CCM Mbeya kilichojiri chuo kikuu TEKU -Sitta+Mwakyembe walisema nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Mbeya kilichojiri chuo kikuu TEKU -Sitta+Mwakyembe walisema nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Jul 21, 2011.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0


  wakuu, nimeletewa hii kitu hebu isomeni kwa makini na haswa kuhusu maneno yaliyotumiwa na hawa viongozi halafu fanya tafakuri ya kina nini kinaendelea ndani ya CCM na taifa kwa ujumla , pia hili kundi lilikuwa linapeleka ujumbe gani kwa taifa na wanaCCM wenzao.
  KIKAO CHA CCM NA WANAVYUO MBEYA- KILICHOFANYIKA KIWIRA MOTEL 16/07/2011​

  MADA: VIJANA MUSTAKABALI WA TAIFA:
  Mwakyembe.
  -Alisema alifuatwa na chama maarufu cha upinzani nyumbani kwake na akaambiwa ahame ccm akagoma.
  -Anasema ni yeye aliyekuwa mkurugenzi wa NBC na akaiamuru ifungwe kwa miezi minne kwasababu ya ufisadi lakini kwasababu yuko imara hakuweza kubabaishwa na mtu yeyote.ndio maana ccm wanashindwa kumfukuza sababu analindwa katiba ya ccm ibara 81.

  -Anasema yeye ataendelea kubaki ccm. -Anasema amefanya mengi ya kukosoa chama lakini bado hakufukuzwa ccm, na atabaki ccm .

  Samweli Sita.
  -Chama chetu kiliota gamba nami nikiwemo serekalini, kwahiyo ndugu wanachuo na wanafunzi tunaomba radhi.-Tumefika pabaya mpaka chama cha CHADEMA/ upinzani ndio wanamnukuu baba wa Taifa na kuiga baadhi ya matendo yake.
  -Chama cha mapinduzi ndicho kinachostahili kujenga Taifa hili nasio chama kingine.-Chama chochote cha siasa hususani ccm lazima kiwe na mizizi mirefu.
  -Baadhi ya wenzetu ndio waliotupoteza .
  -Nikiwa ndani ya kikao cha nec nilishangaa baadhi ya watu wanataka nirudishe kadi yaani watu ambao wameota magamba(mafisadi).
  -Aliendelea kukiri kuwa vita yao ambayo wanapigana sasa ni ngumu sana kwa kuwa wao ni wengi watashinda tu.
  -Mkoa wa Mbeya unatosha kuitwa nchi kwani unajitosheleza kwa kuwa una -Kilimo -Maji -Rasilmali(madini)
  -Wamepanga kuanza mradi mkubwa wa kilimo utakaoanzia Tunduma hadi morogoro.
  -Akasema inashangaza kuna hekari 20, za maua Arusha kwa Tanzania nzima lakini Kenya wana hekari 100. lakini mbeya pekee yaweza kuwa na hekari 600 za maua.
  -Akasema ccm inaweza kuwa matajri mpaka kujenga maghorofa kama chama cha ANC kama tutatokomeza mafisadi
  -Wapinzani wanachekelea kwakuwa tunamatatizo kibao. Nani aliwaambia kuna kusoma bure? wanakufulu hata vitabu vya mwenyezi Mungu hakuna kitu cha bure. Huo ni upuuzi tu.

  Nape Nauye
  -Dr Slaa anang’ang’ania mke asiye wake, kwani mwenye mke yuko ikulu. Kwahiyo yeye akang’ang’ania siatakuwa kibaka
  -Chadema hawana huruma (ni baba wa kambo kwani wanawadanganya watu tuandamane ili msipate muda wa kufanya kazi, kwani wao wamepata pesa na kuishi kwenye viyoyozi.
  -Akasema kuna mtu Zanzibari (makamu wa kwanza wa Rais –Seif) alikuwa mbishi lakini tulipomwambia ukikubali mapinduzi sisi tutakulipa, basi tukamlipa ndio maana anapendeza na tukamtunza kama waziri, kiongozi mstaafu wa serikali ya mapinduzi, akasema lakini chadema ni chama cha msimu tu. Ambacho nacho wataacha na watapotea tu.

  Mary Mwanjelwa.-Tuimarishe chama chetu cha mapinduzi .

