CCM Mambo yazidi kuwa Magumu: Ni kuhusu rasimu ya katiba mpya

Aliyezungumzia ukosefu wa dira si nyerere bana ni Kolimba wewe kila kitu nyerere aisee..

Kweli mabadiliko haya yalitakiwa yaanze enzi za kolimba wameahirisha hadi leo, lakini ni vizuri kwa nchi yetu wacha vyama vya upinzani navyo vikue..ccm ikiwa very powefull ni hatari kwa Taifa..
We Topical nini wewe? Nyerere alilizungumzia hilo kabla hata ya Kolimba. Ninayo hotuba kwenye cd unabisha bure. Hata ukisikiliza hotuba aliyoitoa Singida mwaka 1986 alianza kuzungumzia ukosefu wa mwelekeo ndani ya CCM, na hii ilikuwa kabla ya azimio la Zanzibar.
 
Aisee sawa mkuu,

Kolimba view ilikuwa sahihi sana lakini ccm kwa ukaidi wanaongoza; ngoja tuone haya mabadiliko yatawasaidia nini?
 
We Topical nini wewe? Nyerere alilizungumzia hilo kabla hata ya Kolimba. Ninayo hotuba kwenye cd unabisha bure. Hata ukisikiliza hotuba aliyoitoa Singida mwaka 1986 alianza kuzungumzia ukosefu wa mwelekeo ndani ya CCM, na hii ilikuwa kabla ya azimio la Zanzibar.

ni kweli Nyerere alizungumzia hata kabla nchi hii haijawa na tv wala fm radio.
 
Mchambuzi,
Unajua CCM wanatakiwa kukaa na ufikiria Upya na sii kujaribu kupanga vyeo wakati chama tayario kimeisha poteza Dira.. Mimi nawaomba wao wajitazame kwanza na wafikirie wanachoamini nna matendo yao maana ukisikia KUFURU ikisemwa basi CCM wanaifanya kila siku.. Ebu soma maelezo haya ya huyu kinogzi wa chama anavyozungumzia siasa yao ya UJAMAA na KUJITEGEMEA halafu itazame hali halisi.. Kama wanashindwa huko kwenye msingi wa chama hivi kweli kugawana hizi nafasi ndio kutasaidia kitu..

Makala yenyewe hii hapa - mimi naona NYEKUNDU tupu yaani ukisikia Unafiki basi hakuna zaidi ya huu..

Mwandishi wa Makala hii ni Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Ndugu Omar R. Mapuri ambaye katika toleo lijalo la jarida hili atamalizia Makala yake kwa kueleza juu ya:-Baadhi ya maeneo yaliyohitaji marekebisho ya Sera

UJAMAA NA KUJITEGEMEA KAMA SIASA YA CHAMA:
Kama siasa ya Chama, Ujamaa na Kujitegemea ni lengo la kudumu. Ni kwa msingi huo ndiyo tunasema kwamba Chama Cha Mapinduzi bado kabisa hakijaachana na siasa hiyo. Katiba na sera za CCM zinabainisha wazi wazi msimamo huo kama ilivyokwisha elezewa. Baada ya kuuelewa msimamo huo, ni muhimu pia kuelewa tunapozungumzia Ujamaa na Kujitegemea tunakusudia nini. Tutajaribu kwa kutumia lugha nyepesi kabisa, kutoa ufafanuzi huo katika sehemu hii ya makala haya. Kama inavyojieleza yenyewe, siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ina ncha mbili, yaani ya Ujamaa na ile ya Kujitegemea. Katika Azimio la Arusha, umefanywa uchanganuzi wa kina ambapo Sehemu ya Pili ya Azimio hilo inachambua Siasa ya Ujamaa na Sehemu ya Tatu inachambua Siasa ya Kujitegemea. Kwa maneno mengine siasa yetu hii ni siasa mbili ndani ya moja. Nasi kwa ufupi kabisa tutafanya uchanganuzi kama huo.

