CCM, Mfumo wa Chama kimoja na Kisa cha malaika wa Zawadi

MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
4,927
8,906
Kisa chenyewe!

"Malaika mmoja alimtokea Mtu mmoja nyumbani kwake, akamwambia maombi yake kuhusu hali ngumu yamesikilizwa na hivyo anaweza kumwambia cochote akamsaidia.
Ila kabla hajachagua kuna sharti moja tu, cochote atachokiomba JIRANI atapata Mara Mbili yake!

Yule mtu baada ya kusikia hivyo. Akawaza sana. Baada ya muda akaamua kuchagua Atolewe JICHO MOJA"

Mwisho wa kisa.

Ni nini hapa najaribu kusema.

Unadhani ni kwanini serikali ikipeleka muswada bungeni ambao kwa kawaida huwa unaonekana mbaya lakini ukifika bungeni, ukianza kupigiwa kelele tu either na wabunge wa upinzani au na wadau wengine then ndio unafanywa kuwa Mbaya zaidi ya hapo ?

Unadhani ni kwanini Kitu chochote kinachoonekana kinapigiwa sana kelele na asasi za kiraia na vyama vya upinzani basi kitu hicho hufanaywa kwa nguvu sana.
Unadhani ni kwanini kila mradi wa serikali either wa ununuzi wa ndege, SGR au barabara huwa ni kama sehemu ya kurushia madongo waliokuwa wanaupinga ?

Either way, CCM haijawahi kuwa tayarikwa vyama vingi. Tulilazimika kuingia tu baada ya shinikizola wazungu na utashi tu wa Mwalimu Nyerere ambaye kwasasa hayupo.
Kwasasa upo tu kwaajili ya kuombea pesa za wazungu.

CCM wako TAYARI kuvumilia SHERIA sheria au MAAMUZI hata yawe mabaya kiasi gani ilimradi tu maamuzi hayo ytawauimiza pia Wapinzani. That's their happiness.

Anyway, kuna msemo "Utajua thamani ya kitu pale utakapokipoteza"
 
Huku mtaan naona yameshaanza kuisoma namba nami bila hyana nayasomesh vilivyo

kuna limwanasisiemu lilikua linauguliwa na mkewe (alijifungua kwa operation) lilikuja kuniomba msaada wa fedha kidogo kwa ajili ya kumpeleka hospital ilikua pesa kidogo tu TSH 10,000/=

ilibidi tu nimnyime huko roho inaniuma na kumkomesha zaidi nikaenda kula kitimoto na bia pamoja na wana kwenye ki grocery cha karibu hapa mtaani na alituona
 
Kuwa na ubinadamu, siasa si ugomvi! Kama wao wamegeuza ugomvi wewe sambaza upendo tu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom