Elections 2010 CCM mlezi wa ufisadi

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
298
Utawala wa kifisadi hapa Tanzania mlezi wake ni CCM. Ushindi wa CCM hutegemea sana ufisadi hivyo ni vigumu sana chama hiki kuondoa ufisadi Tanzania. Wakati wote wa kampeni hatukusikia wagombea wa CCM kuanzia urais , ubunge na udiwani walioweza kuzungumzia namna ya kushughulikia ufisadi. Wote tunajua wazi kuwa tatizo kubwa hapa nchini ni utawala wa kifisadi ndio unatufanya tusiendelee.

Ufisadi umetamalaki kila kona ya nchi hii. Huduma hupatikana kwa rushwa, mizengwe. Taifa limesimama, haliendi au hatusogei kabisa. CCM hawana mpango wala dhamira ya kushughulikia ufisadi kwani unawasaidia sana katika kufikia malengo yao ya kifisadi.

Wanachama wa CCM hawawezi kushiriki kupiga vita ufisadi badala yake wanashiriki vilivyo kuulea mfumo huu hatari sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Mara nyingi nashangazwa na baadhi ya wanachama wa CCM wanaohadaa watu kuwa chama chao kinapiga vita ufisadi.

Narudia tena CCM ni mlezi wa wa utawala wa kifisadi hapa nchi. Ili kuondoa ufisadi sharti tuanze kumwondoa mlezi wake ambaye ni CCM.
 
WEWe tafuta njia yakutafuna pia nchi imeoza hiii chukua chako mapema! WALA SI DHAMBI!
 
WEWe tafuta njia yakutafuna pia nchi imeoza hiii chukua chako mapema! WALA SI DHAMBI!

Kamwe sitakuwa tayari kuitafuna nchi yangu, kama ni mali ntatafuta kwa njia halali. Wazee wetu wangekataa tamaa kama wengi wetu tulivyokata tamaa, tungepataje uhuru?

Tuwe pamoja kumshughulikia mlezi wa ufisadi yaani CCM
 
Back
Top Bottom