Siasa ya Ujamaa:
Siasa ya Ujamaa imechambuliwa na wanafalsafa wengi wakubwa waDunia hii wakiongozwa na Karl Marx na Vladmir Lenin. Pia imechambuliwa kwa kina na Mwalimu Julius K. Nyerere kwa mazingira ya Tanzania katika vitabu vyake mbali mbali, ambapo majumuisho yake yaliwekwa katika Azimio la Arusha. Sisi katika makala haya hatukusudii kurejea uchambuzi wa kifalsafa bali tu tunajaribu kumwelezea mwananchi wa kawaida maana pana na nyepesi inayokusudiwa katika Siasa ya Ujamaa. Kwetu sisi Ujamaa maana yake ni kugawana utajiri wa nchi kwa usawa na kwa haki katika misingi ya kuheshimiana.

Jitihada zetu za kiutekelezaji katika kufikia lengo hilo kama zinavyoongozwa na Azimio la Arusha zimekuwa zikichukua sura za kusambaza huduma za jamii (elimu, afya, maji n.k.) kwa wote, kujenga misingi ya fursa sawa za kujiendeleza, kuondoa unyonyaji, kupiga vita kila aina ya ubaguzi na dharau, kuwatetea wanyonge na kuwasaidia kujikwamua na kadhalika. Uamuzi wa kuanzisha vijiji vya ujamaa katika miaka ya sabini ulikuwa na lengo la kurahisisha utekelezaji wa juhudi hizi. Pamoja na matatizo ya hapa na pale ya utekelezaji, tunaamini Watanzania walio wengi hasa wanyonge, bado wanapenda kufikiwa kwa malengo hayo. Ndiyo maana tunasema Siasa ya Ujamaa ni ya kudumu.
Kugawana au kusambaza kwa wote utajiri wa nchi (si kwa kugawana fedha bali kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wote) ni sura moja tu ya Ujamaa. Lakini pia kuna sura ya pili ambayo ni ya kuuchuma huo utajiri wenyewe wa kugawana. Katika Azimio la Arusha, unafafanuliwa utaratibu wa kuchuma utajiri bila ya kunyonyana. Mkakati uliowekwa ni wa njia kuu za uchumi wa nchi kuwekwa chini ya wakulima na wafanyakazi kupitia vyombo vya Serikali

Siasa ya Kujitegemea:
Siasa ya Kujitegemea imechambuliwa kwa kina katika Sehemu ya Tatu ya Azimio la Arusha. Siasa hii inajikita katika kuleta maendeleo ya kweli ya nchi na ya wananchi wenyewe hasa wanyonge. Hoja inajengwa kwamba huwezi kuzungumzia maendeleo ya kweli kama maendeleo hayo ni ya vitu tu na si ya watu wenyewe na kama maendeleo hayo yamejengwa juu ya msingi wa utegemezi wa fadhila za nje. Inasisitizwa kwamba fedha si msingi wa maendeleo bali ni matokeo ya maendeleo. Kwa hivyo mkakati unaotiliwa mkazo ni wa kujituma katika kujiletea maendeleo bila ya kusubiri fedha kwanza au misaada na mikopo kutoka nje. Vitu hivyo kama vitapatikana vije tu kusaidia juhudi zetu za kujitegemea na kamwe visiruhusiwe kuhatarisha uhuru wetu.

Kwa mnasaba huo, Siasa ya Kujitegemea inasisitiza kwamba: Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha. Fedha ni matokeo siyo msingi wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji vitu vinne: (i) Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa safi na (iv) Uongozi bora. Kwa kuzingatia ukweli kwamba nchi yetu ina watu wengi na eneo kubwa la ardhi, mkakati wa siasa ya kujitegemea unabainisha kwamba maendeleo yataletwa na kilimo na hivyo pia unamjali zaidi mkulima vijijini.

Siasa ya Kujitegemea imebainisha masharti mawili ya maendeleo. Masharti hayo ni Juhudi na Maarifa. Juhudi inaashiria kufanya kazi kwa kujituma na Maarifa ni kiashirio cha matumizi ya utaalamu na teknolojia kwa lengo la kuziongezea tija juhudi.
Kwa jumla, mtu hahitaji utafiti wa kina kubaini kwamba karibu yote yaliyoelezewa kuhusiana na Siasa ya Kujitegemea yalikuwa na ukweli mwaka 1967 na bado yana ukweli hadi leo. Aidha, yote hayo yanaendelea kupendwa na Watanzania walio wengi ambao siyo tu wameyakubali, bali pia wanajitahidi kuyatekeleza. Kwa mfano Watanzania pamoja na unyonge wao, hawakubali kuonewa wala kunyanyaswa. Pia, Watanzania wamejiletea maendeleo mengi (shule, zahanati, visima, njia, maji n.k.) kwa kujitegemea bila ya kusubiri fedha. Na zaidi ya yote, Watanzania wanajituma kwa bidii kubwa. Kwa kuzingatia ukweli huo, mtu hapaswi kupata taabu sana kuelewa kwa nini Siasa ya Kujitegemea inaendelea kuwa siasa ya CCM.

