Ccm mbeya yajipanga kuishinda chadema udiwani kata ya iyera mbeya mjini kijeshi

 • Thread starter Geofrey Andrew Sanga
 • Start date

G

Geofrey Andrew Sanga

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2013
Messages
251
Likes
3
Points
35
G

Geofrey Andrew Sanga

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2013
251 3 35
 • CCM yajifua kijeshi Mbeya
  • Yadaiwa kuunda kambi kwa maagizo ya Mwigulu
 • NI BAADA YA KUSHINDWA SIASA ZA MAJUKWAANI VIBAYA MNO NA UPANDE WA CHADEMA
 • NA KUONA KITI KINAENDA CHADEMA HASA BAADA YA KUDAIWA MGOMBEA WAO SI MKAZI WA KATA HIYO NA INASEMEKANA NI RAIA WA NCHI MOJA HUKO BARANI ASIA HATA KISWAHILI HAJUI KUONGEA VIZURI

  HOFU ya vitendo vya kijangili imezuka mkoani hapa baada ya kuwepo kwa tuhuma za kambi tatu zinazoendesha mafunzo ya kijeshi, zikidaiwa kuendeshwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Tuhuma hizi nzito zilizotolewa na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, zimedai kuwa kambi hizo zimeanzishwa kutokana na agizo la Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.

  Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija alisema kuwa kambi hizo zimewekwa katika shule tatu za sekondari zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM ambako vijana wa chama hicho wanapatiwa mafunzo ya kijeshi.

  Mwambigija alisema kambi hizo zilizoko Ivumwe, Itende na Igawilo, zinaendesha mafunzo hayo huku vijana wakisikika wakitamka maneno ya ‘kata kucha', ‘ng'oa meno', ‘ingiza chupa' na mengine yanayotishia usalama wa watu.

  "Tumepata taarifa kuwa vijana hao wanatekeleza maagizo yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba. Vijana hao wapo Ivumwe, Itende na Igawilo, wanatamka maneno hatarishi, wakiimba, kata kucha, ng'oa meno, ingiza chupa na mengine hatuwezi kuyataja, ni hatarishi sana," alisema Mwambigija.

  Mwenyekiti huyo alisema wamegundua kuwa hatua hiyo inalenga pia kuwatisha wananchi wasijitokeze katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Iyela jijini Mbeya unaotarajiwa kufanyika Juni 16.

  "Baada ya kufuatilia tumeona mwenendo wa mazoezi hayo una lengo la kuwatisha wapiga kura na kuwafanya wananchi waogope kujitokeza siku ya kupiga kura.

  "CHADEMA tunataka kuona uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki, na CCM walipewa muda wa kufanya kampeni, hawajafanya kiasi cha kutosha, kwa hali hiyo wasitumie mbinu nyingine ili kuvuruga uchaguzi," alisema.

  Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Kanda ya Nyanda za Juu, Lucas Mwampiki ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA Mbeya Mjini, alisema kwa kutumia mbinu za kiintelijensia walifika zilipo kambi hizo kushuhudia hamasa na mafunzo waliyokuwa wakipewa vijana hao.

  "Mafunzo na matamshi wanayopatiwa vijana hao hayana sura ya uzalendo, na sijawahi kuona wala kusikia chama kikongwe kikiwafundisha vijana wake maneno hatarishi.

  "Sisi tumetekeleza wajibu wetu baada ya kugundua kuwa kambi za wenzetu hazina lengo zuri na uchaguzi huu. Nimeongea na RPC, RCO RSO na CID na viongozi wetu wa chama ngazi ya juu ili kuwajulisha kile kinachoweza kutokea," alisema Mwampiki.

  Baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya wilaya walipohojiwa kuhusu kuwepo kwa kambi hizo, hususan muda huu wa kampeni za udiwani, walikiri na kusema wanatekeleza maagizo ya Mwigulu.

