CCM Meru yavuna wanachama wapya 150, akiwemo mwenyekiti wa CHADEMA

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,133
659
Aliyekuwa mwewnyekiti wa Chadema bw Nuru Maeda akirudisha kadi ya chadema na kuchukua ya CCM MBele ya katibu wa CCM wilaya ya Meru bw Langaeli Akyoo Picha, Habari na Gladness Mushi wa Fullshangwe- Arusha Wakati chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiwa kinaendelea na Oparesheni ya Vua Gamba vaa Gwanda ikiwa inaendelea chama cha mapinduzi (CCM)kimefanikiwa kuvuna wanachama wapya 150 kutoka Chadema ndani ya Eneo la Magadirisho Wilyani Meru Mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa Tawi la Magadirisho, Bw Nuru Maeda.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa CCM wilaya ya Meru bw Langaeli Akyoo wakati wa kuwapokea wanachama wapya akiwemo mwenyekiti huyo sanjari na kufungua ofisi mpya ya tawi hilo mapema jana. Aidha bw Akyoo alisema kuwa wamefanikiwa kupata wanachama hao wapya 150 kwa kipindi cha wiki mbili ambapo wanachama hao hapo awali walikuwa ndani ya chama cha Chadema na hivyo kurudi katika chama Tawala Alifafanua kuwa mbali na kuweza kuvuna wanachama wapya 150 kutoka Chadema pia wamedhamiria kufanya mabadiliko mbalimbali ambapo mabadiliko hayo yataweza kuchochea kwa kiwango kikubwa Mabadiliko hata ndani ya Mashina,Kata,na hatimaye kwa Wilaya nzima.

"hawa wanachama 150 ni wapya kabisa na wanatoka hapa hapa Magadirisho na tunachofurai ni kuona kuwa watu wanatiumia vema
demokrasia yao wenyewe na pia zoezi hili halitakuwa lakuisha kwa mfululizo tumejipanga kuhakikisha kuwa tunaendelea kuvuna wanachama wengi zaidi nah ii ni dalili kuwa Jimbo bado lipo ndani yetu kwani kwa sasa ni sawa na limekopeshwa tu ila bado ni mali ya CCM"aliongeza Bw Akyoo Pia alisema kuwa ingawaje wamefanikiwa kuvuna wanachama 150 pamoja na mwenyekiti wa Chadema bado wana mipango na mikakati mbalimbali ya kuweza kusaidia jamii ya watu wa eneo la Magadirisho hasa kwa Upande wa kukuza na
kuimarisha zaidi uchumi wa maisha yao Alisema kuwa Chama hicho kwa Wilaya ya Meru kimejidhatiti kuimarisha chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) ya Magadirisho ambapo kupitia chama hicho wananchi wataweza kuimarisha shuguli zote za kiuchumi ambapo wengine wanakosa dhamana kama hiyo hali ambayo inachangia sana umaskini.

Awali aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, Bw Nuru Maeda akikabidhi kadi hiyo ya Chadema na kupokea ya CCM alisema kuwa kilichomfanya akimbie chama hicho ni pamoja na kukosekana kwa uzalendo ambao unatangazwa kila siku hali ambayo inasababisha
madhara kwa wanachama wake Alifafanua kuwa demokmrasia ndiyo iliyomfanya akimbie chama hicho na kutokana na hali hiyo bado ana mpango wa kuendelea kuwachukua wafuasi wake mbalimbali ambao alikuwa nao ndani ya Chadema kwa kuwa hata Katiba ya Nchi nayo ina waruhusu kufanya hivyo.

"Nilikuwa ni Miongoni mwa Viongozi wa Chadema lakini leo narudi Ccm ili niweze kuboresha zaidi chama changu hapa kijijini na pia
nawasihi sana wananchi wenzangu hakikisheni kuwa kamwe hamuwui kwenye utawala wa vita ambao uanchangia kupata matatizo makubwa sana"aliongeza Bw Maeda.

Chanzo: GUMZO LA JIJI BLOG.
 
yaani wamevuna wanachama 150 ndani ya wiki mbili? Hiki ndio chama tawala bana hahaaa haaaa
 
Hii habari mbona ni ya zamani sana au kwenu ni mpya kilasiku, na isha letwa humu si chini ya Mara 38 hii ya leo inaweza kuwa ni mara ya 40 kuletwa humu
 
Walikuwa wanavhama wa ccm ndani ya wiki mbili wakawa chadema and then wakavunwa na ccm???
Utata mtupu!!!!!
 
Umeshavimbiwa na kideri asubuhii hii mbona hii habari ni ya siku nyingi sana au kwako ndio mpya.Kesi ya mwenyekiti wenu wa kijiji aliyekuwa ameficha silaa zilizotumika kumua mbwambo inaendeleaje?
 
Kweli kwangu ni mpya,nimeiona kwenye blog ya GUMZO LA JIJI leo,na imeandikwa ni ya tar. 28 july.
 
uwongo mtupu,mtahangaika sana...suala la kaskazini ni ndoto za mchana na ccm wanajua hilo
 
Hii habari ya muda mrefu sana! na huenda hata jamaa walisharudisha kadi za magamba baada ya kula elfu kumi kumi na hawajapewa zingine tena.
 
Mleta mada umeongeza sifuri badala ya 15 wewe umeandika 150 tafadhali sana rekebisha
 
unamweka kundi gani mtu anayepoteza kitu chake na baada ya kukipata anakiita kipya?
1.zuzu.
2.kichaa.
3.mwendawazimu.
4.chizi.
5.mbumbumbu.
6.limbukeni.
7.hamnazo.
8.kilaza

au nini?
 
Tetesi: Joshua Nassari ajiunga na magamba

Mna ndoto za mchana nyie magamba! Sijaona mkutano wa hadhara wa ccm toka baada ya uchaguzi mdogo wa Arumeru hapa Arusha! Nape tunamuonaga akizunguka kufanya mikutano kwenye masoko lakini hajafanya mkutano kwenye soko la hapa Arusha!
 
masikini wanahesabu mpaka vivuli sasa,unafikiri wanachama ni mahindi mpaka uvune kirahisi rahisi tu.hata hivyo sio vibaya kwa mgonjwa kujipa moyo hamu ya kula imerudi kwa vijiko viwili vya uji.ingawa akiwa mzima anamaliza jagi zima.
 
Back
Top Bottom