa ruzuku kwa vyama vyenye wabunge peke yake kama vile ni wanachama wa vyama hivyo tu ndiyo wanalipa kodi katika nchi hii.
Kwa miaka zaidi ya 20 ya mfumo wa vyama vingi nchini, viongozi wa CCM waliokamatwa na Polisi kwa makosa ya kisiasa ni kama tone la sukari kwenye bahari. Lakini viongozi wa vyama vingine wanakamatwa kama mchezo wa kuigiza kila siku. Ni kama vile kuwa kiongozi wa chama cha upinzani Tanzania ni laana. Nyie kwenu mnaona shwari tu
Nchi hii miaka yote inaoongozwa na nyie lakini kila kushindwa kwenu mnadai ni kwa sababu ya vyama vingine vya siasa ama viongozi wao. CCM mnakera sana kwa kujifanya kwenu kwamba nyie ndiyo wenye hatimiliki ya siasa za nchi hii!