CCM mbona mnajimaliza wenyewe!!

SULWE

Member
Apr 6, 2017
90
33
Nawashukuru wadau wote kwa juhudi zenu za kusaidia serikali hii ya awamu ya tano kuhakikisha inasonga mbele kuleta maendeleo Makubwa, ipo dhamira nzuri kutoka kwa viongozi wetu, wanayo yatenda viongozi wetu yanathibisha hiyo nia njema. Lakini naomba niwakumbushe chama tawala kuwa kwa haya yafuatayo mnajimaliza wenyewe.

1: Mnawakatisha tamaa watumishi katika halmashauri zetu, kwa mfano, tokea pesa za elimu bure ianze waalimu wamesahaulika Kabisa, serikali inajali matokeo mazuri ya wanafunzi lakini hakuna mikakati kuwasaidia waalimu , Nyumba za waalimu hazifai kuishi binadamu, makato ya kodi, bodi ya mkopo,bima ya afya, CWT, Pensheni, ubabe wa wakuu wa wilaya na mengineyo mengi yanawarudisha nyuma waalimu, mwisho wa mwezi take home ni 200,000 na point, toka kwenye 500,000 ebu mtafakari ufanisi hapa.

2: Pesa za maendeleo 34 asilimia .

3:Matukio ya utekaji na vitisho Kwani vyombo vya habari na mpokimya.

4: Mgawanyiko ndani ya chamá na mpo kimya.

5: Yapo mengi ya kusema, lakini naomba nizungumzie uwakilishi wetu bunge la Afrika mashariki , naomba kuuliza kuwa chadema wasipo kuwa na uwakilishi EALA mnapata faida gani? Tanzania ikiwa na wawakilishi wachache nihasara kwa chadema au kwa serikali, kila siku mnajitanabaisha kama wasema kweli na fitina kwenu mwiko, je hii ni fitina ama?

Mwisho nauliza swala la mkuu wa mkoa Dar es alam , ndugu Paul makonda lina kigugumizi gani, kwanini isiwekwe wazi ili ukweli ijulikane?

Naomba kuwasilisha.
 
Mvua ndo hizo......., msilalamike kuna njaa wakati kucha mpo kwenye soga za matukio badala ya kuzitumia kwenye kilimo.Halafu muandamane serikali iwape chakula cha bure
 
Back
Top Bottom