Kama ilivyo katika siasa ya ujamaa, bila shaka yamejitokeza hapa na pale matatizo ya kiutekelezaji. Yapo matatizo yaliyo nje ya uwezo wetu kama vile matatizo ya kiuchumi ya dunia ambayo yalipotukumba na sisi yaliathiri utekelezaji wetu. Lakini pia yapo matatizo yaliyotokana na kasoro zetu wenyewe kama vile kuweka mkazo mdogo katika maarifa na badala yake kukazania tu juhudi ambapo matokeo yake yamekuwa ni tija ndogo katika uzalishaji hasa katika kilimo. Maeneo kama haya ya matatizo na kasoro ndiyo yanayotoa fursa ya kuzipitia upya baadhi ya sera za Chama kama tutakavyobainisha baadaye.
 
Mkuu,
Hii ni makala ya lini? Mapuri alikuwa katibu mwenezi miaka ya nyuma sana, wakati wa Mkapa, baadae akapelekwa China kuwa Balozi. be what it may, nakubaliana na wewe kuhusu CCM kukosa dira na kuendesha siasa za kujichanganya. Huyu mwandisha anaongelea azimio la arusha kwa maana ipi wakati azimio linalotawala sasa ni lile la zanzibar? Na kuhusu masuala ya kugawa utajiri kwa wananchi, kuinua kilimo, mambo haya wakiyatamka majukwaani kwa kweli watajitafutia kupigwa mawe, kweli kabisa kwasababu katika mazingira ya leo ya CCM na jinsi inavyoendesha uchumi wa nchi hii na kupelekea watanzania wengi kuwa watumwa na mafukara katika nchi yao iliyojaa kila aina ya rasilimali, maneno mengi uliyoya highlight rangi nyekundu ni maneno yanayotia hasira na uchungu sana, kwani ni kama kusanifu tu maskini wa nchi hii. Nimeshtuka sana kuona huyo Mapuri akijitahidi kutetea kitu ambacho hakipo. Sijui viongozi wa CCM huwa wanaingiwa na wazimu gani. Hata Nape miezi kadhaa iliyopita alijibu maneno kama hayo hayo kwenye mdahalo alipoulizwa CCM inafuata itikadi gani. Binafsi nilishtuka na sikuelewa kabisa mtu mwenye upeo kama wake anasukumwa na nini kutetea itikadi ya ujamaa wa Marx-Lenin, nyakati hizi.
 
Ndugu yangu Mchambuzi,

Naweza kukubaliana na hoja zako, lakini mabadiliko haya ya Katiba sioni kama kinaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa mafisadi ambao wanataka kuingia Ikulu kwa njia yoyote ile.

Chaguzi za ndani za CCM kwa ngazi za Wilaya na Mikoa, zimekuwa zikiendeshwa kwa mfumo huu huu, na bado mafisadi hao hao walifanikiwa kupanga safu ya uongozi kuanzia ngazi ya Wilaya mpaka Mkoa. Sasa ni kipi kitawashinda leo hii kupata mjumbe wa NEC kwenye ngazi ya wilaya?

Iwapo kwenye Kura za Maoni watu wanahongwa shilingi elfu 5 au 10, na kutoa kura kwa mgombea, leo hii ndio watashindwa kuwahonga wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ambao wanamchagua mjumbe mmoja wa NEC?

Mfumo wa Uhongaji ndani ya CCM hauhitaji uwepo wa mhusika mkuu, bali ni swala la mhusika mkuu kutafuta mtu wake na kuhakikisha kwamba anasimamia kila kitu ili kuhakikisha kwamba mgombea wao anashinda.

