maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Mwaka 1984 CCM ikiwa chini ya uwenyekiti wa baba wa taifa mwalimu Julius K Nyerere ilimfukuzilia mbali aliyekuwa makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi.
Jumbe alipokwa nafasi zote za uongozi alizokuwa anazishikilia ndani ya chama na serikali kwa kile kilichoitwa kuchafua hali ya hewa.
Kwa mtazamo wangu kile wanachokifanya Rais Mohamed Shein na makamo wake balozi Seif Iddi hakina tofauti na wakati mwingine ni zaidi ya kile alichokifanya Jumbe wakati ule.
Dk Shein, kiongozi aliyeapa kuilinda katiba ya Zanzibar, kwa kitendo chake cha kukubaliana na wahafidhina wa CCM kupora ushindi wa CUF na kung'ang'ania ikulu na hata kutangaza matakwa yake ya kurudia uchaguzi ni uvunjaji wa makusudi wa katiba na kupandikiza hisia za vurugu na vita, kitendo kinachomwondolea sifa ya kuwa kiongozi anayeweza kuisimamia na kuilinda katiba.
Dawa ya watu wa aina ya Shein na balozi Seif Iddi ni kwa chama chao cha CCM kuwafukuzilia mbali kutoka katika chama chao kabla hawajaiingiza nch katika machafuko.

Last edited: