CCM Mara: Bulembo aliiuza Shule ya wazazi Isango saa 2 usiku kwa milioni 70

Wakati mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Wazazi ukiendelea, alisimama Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mrida Marocha aliyemtaja Abdallah Bulembo kuwa yeye na kundi lake walishiriki kuiuza Sekondari ya Isango. Alisema walifanya hivyo saa mbili usiku kwa bei ya Sh70 milioni.

Marocha alisema shule hiyo alikabidhiwa Mwalimu Nyerere na wakoloni maalumu kwa ajili ya wasichana na alitumia nafasi yake kuwapa wazazi, lakini wachache waliiuza na kugawana.

“Shule ile ndiyo alisoma Gaudencia Kabaka (mwenyekiti wa UWT Taifa), Bulembo namtaja hata kama ana watu wake hapa wakamwambie, aliyeichukua ameanza kuipaka rangi,” alisema Marocha.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dk Edmund Mndolwa alikiri kuwa na taarifa za mgogoro wa Shule ya Isango, akisema kuna wakati alikaa hapo hadi usiku lakini mgogoro wake ni mkubwa.

Akijibu tuhuma hizo, Bulembo alisema “muulize huyo (Marocha) aliingia lini kwenye chama kama si mwaka wa tano huu, hajui chochote, nimehangaika na shule hiyo kwa miaka minne Mahakama Kuu nikitaka kuinasua kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa Musoma, mimi hata niliposhika nafasi ya mwenyekiti nilikuwa natokea Mara kwa hiyo nayajua mengi.”

Bulembo alisema Marocha hajui historia zaidi ya kuibukia kwenye uongozi na kutaka aseme ili asikike, huku akieleza kuwa yeye (Bulembo) ni mstaafu anayeweza kuwa na udhaifu lakini hauhusu uuzaji wa shule za jumuiya.

Nyerere alikuwa anawachangisha wa TZ kukijenga chama Leo hii vijana wanauza Mali hizo Kwa Bei Chee kabisa
 
Back
Top Bottom