Hoja ya TAKUKURU naomba wala usiingize. Jiulize, ni wangapi ambao walishikwa wakihonga kwenye kura za maoni za 2010 kwa upande wa CCM? Je, kesi ngapi zilipelekwa mahakamani? Wapo walioshikwa na ushahidi wa wazi kabisa, lakini waliachwa wakapeta. Kesi pekee ninayoikumbuka ilikuwa ni ya Mwakalebela ambaye alipambana na Mwanamtandao Mama Monica Mbega. Mimi binafsi sina imani na Polisi wala TAKUKURU kwa kuwa wanafanya kazi kwa kuangalia nani anahusika na yuko kundi gani. Unakumbuka kesi ya yule mama wa Moshi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya mkoani Kigoma? Kamanda wa PCCB alijikuta akihamishwa ghafla mara sakata hilo liliporipotiwa, kwanini?

Lowassa bado ana nguvu sana ndani ya PCCB na Jeshi la Polisi, na ndio maana issues zote zinazomgusa Lowassa au vijana wake wa UVCCM, polisi na PCCB huwa wako makini sana katika kuzi-handle. Bado CCM yenyewe inamgwaya Lowassa, na sijui ni kwanini inamgwaya na hilo ndio linampa nguvu zaidi.

Uchaguzi wa ndani wa CCM wa mwaka 2007, kuna watu walikuwa wanatumia jina Kikwete kama kete ya kuchaguliwa, kwamba mimi ndio chaguo la Kikwete so, nipeni kura na walishinda. Kwa jinsi mambo yalivyo ndani ya CCM sasa hivi, usije ukashangaa watu wanaanza kutumia jina la Lowassa ili washinde uchaguzi wa ndani na hao hao ndio ambao watakuja kuiangamiza CCM.

Kuonyesha ni jinsi gani CCM inamgwaya Lowassa, wale vijana waliokusanyika Dodoma kwenye kikao cha CC na NEC mara baada ya uchaguzi wa Igunga, walichukuliwa hatua gani? Kikwete alikuwa na details zote za mkusanyiko wa vijana kutoka mikoa yote ya Tanzania na kwamba walilipiwa nauli kuja Dodoma, na malazi na gharama nyinginezo za kuwepo kwao Dodoma. Je, Kikwete na CC waliwafanya nini? Wassira na Lukuvi waliishia kumsema Malisa bila kuchukua hatua yoyote.

Hali hiyo kwa jinsi inavyoendelea kuachwa ndiyo inawapa kiburi Lowassa na kundi lake. So, wale wote ambao hawakuwa kambi ya Lowassa, wataona kwamba huyu ndo mbabe so ukikaa kwenye kundi lake hakuna mtu atakugusa, iwe ni Kamati ya Maadili ya CCM, Jeshi la Polisi, au PCCB. Wale vijana wa Arusha walipofungua matawi na kufanya mikutano yao bila kibali cha Jeshi la Polisi, walifanywa nini?

Hii ngoma bado ni nzito, tatizo ni kwamba uongozi wa chama hautaki kwenda kwenye kiini cha tatizo ili kuweza kulitatua, wanaendelea kuzunguka tu na mwisho wake ni kwamba kansa inaendelea kusambaa.

Keil,

Nakubaliana na hoja zako nyingi kimsingi. Hoja yangu ilikuwa tu kwamba, mabadiliko haya yatapunguza kasi ya wote wanaowania Urais kupitia ticket ya CCM, kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mfano, ili jina lako liwe na nguvu katika vikao vya uteuzi wa wagombea, ni muhimu sana pia wewe mwenyewe kama mgombea Urais, uwe mjumbe wa NEC na pia uwe na watu wako kwenye NEC na kamati kuu, kwani hivi ndio vikao vya maamuzi na vya kukata/kupitisha majina. Lakini chini ya mabadiliko haya, ina maana kwanza, mawaziri wote automatically hawataweza kugombea NEC kwasababu ujumbe wa NEC kuanzia mwaka huu ni full time job. Pili wabunge waliokuwa na influence ndani ya NEC na Kamati kuu, ambao walikuwa ni wapiga debe wa wagombea mbalimbali, hawatakuwepo tena katika NEC. Kwa maana hiyo, inabidi wale wote wanaowania Urais wajipange na safu yao mpya, hasa huko wilayani ambako wajumbe wengi (221) ndiko watakapotokea.

Kwa mtazamo wako, ikizingatiwa kwamba mabadiliko haya yamelenga kuvunja nguvu ya wagombea fulani fulani, unadhani itakuwa rahisi kiasi hicho kwa wagombea Urais 2015 kushindana na mikakati ya chama, na kuamua kuzunguka nchi kukusanya wajumbe wa NEC kutoka huko wilayani, bila ya mbinu zao kuonekana wazi? Kwani hatujui wahusika wa mabadiliko hayo ya CCM wamejipanga vipi kukabiliana na hilo, na nina uhakika watahakikisha mabadiliko waliyofanya yanaleta ufanisi wanaoutarajia.

Na je, kwa mtazamo wako, wagombea hawa wa urais kupitia tiketi ya CCM 2015, unadhani bado watakuwa na nguvu kubwa katika vikao vya maamuzi iwapo wao wenyewe wataacha kuwa wajumbe wa NEC na kubakia wabunge tu? Ubunge pekee hautoshi kukupa profile nzuri ya kuteuliwa 2015, bali ujumbe wa NEC.

Nadhani unachotaka kusema ni kwamba kutokana na nguvu ya fedha ya wagombea fulani fulani, watafanikiwa kuruka vizingiti vyote hivi. Mtazamo wangu ni kwamba, ndio watajaribu lakini walioamua kufanya mabadiliko haya hawataachia nguvu ya pesa ipelekee mabadiliko waliyokusudia yaonekane ni kazi bure. Pia pamoja na pesa kuweza kushinda vikwazo hivi, ni dhahiri kwamba equation yote imebadilika na itabidi wagombea hao wa urais wajipange kweli kweli, hasa ukizingatia kwamba mabadiliko haya yamelenga kuwapunguza spidi yao, na nina uhakika kina Nape and group, have other options on the table, to make sure wagombea wote ambao hawawataki, hawatafanikiwa.

Na kuhusu suala la pesa na Urais, kwa mtazamo wangu, wagombea wote watatumia pesa nyingi sana, watachopishana ni viwango tu, kwahiyo sio sahihi sana kwa mtu kujenga hoja kwamba mabadiliko haya yamemlenga mtu mmoja au yatamwathiri mtu mmoja. Kazi ipo.
 
Mkuu Mchambuzi unajua wewe ni kati ya wana CCM wachache unayekemea na kupinga vitendo vya rushwa lakini wana CCM wengi kuanzia ngazi ya chini mpaka juu,rushwa ni sehemu ya maisha yao.

Unajua tatizo ni kwamba, chini ya mfumo wa chama kimoja, uongozi wa CCM ulikuwa ni ajira, katika ngazi zote na posho na mishahara ilikuwa inalipwa. Lakini kuanzia mwaka 1992 (vyama vingi viliporuhusiwa), utaratibu mpya ukaweka wazi kwamba kuanzia sasa, shughuli zote za chama zitakuwa ni za kujitolea, except kwenye nafasi chache sana, hasa kuanzia ngazi ya wilaya kwa nafasi za utendaji pekee (makatibu), sio wenyeviti. Baada ya uamuzi huu kutolewa, Chama kikawapa uhuru viongozi wote wa kujitolea katika ngazi zote, kujitafutia hela kwa njia wanazojua wenyewe kuendesha vikao, shughuli za chama n.k, kwani Chama hakina tena hela ya kufanikisha hayo. Hapo ndipo dirisha la rushwa na ufisadi likafunguliwa rasmi, na ni vigumu sana kwa CCM kulifunga dirisha hili, hasa kwa kuzingatia kwamba hiyo ndiyo njia pekee ya viongozi hawa kuishi baada ya posho na mishahara kufutwa tangia mwaka 1992. Wakilifunga dirisha hili maana yake ni kwamba nafasi za uongozi hasa huko ngazi za chini hazitakuwa na mvuto tena kuzigombea, na hii itakuwa ni hatari kwa chama, kwani wanachama wa CCM wapo kwenye matawi, sio wilayani, mikoani wala taifa. Nguvu ya CCM ni matawi.
 
Ni vigumu sana kuwahonga wanachama wilayani. Composition ya wajumbe wa wilayani is more scattered kuliko ya mikoani.
Naufagilia sana huu uamuzi...... JK kammaliza EL kiaina.
 
