MtuHabari
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 321
- 1,019
Ni wazi kuwa sakata la uvunjifu wa katiba Bungeni linamkera sana Mheshimiwa Rais mama Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM.
Tatizo ni kuwa kama Rais hapendi aonekane kuwa anaingilia mihimili mingine ya nchi kwa kutoa kauli, maana kauli ya Rais ni kama sheria.
Spika Ndugai analijua hilo na anatumia upole huo wa mama kuendelea kufanya ujinga unao aibisha Bunge, Chama chake na Rais pia.
Je, kwa nini Ndugai ambaye ni mjumbe wa Kamati kuu ya chama CCM haimuonyi kuwa ana mdhalilisha Rais? Au kwa vile ni mwanamke mnayemuona "mzuri na mweupe" kama alivyokuwa anamuona na kumuita Marehemu Rais Magufuli wakati akiwa Makamu wa Rais?
CCM ni wajibu wenu kumlinda mwenyekiti wenu dhidi ya Spika anayetumia kinga ya kibunge kumdhalilisha mwenyekiti wenu, waagizeni wabunge wenu wamshikishe adabu kwa tishio la kumn'goa kwa kura na atashika adabu.