CCM mkimwachia Rais Magufuli atakuwa kama Kagame!

abudist

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
850
781
Maneno ya mwalimu Nyerere Julai 19. 1967 ''Udikteta ni serikali ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache na wao ndiyo huwa sheria. Anayepinga watakayo, basi huonyeshwa cha mtema kuni,''

Leo hii ndicho anachofanya Rais Magufuli kwamba mtu mwingine yeyote mwenye maoni tofauti na yale ni adui na lazima aadhibiwe. Sasa amekubali kumtoa kumtoa Mh. Nape Nnauye mtu ambaye amefanya kazi yake kwa weledi. Ilimradi amlinde Daudi Bashite ambaye mpaka sasa, kwa taarifa zilizopo rasmi imedhihirika ametenda makosa ya jinai. Sasa Magufuli anaendeleza ubabe na udikteta ndani ya CCM baada ya kuwaadhibu wanachama kwa kuwa na maoni tofauti. Na sasa anafanya haya kwa nchi nzima sababu yeye ni rais wa wote na siyo wa CCM tu.

Hivyo ndivyo afanyavyo rafiki ya Kagame. Kagame hawakandimizi, kuwafunga na kuwaua wapinzani tu, bali hufanya hivyo hivyo kwa watu ndani ya chama chake wanaopingana na maoni yake. Hivyo ni ndivyo anavyofanya Kagame na hatimae kama hayo hayatoshi amekuja kubadilisha katiba na sasa ataongoza milele. Sasa CCM isipomthibiti Magufuli atataka apitwe bila kupingwa na ndani ya CCM (Sababu wataogopa wakimpinga watakuwa wasaliti) kama mgomba 2020. Na akipita na kuchaguliwa basi ataanza mkakati wa kubadilisha katiba ya Tanzania ili yeye aendelee kuwa rais zaidi ya miaka 10. Na jinsi anavyotupeleka hilo linawezekana na ndiyo inavyoonesha nia yake. Mtu huyu anaviashiria vyote vya udikteta. Ikumbukwe CCM bila Alhaji Kinana na Mh. Nape isingeshinda uchaguzi uliopita. Ushindi ulitokana na juhudi za hawa wawili kuwa majasiri na kurudisha imani za wananchi. Magufuli alikuwa 'Outsider' na alipata nafasi hii baada ya kuwa kwenye muda muafaka. Lakini sasa hakumbuki nani alimuweka hapo na hiyo ni hatari kubwa. NA NDIYO MAANA RAIS HUYU, HATAKI KUENDELEZA JUHUDI ZA KUPATIKANA KWA KATIBA MPYA ILIYOPENDEKWEZWA. INGAWAJE IMEWAGHALIMU MABILIONI YA PESA WALIPA KODI LAKINI IMEWEKWA KAPUNI.
 

Attachments

  • IMG-20170323-WA0005.jpg
    IMG-20170323-WA0005.jpg
    25.6 KB · Views: 51
mtu anayetenda na kufanya kazi yake kwa kufuata misingi, taratibu na kanuni za sheria anatumbuliwa na yule anayevunja,kuharibu na kutofuata sheria analindwa anatetewa na kuachwa..hili ni jambo la kushangaza mpaka hapo no democracy no rule of law..
 
Hata akiwa dikteta poa tu, as long as he's delivering.
sentensi moja tu ya yale aliyofanya na yana tija tafadhari kwa sisi tusioona. Mimi najua vihiyo wametemwa ila Bashite bado, viwanda vingapi vimeanza kujengwa, Bashite kapewa eneo hewa na akakubali mbele ya matv yote, bado nasubiri useme.
 
Matendo yake ndivyo walivyoanza madikteta wote duniani kutumia nguvu ya utawala wake kuzima vilio vya walio wengi!

Na kuteua wale tu ambao watamlamba miguu na kumtetea matendo yake ya kidhalimu,

sasa naiona dalili ya wazi iliopo mbele yetu kwa kufumbia macho yale yote yaliopigiwa kelele ndani ya nchi,

Ni dalili tosha anataka kutengeneza taifa la kabila lake ndani ya nchi ilioyo huru,

Bado hatujachelewa 2020 si mbali tusiangalie rangi tuungane watanzania kuundoa huu mti ulioanza kumea hapa!
 
Back
Top Bottom