Kupona kwa Tanzania katika hali mbovu tuliyonayo sasa, basi tuombe Mungu chama kilichopo madarakani eidha kikatike au kitoke madarakani walau hata kwa kipindi kimoja cha uongozi. Eeh Mola saidia hili.
 
Lowassa kama mtu haogopwi hatishi na haogopwi hata n nzi tu.
Fedha yake Lowassa ndiyo inayoogopwa na hata kusujudiwa.
Ile kashfa ya Richmond Wizi wa Bank Kuu na Madudu engine ndani ya serikali yana mkono wa Lowassa.

Lowassa ndiye aliye kuwa akikusanya malipo yote ya Richmond na Baadaye Dowans.
Lowassa ndiye kiongozi wa kwanzawa ngazi ya juu ndani ya serikali ya CCM kuibamamilioni ya fedha huu akilindwa na Polisi, Jeshi, Usalama wa Taifa,Ikulu na Takukuru.

Lowassaa anataka U rais wa Tanzania hata gharama yake ikiwa ni kuibinafsisha serikali.

Fedha aliyoikomba kutoka hazina ya Taifa sasa anapita nayo kwenye kila Usharika na Kigango na kuwanunua waumini kwa kile akiitacho mchango wa harambee ya kanisa huku yeye binafsi akitoa mamilioni ya fedha za wizi kuwanasa. Wachngaji kupewa mamilioni ya wizi kujikimu.

Makanisa siku zote ni kama shimo la maji taka.

Yanapinga wizi lakini yanpokea fedha kutoka kwa wezi kama Lowassa.
Makanisa;
Yanapinga wauaji na majambazi lakini jambazi akitoa mchango mnene unapokelewa unapigwa busu na kubarikiwa kwa nguvu zote.

Yanapinga ulevi umalaya na uasherati lakini yanapokea fedha kutoka kwenye madangulo na club za pombe. Yanahubiri Amani Haki na Upendo lakini siku zote yanafungamanana madikteta waujaji na wavunjaji wa haki za binadamu,wene mdangulo na biashara za malaya.wchungaji ni malaya namba moja na wazinzi wakubwa. hutembea na wake za watu wachumba wa watu wazi wazi.

Yanapinga ushoga lakini wachungaji wengi ni mashoga(Mabasha) wanatembea na watu wa jinsia yao, wanatembea na vijana wadogo, wanabaka vijana wadogo kinyume na maumbile yao.

Ndiyo maana baada ya mapinduzi ya nchi nyingi Maaskafu mashemazi na wachungaaji wengi hujikuta wakiingia mitimi kuponya nafsi zao kwa sababu ya kushiriki kwao katika uovu.

Lowassa amaechagua kanisa katika kueneza sumu yake ili ingie Ikulu.

Ole wako Edward Lowassa siku inakuja ambayo utatamani kwamba hukuzaliwa kabisa.
Magugu unayo yapanda utayavuna na kuyaweka gharani hata punje ya mwisho.

"Lowassa bado ana nguvu sana ndani ya PCCB na Jeshi la Polisi, na ndio maana issues zote zinazomgusa Lowassa au vijana wake wa UVCCM, polisi na PCCB huwa wako makini sana katika kuzi-handle. Bado CCM yenyewe inamgwaya Lowassa, na sijui ni kwanini inamgwaya na hilo ndio linampa nguvu zaidi.
"
 
Keil,

Nakubaliana na hoja zako nyingi kimsingi. Hoja yangu ilikuwa tu kwamba, mabadiliko haya yatapunguza kasi ya wote wanaowania Urais kupitia ticket ya CCM, kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mfano, ili jina lako liwe na nguvu katika vikao vya uteuzi wa wagombea, ni muhimu sana pia wewe mwenyewe kama mgombea Urais, uwe mjumbe wa NEC na pia uwe na watu wako kwenye NEC na kamati kuu, kwani hivi ndio vikao vya maamuzi na vya kukata/kupitisha majina. Lakini chini ya mabadiliko haya, ina maana kwanza, mawaziri wote automatically hawataweza kugombea NEC kwasababu ujumbe wa NEC kuanzia mwaka huu ni full time job. Pili wabunge waliokuwa na influence ndani ya NEC na Kamati kuu, ambao walikuwa ni wapiga debe wa wagombea mbalimbali, hawatakuwepo tena katika NEC. Kwa maana hiyo, inabidi wale wote wanaowania Urais wajipange na safu yao mpya, hasa huko wilayani ambako wajumbe wengi (221) ndiko watakapotokea.