  Wakiongea kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, viongozi wawili wa CCM walisema kuwa wanajua maelekezo yaliyotolewa kuhusu mafunzo katika kambi hizo, lakini wakasema anayetakiwa kuzungumza ni Mwigulu mwenyewe.

  "Kambi zipo, lakini kwangu binafsi sielewi vijana waliowekwa kambini wanafundishwa nini, maana huko sijafika bado," alisema mmoja wa viongozi hao.

  Alipotafutwa kwa njia ya simu, Mwigulu hakuweza kupatikana kwa vile simu yake ilikuwa imezimwa wakati wote. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, bado ilionekana haijafunguliwa.

  Aidha, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Boyd Mwabulanga, alisema kuwa tangu kampeni zilipoanza wamegundua kuwepo kwa vitendo visivyoridhisha ikiwemo mbinu za kughushi shahada za kupigia kura.

  Mwabulanga alisema kuwa wanawaomba wenzao CCM kuacha kutumia mbinu chafu zenye lengo la kuwaogopesha wananchi na mikakati iliyoandaliwa ya kutumia vyombo vya dola ikiwemo kupiga mabomu ya machozi ili watu waogope na kushindwa kujitokeza siku ya upigaji kura.

  Kadhalika, alisema kuna tuhuma kwamba CCM wameanza mbinu chafu za kughushi shahada za kupigia kura maeneo ya Kabwe jijini Mbeya na kumtaja mtu mwenye mashine inayotumika kughushi.

  Pia alisema kuwa baadhi ya wajumbe wa nyumba kumi kumi (mabalozi) wa CCM wamenaswa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama, lakini siku ya pili wameshangaa kuwaona wakitamba mitaani hali ambayo inazidisha kiburi na kuonyesha dhahiri CCM wanavyotegemea polisi.

  Kauli ya RPC

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Mbeya, Diwani amekiri kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa uongozi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, na kudai kuwa wanafuatilia suala hilo.

  "Tumepata habari hizo na tunafuatilia kwa njia na mbinu zetu, na hadi sasa tunajua kuna mafunzo ya vijana wa CCM yanaendelea," alisema Kamanda Diwani.

  Hata hivyo, Kamanda Diwani alidai kuwa wanachojua ni kuwepo kwa mafunzo ya kawaida kwa vijana wa CCM, na ndiyo maana yanafanyika ndani na kwamba hayahatarishi amani na usalama.

  "Lakini bado tunawaomba CHADEMA watusaidie kufuatilia na kama watagundua tofauti na haya tunayoyajua hadi sasa, watuarifu. Kwa sasa hatuwezi kumkamata yeyote kama wanavyotaka tufanye," alisema.

  Tuhuma hizo zinakuja kukiwa na taarifa za kuvamiwa na kujeruhiwa vibaya kwa makada wa CHADEMA mkoani Arusha kunakohusishwa na kampeni za uchaguzi.

  Mapema wiki hii, kundi la vijana wanaoaminika kuwa wafuasi wa CCM walivamia mkutano wa CHADEMA na kuwajeruhi vibaya baadhi ya watu, jambo lililosababisha kuzuka kwa
 
G

Geofrey Andrew Sanga

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2013
Messages
251
Likes
3
Points
35
G

Geofrey Andrew Sanga

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2013
251 3 35
Huu si mwanzo wa ugaidi jamani?. Polisi interenjesia vipi jmeenda likizo au kazi yenu ni kupambana na chadema tu
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,408
Likes
505
Points
180
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,408 505 180
Unapoishiwa hoja lazima utumie nguvu ndo haya sasa
 
Augustine Moshi

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2006
Messages
2,319
Likes
409
Points
180
Augustine Moshi

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2006
2,319 409 180
CCM ijifunze jinsi vyama vikongwe kama KANU na UNIP vilivyokwenda benji kwa amani, kwa manufaa ya wananchi.

Kutawala kwa kutumia mbinu chafu za fujo, kuiba kura na kumwaga damu kutaleta mauti ya milele, yaani jehanamu, kwa viongozi wengi wa CCM.