  Ole sendeka.-Waliwaambia vijana kuwa umefika wakati wa kupeana zamu za uongozi na vijana.

  Nyalandu.
  -Lazara aliongelea kuwa maisha yanakusudi kwamba kijana lazima uwe na kusudi la maisha yako .-Akawaambia vijana hasa wanachuo kuwa ndio rasilimali ya taifa.
  -Akaendelea akisema kwamba kila mwanadamu anauwezo mkubwa lakini huwa anatumia 10% tu ya uwezo wake.
  -Akasema vijana wa CCM wana mashaka hata wanaogopa kuvaa nguo za CCM.
  -Alikiri kuwa ndani ya CCM kuna watu wanokiharibu chama akasema watawashughulikia wanao kiharibu chama cha mapinduzi.
  -Aliwaambia wanachuo wafikirie juu ya Tanzania yao.

  Hitimisho.

  -Hata hivyo vyuoni wakuu wa vyuo bila aibu wanawatishia wana vyuo, wafanyakazi, kuwa hatutamaliza vyuo kwani watatufukuza, wanasema tuhamie CCM Lakin mwalimu mmoja Allawi Dean of student ndiye aliyefanya kazi kuhakikisha mkutano na wanavyuo unafanikiwa kati ya viongozi hao wa CCM na wanachuo wa Teku Mbeya ikiwa ni pamoja na kutumia Serikali ya chuo yaani TEKUSO, kufanikisha kufanyika kwa semina ya CCM.

  Mytake ; Vita ni kubwa sana ndani ya CCM na waasisi wa CCJ hawako tayari kurudi nyuma na wanajua kuwa kama hawatapata mtu wao kugombea na ama kushinda Urais watakuwa kwenye wakati mgumu sana hivyo hali ni mbaya ndani ya CCM .
   
 2. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu ili taarifa iwe reasonable basi uwe unaweka source ya habaro vinginevyo haina maana kuweka tarifa kama hii..Nape ovyo yeye kawapa mimba wasichana wangapi? Muuaji mkubwa tu huyo..
   
 3. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hiki Chama Kinachoongozwa Majambazi Kitakufa lini? Nakichukia sana
   
 4. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Tunaomba uthibitisho toka kwenu wanateku kama hayo ni kweli ili tuanze kuchangia.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Magamba in action! kumbe hata 6 ka-develop gamba gumu la ccj!
   
 6. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kweli siasa za wanadamu na utumishi wa shetani ni pete na kidole.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  kwavile kilikua na mwanzo mwisho lazima upo na ushaanzakuonekana tumwombe MUNGU tu tutaikomboa nchi yetu kwakupata uhuru rasmi kwani uliopo ni uhuru kivuli
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata kama cdm kitakua chama cha msimu ila kinawatoa jasho mpaka kila viongozi wa CCM Wakilala kwenye ndoto wanakiota
   
 9. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Magamba hayawezi kwisha kwani ni mengi mno yanatofautiana ukubwa tu. Na kama ikitokea muujiza wakayamaliza, basi aidha joka hilo litakosa ulinzi wa mwili litakufa hata kwa jua tu, ama lita anza kujiparura mabaki ya CCJ. kifupi lazima mnyama afe tu.
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Lazima wawe makini kwani tayari Malawi wameanza masuala ya mke wa mtu na siasa ambazo hazina ukweli ztatufikisha huko NAPE ana bore mno sasa anawaudhi Wa- Z'bar Shariff siyo size yake anapaswa kumuuliza nini cha kufanya ktk siasa za TZ
   
 11. M

  MAURIN Senior Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni chama cha majambazi na wasio kuwa na fikra njema na watu wenye kuwaza kutumia makamasi akili wakiwa wamezifungia kabatini.
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna mtu anajua kwamba walipokuwa kyela maeneo ya Ipinda walifukuzwa Mwakyembe akiitwa msanii yani Joti wakakimbia kila mtu njia yake wakaenda kukutana Kiwira hoteli mengi hajaandikwa kwenye magazeti haikuwa smooth trip waoha kama nini Mbeya mjini mpaka RPC alikuwa doria ha ha chama cha magamba wanakazi
  Sijasikia CUF wakilizungumzia swala la NAPE kumuita Katibu mkuu wa chama cha CUF amekwenda ikulu kwa ajili ya njaa ,je wananchi tuamini hvyo
   
Loading...