Mkuu Mchambuzi,

Nimechukua hiyo para ya kwanza tu ili tuweze kuijadili kwa marefu na mapana dhana nzima ya haya mabadiliko. Wajumbe wa NEC ambao watakuwa ni full time job ni wa kutoka wilayani tu. So, mawaziri na wabunge bado wana opportunity ya kuingia kwenye NEC na CC kupitia matundu yafuatayo:

(a) ngazi ya taifa
wajumbe 10 kutoka tanzania bara

wajumbe 10 kutoka tanzania visiwani
(b) wajumbe 10 wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM taifa
(c) wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao.
(d). Wajumbe wanaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi
i. Wanaochaguliwa na bunge 10 (bara 8, zanzibar 2)
ii. Wanaochaguliwa na blw 5 (zanzibar 5)
(e). Wajumbe wanaochaguliwa kutoka wilayani (221) wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa waliochaguliwa kupitia wilaya watakuwa ni viongozi wa kazi za muda wote ili kuweka wazi zaidi wajibu wa wajumbe hao wa kuwa karibu na wanachama na kushughulikia shida zao.
(f). Wajumbe toka kwenye jumuiya za chama
i. Wanaochaguliwa na uwt 15 (bara 9, zanzibar 6)
ii. Wanaochaguliwa na uvccm 10 (bara 6, zanzibar 4)
iii.wanaotokana na wazazi 5 (bara 3, zanzibar 2)

Kwa hiyo mawaziri na wabunge bado wanaweza kupitia kwenye tundu la NEC (Taifa), wawakilishi wa wabunge wa CCM au kupitia kwenye Jumuiya za Chama na haswa UWT.

Tatizo la mabadiliko haya ya Katiba, hayalengi kuipatia CCM viongozi waadilifu wala kupunguza mlundikano wa vyeo kwa mtu mmoja. Mfano mdogo tu, je, baada ya haya mabadiliko, Januari Makamba, Mwigulu Nchemba na Chilligati watabaki kuwa wajumbe wa Secretariat ya NEC ambao wanahudhuria vikao vyote na bado ni wabunge? Mwenyekiti wa UWT Taifa ni waziri, mjumbe wa NEC na CC. Anna Makinda ni Mbunge, Spika, Mjumbe wa CC na NEC, Eng. Stella Manyanya ni Mkuu wa Mkoa, Mbunge na Mjumbe wa NEC kupitia UWT.

Katiba za UWT, Wazazi, na UVCCM hazijabadilishwa katika kuweka sifa za wagombea wa ujumbe wa NEC kupitia Jumuiya hizo. Wala wagombea wa NEC Taifa haijasemwa kwamba wasiwe mawaziri. Contradiction iko kwenye kundi la wawakilishi wa wabunge, what if mwakilishi wa wabunge ni Waziri?

Kwa mtazamo wangu, mabadiliko haya hayajafanyiwa kazi kwa kina na kwa umakini. Wangeweka wazi kwamba nafasi za NEC Taifa wabunge wote hawaruhusiwi kugombea. Pia futa kundi la wawakilishi wa wabunge kwenye NEC.

Haya ni matunda ya kushindikana kwa operation vua gamba kwa kuwa tayari Chama kilishatekwa na matajiri na hawajui namna ya kukirudisha kwa walalahoi. Kila njia wanayopendekeza inaonekana kama vile haifanyi kazi. Walianza na kuvua magamba, imeshindwa. Wamekuja na mabadiliko ya Katika, nayo itashindwa bado kuna watu wataendelea kuwa na influence kwenye vikao vya NEC na CC. Mwisho wanataka kuunda Kamati ya Maadili na Nidhamu [ingawa ilikuwepo ambayo ilikuwa inaongozwa na JK]. Sasa kwa sababu JK hataki kuonekana yeye ni mbaya, anataka kusukumia watu wengine wafanye kazi ya kudhibiti mafisadi. Sasa kama NEC na CC wameshindwa kuwadhibiti, hiyo Kamati mpya ya maadili itawezaje kuwashughulikia wale wote ambao wanaonekana kwamba ni magamba?
 
