Uchaguzi 2020 CCM mnajitapa kuwang'oa wapinzani katika majimbo yao kwa gharama yoyote, hiyo gharama muitumie kuondoa umaskini kwa wananchi

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Kumekuwa na kasumba ya viongozi wa CCM kujitapa kuwa Octoba 2020 wabunge wa Upinzani watang'olewa katika majimbo yao kwa gharama yoyote.

Hiyo gharama yoyote ni ipi? Wizi, rushwa, kutangaza CCM hata kama hakushinda, kuwateka au kuwafunga wagombea wa upinzani, kuwaondoa katika fomu za wagombea?

Kama ni gharama yoyote (nguvu au pesa), iwekeni katika kuboresha maisha ya wananchi. Mmefanya siasa miaka minne mfululizo peke yenu lakini bado mnawaogopa wapinzani?

Zitto amezuiliwa Kigoma, ila Bashiru anafanya mikutano halafu anajitapa kumng'oa Zitto. Haha haaaa VITUKO VYA MWAKA.

UNAPIGANA NA MTU ULIYEMFUNGA PINGU MWILI MZIMA HALAFU UNAJIONA MSHINDI...
 
Kwanini usifikirie wao kutumia midomo two kupitia napiga kura, unakimbilia rushwa n.k. tu
 
Wao wajitangaze washindi nchi nzima hata leo wasisubiri October lkn watakuwa kama yule bwana (Gehazi) aliyemtapeli Jenerali Naaman, 2 Wafalme 5:20-27.
Sasa ccm watakuwa wamefaidi nini kuwa ktk ligi moja na akina Zanu-PF.

This will be a very foolish blunder that will cost them dearly throughout history of their existence as a political party.
 
:D :D :D :D sawa mkuu, sio mbaya ila nilipenda nijue liko level gani kielimu Hilo SoMo, huenda sjaifikia hio level
Somo la kufikiria lipo kila level, ShariaE. Umakini wako tu ndiyo utakufanya ujue somo la kufikiria lipo, sio shuleni tu, ila hata kwenye maisha yetu ya kila siku.

Tatizo mfumo wa elimu tulioupata wa Tanzania wengi ni ule unaohamasisha kukariri na ndiyo maana sishangai kuwa wengi wetu huwa hatufikirii ila tunakariri tu.

Kwa lugha nyepesi, Kufikiria ni somo ambalo ulifundishwa kuanzia nyumbani hadi leo ila linahitaji umakini tu kujua unafunzwa kufikiria. Naamini umenielewa sasa.
 
Akhsante, nimekuelewa.
 
CCM ndiye aliyesababisha nchi hii iwe fukara wa kutupwa pale ilipoamua kujikita kwenye uchawi wa mwenge na mambo ya matambiko.
Haikujikita kwenye kuboresha elimu Wala kukuza uchumi.
Sisiemu nyoko kabisa.
Nyoko ni mama
 
Yaani ungekuwa karibu ningekupa soda umeusoma ubongo wangu .Dk mzima busy kupata majimbo ya wapinzani badala ya kuongelea maendeleo ,wame implement ilani yao ki vipi .Mipango ipi next 5years nk.
 
Wale wananchi wa Kigoma na majimbo mengine chini ya upinzani tunataka kuyarudisha kundini nao wapate maendeleo kwa kasi kama wanyonge wenzao chini ya CCM. Hamuoni majimbo yaliyo chini ya CCM yalivyopiga hatua kimaendeleo chini ya chama cha wanyonge CCM?. CCM ni chama cha wanyonge hivyo lazima tuhakikishe wanyonge wote wanakuwa CCM.
 
Ukonga mbona mmelitelekeza
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom