CCM mnaburuzwa na upinzani mmekosa ubunifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM mnaburuzwa na upinzani mmekosa ubunifu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jun 8, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Chama changu ninakiheshimu sana kama chama, ila napata shida kweli na wengi wa nyinyi viongozi, hii tabia gani hii kila upinzani wakileta daladala mnadandia hata hamjui linakokwenda, kwani nyie hamjapanga safari yenu vizuri? kwanini msipange safari yenu vema na mkaiweka yenye mvuto mkiwashawishi watu kule mnakokwenda ili wajiunge na nyinyi? Nimesoma na mabango yenu ya mjini ni ishara tosha kabisa kwa wengi kuwa hamna hoja mnasubiri upinzani wawaburuze mjibu hoja.

  Kwakweli kibao kimegeuka, zamani upinzani walikuwa wanahangaika na hoja za CCM; leo CCM wanahangaika na hoja za upinzani... ni nini? Mnazani mkijipanga vizuri na mkaacha utumbo wenu uliojaa ubinafsi na kuacha kuhangaika na hoja za upinzani mkawa na hoja zenu mkaziwekea uzito na mkawa wa kweli sio wanafiki, wazandikiki wenye kupeana madaraka kati yenu, marafiki wenu na ndugu zenu kwaajili tu ya kuishiwa na sifa ya uongozi na utawaa hivyo mnataka mambo rahisi maana marafiki na ndugu watawatii hata kama hamna nidhamu wala sifa ya kuongoza.

  Mnatutia aibu, huu mkutano sio wakati wake, na kwama mliupanga kabla mngeupotezea unawaletea aibu... na natumaini kesho hamtaleta uswahili na matusi kama mnavyofanya kwenye mikutano mingi, hatutaki matusi tunataka hoja hatutaki upumbavu wenu wa kuleta huhuni kwenye chama. leteni hoja zenu msilete matusi.

  Nawaambia CDM kama chama na viongozi hawawezi kifikia CCM hata kidogo kiubora, ila nyinyi nyuinyi nyinyi mlioko madarakani mmejimilikisha CCM so utumbo uliooza na maharage ya kuchacha ndio manwalisha watu, mnakiuwa chama siamini....

  MNAJUA WATU WANATAKA NINI? MVUTO WA HOJA, MVUTO WA VIONGOZI, MVUTO WA HAMASA NA UHAMASISHAJI NA KUTIANA MOYO NA KUHAMASISHANA KUFANYA JUHUDI ZA MAENDELEO. HOTUBA ZENU NA STAILI ZENU ZA HOTUBA NI ZILEZILE HAZIBADILIKI HAZINA MVUTO KABISAA, WALA SAUTI YA VIONGOZI HAINA TOFAUTI YA MTU ALIYEVIMBIWA AKIMHUTUBIA MWENYE NJAA.

  MNALO HILI? MNAWEZA KULETA HILI? kati ya haya yote hakuna hata moja linaloweza kuletwa kwa rushwa.
   
 2. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa nin mnaudharau ubunifu wa Nape nyinyi?
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  CCM inaelekea shimoni na sasa imefika a point of no return! unajua mtu anayezama akiona hata unyasi anajaribu kuushika akifikiri utamuokoa! Hakuna mtu CCM anayefikiria future ya chama sasa hivi kila mtu yupo busy kuiba na kujitajirisha harakaharaka kwani wameshaona mwisho wao! Ndipo Hoja za wapinzani zinapokuwa nyingi wanakurupuka kujibu na wanajibu utumbo! Utasikia hoja za kipuuzi atakazotoa wasirra kama atakuwepo kesho jangwani!!Hii kudandia daladala ya wapinzani ni kujaribu kujisukuma ifike 2015, maana wanaogopa chama kisisambaratike kabla ya hapo!!
   
 4. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Ninamheshimu Nape, yeye na kundi la vijana wengine wasio jiweka wazi walifanya juhudi za makusudi za kutaka kukifufua chama ikiwa ni pamoja na kuandaa mapendekezo ya re-branding, kati yao walikuweopo wataalamu waliobobea kwenye social marketing na wenye mafanikio makuwba kwa makampuni tunayoyajua yanayofanya vema kwenye soko) na juhudi zake ni za wazi, ila mara ngapi tumeona juhudi zake zikihujumiwa?? Wako watu ndani ya CCM wanaamini hiki chama ni cha kwao... hawaoni mbele wala nyuma
   
 5. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Nape ndiyo kakosa ubunifu siyo CCM
   
 6. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nape ni kama tone la wino katika bahari, itabadilika rangi kweli?
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Ccm inacheza kiduku cha nape.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 8. p

  petrol JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Kwa mbali naona kama kuna kaukweli ........... ccm kufuata upepo wa chadema. LAKINI ANGALIZO: Yatakayosemwa kesho, yasipingane na hotuba ya bajeti wiki kesho. Vinginevyo itakuwa tena fursa ya chadema kuirarua serikali na ccm humo bungeni na baada ya vikao vya bunge chadema kurejea kwa wananchi kushindilia msumari zaidi. chonde chonde ccm, acheni kuwapa turufu ya kisiasa hao chadema. ninachoeleza ni kukubaliana na mawazo kwamba timing ya mkutano wa kesho hapo jangwani inaweza usiwe mtaji kwa ccm. itaweza kula kwenu. malalamiko kuhusu maisha magumu, ukosefu wa kazi kwa vijana, bei ndogo ya mazao ya kilimo, matatizo ya maji hata katika jiji la dar, umeme, ufisadi, reli ya kati, n.k. n.k. ni masuala mazito na hayawezi kuzungumziwa kijuujuu hapo jangwani. Bajeti ndiyo itakayotoa majibu. tusisahau hilo. tukifanya hivyo tutazidi kuichimbia ccm kaburi la kisiasa .
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,832
  Trophy Points: 280
  Pole sana prof majimarefu,hii ndio nyinyiemu ya nape. Nawashauri mkae kikao na muamue kumuweka lusinde kama katibu mwenezi taifa kuliko Nape ambaye amekuja na style ya copy and post from cdm.
   
Loading...