CCM Mara wapasuka...........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Gazeti La Mtanzania ambalo ni maarufu kwa kukipamba Chama Cha Mapinduzi safari hii naona uzalendo umeshindikana na wamebidi kutupasha habari juu ya mpasuko mkubwa ndani ya Chama hicho mara baada ya uchaguzi..............katika Mkoa wa Mara...........

Majeraha hayo yamesababisha madiwani wengi wa chama hicho kudhamiria kujjiengua na kujiunga na upinzani..........................
 
Mkuu, Ruta.
Mara nyingi unapata habari lakini unazitoa hapa kwa mstari mmoja tu , hii inasababisha mtu ambaye hana access na hiyo habari (hasa magazeti) ashindwe kuchangia maana hana habari kamili.
Ombi kwako, kama unaweza, uwe unabandika hiyo habari / article watu waipitie.
Asante
 
ukiona hivyo wanapingana na maamuzi ya viongozi wa ccm mkoa na yawezekana bosi wao anamkono kwenye huo mpasuko
 
Mkuu, Ruta.
Mara nyingi unapata habari lakini unazitoa hapa kwa mstari mmoja tu , hii inasababisha mtu ambaye hana access na hiyo habari (hasa magazeti) ashindwe kuchangia maana hana habari kamili.
Ombi kwako, kama unaweza, uwe unabandika hiyo habari / article watu waipitie.
Asante

Wakati mwingine tunawapunguzia muda wa kusoma habari ndefu.............................lakini point taken...................
 
Kwa kifupi muhariri wa gazeti la mtanzania sasa hivi ni mwingine,anaitwa (danny mwakiteleko) nadhani huyu anaakili timamu tofauti na yule wa mwanzo(muhingo rweyemamu)
 
chanzo cha mpasuko ni kuenguliwa majina ya madiwani wanaogombea umeya, kamati ya siasa mkoa chini ya makongoro imepitisha majina yao, madiwani zaidi ya 40 wametishia kujiunga ktk vyama makini (upinzani)
 
Wilaya mpya ya Rorya imechagua wezi na majambazi watupu kwenye UDIWANI na UBUNGE. Wanalindana kwelikweli, wanataka washike nafasi zote nyeti kwenye wilaya ile. CCM ni kokoro bwana!
 
Mara nyingi CCM wakipoteza jimbo kinachofuata ni mtafaruku wa uongozi, kuaminiana hupungua. Inaweza ikawa hivyo na vyama vingine pia. Sasa kwa Musoma nadhani iko shughuli hasa ukizingatia mwenyekiti wa CCM mkoa ana uhusiano wa karibu na mbunge wa upinzani aliyeshinda. Haitakuwa rahisi kwake, kazi anayo.
 
Tatizo liko Rorya ambako Kamati ya Siasa (CCM) ya Mkoa inavutana na Kamati ya Siasa ya Wilaya kuhusu nani agombee Uenyekiti wa Halmashauri ya wilaya mpya ya Rorya. Mbunge mpya wa Jimbo hili Lameck Airo ana nguvu na ushawishi mkubwa mno na anataka kupanga safu ya Uongozi anaoutaka yeye.
 
ni kweli mkuu, tatizo ni kukatwa jina la mwenyekiti aliepita Chales obutu ochele (ambaye ni mpambe wa karibu wa lameck airo) pamoja na diwani shirati Ongujo ambao wana kuhasama pamoja na nguvu ya fedha, hivyo basi ili kuondoa mpasuko ikabidi kamati ya mkoa ikate majina yote mawili na kubakiza jina la diwani wa nyahingo na wa nyamtinga
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom