CCM mkitaka kuisimamia serikali yenu vizuri, tenganisheni chama na serikali

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Mambo hayako sawa katika taifa hili.

Ukikosoa tabu kwa chama!
Ukinyamaza tabu kwa wapiga kura wako!
Na sasa wengi hujikuta wakiponda kwa asilimia mia! na kuunga mkono kwa asilimia mia!
Kimsingi nimekuja kugundua kuwa mfumo huu ni bonge la karakana ya unafiki wa kiwango cha lami.

Na tena; mkiendelea kukumbatia mfumo huu, japo kwa miaka mitano tu, sitanii, mtakuwa mmeshawapoteza askari wenu wote makini, na hivyo kubakiwa na wale viroja wachekeshaji tu!

Ndugu zangu wanaccm, sote tunakubaliana kuwa; haiwezekani, kwa rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama kuikosoa serikali anayoingoza yeye mwenyewe!

Hii ndiyo sababu kuu inayofanya wabunge wakosoaji wa ndani ya ccm kuonekana ni wapinzani, au tuseme ni wabaya wa chama!
Na ndiyo maana hawana mtetezi mwenye nguvu ndani ya chama chao!
Nami nakiri kuiona tabu mnayoata toka kwa wakosoaji wenu, lakini hata hivyo hatari ya kunyamazia uozo, tena mwingine uliokithiri ni kubwa kuliko tabu mnayopewa na wakosoaji wenu.

Labda tu kama uwepo wa chama chenu madarakani hautegemei sanduku la kura wakati wa uchaguzi, hapo mtakuwa sawa!

Mwisho, hivi kulingana na mfumo wa daemokrasia tunaoufuata kuna ugumu gani wa kutenganisha hizi kofia mbili ili moja isimamie nyingine?
Ni mawazo yangu tu.
 
Kwa sasa CCM ndiyo SERIKALI na SERIKALI ndiyo CCM ni ngumu sana kujipambanua na alisema wanachama wa CCM ndiyo waajiri wa wafanyakazi serikalini,upate picha kinachoendelea.
 
Ccm inasimamiwa na serikàli hivyo hakuna uwezekano wa kujitoa,
Nakubaliana na hoja yako.
Kwa hali ilivyo ni rahisi serikali kuisimamia ccm kuliko ccm kuisimamia serikali.
 
Back
Top Bottom