In the end, when the dust has settled and time has given way to eternity, many CCM leaders will have gained some years of forced domination but lost their eternal lives.
 
T

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,335
Likes
339
Points
180
Age
28
T

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,335 339 180
 • CCM yajifua kijeshi Mbeya
  • Yadaiwa kuunda kambi kwa maagizo ya Mwigulu.....
  Mapema wiki hii, kundi la vijana wanaoaminika kuwa wafuasi wa CCM walivamia mkutano wa CHADEMA na kuwajeruhi vibaya baadhi ya watu, jambo lililosababisha kuzuka kwa
Sasa ndiyo nini umeandika.
 
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,607
Likes
13,069
Points
280
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,607 13,069 280
Wananchi wa Mbeya ni wanajeshi tangu long kitambo.
Subiri uuone mziki wao uufananishe na wa hilo jeshi kuchovya.
 
G

Geofrey Andrew Sanga

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2013
Messages
251
Likes
3
Points
35
G

Geofrey Andrew Sanga

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2013
251 3 35
we umesoma nini? kama hujui kusoma omba nikuletee picha uione
 
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
2,524
Likes
6
Points
135
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
2,524 6 135
Acha wehu wewe. Yule jamaa wa Rombo anayegombea Arusha sio mzaliwa wa kata husika mbona hujamsema.
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Chadema imeishiwa mbinu za kisiada imebaki kuchafua watu na vyombo vya dola
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Acha wehu wewe. Yule jamaa wa Rombo anayegombea Arusha sio mzaliwa wa kata husika mbona hujamsema.
Ndio zao kusomba wachaga na kuwapeleka maeneo yenye uchaguzi wakagombee. Ona lema, mnyika, mdee na kiwia
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Take it from me, CHADEMA yafa
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Huu si mwanzo wa ugaidi jamani?. Polisi interenjesia vipi jmeenda likizo au kazi yenu ni kupambana na chadema tu
Form four failure at work..interenjesia ndio nini??? Acha ugaidi na acha kutembea na sumu hadi bar
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,679
Likes
3,241
Points
280
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,679 3,241 280
Huu si mwanzo wa ugaidi jamani?. Polisi interenjesia vipi jmeenda likizo au kazi yenu ni kupambana na chadema tu
Kama nda anategemea Intelejesia ya CHADEMA. Kama hawawezi si walete FBI na hili?
 
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
8,658
Likes
5,710
Points
280
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
8,658 5,710 280
Unapoishiwa hoja lazima utumie nguvu ndo haya sasa
Wakati vyama vingi vinaingia nilikuwa Kenya. Moi na vibaraka wake walitumia uhuni kama huu kuwaogofya waliokuwa wanadai vyama vingi. Kibaraka mmoja wa Moi alisikika anawaamuru vijana wa KANU. ''Tembeeni na visu vyenu vikali, na wote wanaonyoosha vidole viwili (alama ya v kama Chadema iliyokuwa inatumiwa na wanaodai vyama vingi) mvikate, mvipeleke kwenye ofisi za Kanu kwa kumbukumbu!
 
kbosho

kbosho

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2012
Messages
12,614
Likes
3,472
Points
280
kbosho

kbosho

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2012
12,614 3,472 280
tanzania hakuna demokrasia ya kweli ni danganya toto tu....ccm nao watambuwe raia wa sasa sio wale wa miaka ya 47' pia wajuwe upuuzi wanao ufanya hautadumu na hawataweza kufanya kwa watu wote..
 
C

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
3,607
Likes
40
Points
0
C

Concrete

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
3,607 40 0
Ni wazi kata ya Iyela itakwenda CHADEMA tu.
CCM haipendwi Mbeya mjini lakini pia mgombea wa CCM ni wa ovyo kabisa.
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,408
Likes
505
Points
180
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,408 505 180
Kauli Mbiu toa meno toa kucha chinja!
Na hiki ndio chama tawala
 

Forum statistics

Threads 1,272,606
Members 490,036
Posts 30,454,959