Tatizo la CCM sio mgawanyo wa madaraka! ni kukosa mwelekeo wa siasa kwa kuacha misingi ya chama na kukigeuza kama ngazi ya wajanja. Watu walipogundua kuwa serikali haina nguvu zaidi ya chama kila mmoja akajikita huko kutengeneza njia au kulinda masilahi.

Matokeo yake chama kinaongozwa na watu wasiojua maadili, taratibu, kanuni na siasa. Ushahidi ni pale chama kama CCM kinaposhindwa kuwachukulia hatua watu wawili au watatu kwasababu tu watu hao wamekinunua chama na si sera au itikadi.

Kurudisha chaguzi katika ngazi za chini hakutasaidia kwasababu hata sasa tunshuhudia wagombea wa uongozi katika kata wakifanya yale yale ya wabunge. Kila mtu amejua kuwa chama si itikadi wala maadili bali chumo na ajira inayolipa kweli kweli.
Inapofikia PhD holder anagombea udiwani ujue hapo lipo jambo. Hivi kuna nani katika ngazi ya wilaya anayeweza kumgusa papa aliyeshindikana kwa NEC na CC kama si kujidanganya.

Mgogoro wa wabunge una sura mbili.
Sura ya kwanza ni masilahi, kwamba mbunge anaweza kuwa mjumbe wa kamati lukuki akijikusanya masilahi.

Sura ya pili ambayo ni muhimu sana ni uongozi. Wabunge wanaelewa wazi kuwa kutokuwepo kwao ndani ya uongozi kunaweza kuwaathiri sana katika teuzi. Chukulia mfano wa Nzega ambako sasa tuna ushahidi kutoka ndani ya chama mgombea alienguliwa ili fulani apewe fursa! Spika aliondolewa katika kinyang'anyiro kwasababu 'wabaya' wake walijipanga ndani ya CC.
Ikatolewa sababu ndogo tu,hii ni zamu ya akina mama.

Nimekupa mifano hiyo miwili ili uone ni jinsi gani wabunge wanahisi kukalia kuti kavu nje ya chama. Ingawa nguvu ya pesa inaweza kutumika lakini si kila mbunge wa CCM mwenye ubavu huo. Ukizingatia kuwa wafanya biashara wanamshiko wabunge wanaona hali ni mbaya kwa upande wao.

Sio kwamba wanataka nafasi walitumikie taifa, la hasha! wanataka nafasi za kutetea masilahi yao. Sasa kama huyu ndiye mtu unayemtegemea atengeneze sera za chama utakuwa umejidanganya, na ni kuanzia hapo ndipo kunakuja kitu 'masilahi kwanza itikadi ya chama baadaye' Sasa hapo chama hakijapoteza dira na mwelekeo.

CCM tafuteni dawa ya kutibu gonjwa kuanzia ngazi za juu tatizo lilipo na si kutafuta aspirin
 
Kunaweza kuwa na sababu nyingine za chama kuvunjika vipande vipande lakini sio hili la mabadiliko ya katiba juu ya wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama, hasa NEC kwani hili litakipa chama uhai zaidi hata kama utakuwa ni wa muda mfupi. Tofauti na zamani, wajumbe wa NEC wengi watatokea wilayani. Hii ni mbinu ya kukisogeza chama karibu na wananchi zaidi tofauti na zamani ambapo kila mkoa ulikuwa unatoa mjumbe mmoja tu wa NEC. Pia kulikuwa na tatizo la viongozi kujirundikia vyeo, mfano wabunge kuwa pia wajumbe wa NEC. Hili sasa litakwisha kwani chini ya mapendekezo mapya, wabunge watapigwa technical knock-out huko huko majimboni kwao. Hii itatoa nafasi kwa wanachama wa CCM huko ngazi za chini kuhisi kwamba sasa na wao wana sauti katika ngazi za juu za maamuzi za chama.

Wataoathirika na mpango huu mpya ni wale viongozi wenye tabia ya kununua kura - wenye uwezo wa kifedha wa kuwanunua wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa kuwanunulia konyagi na biskuti na kuwapa vibahasha wakati wa safari zao kutokea kanda ya ziwa na treni ya kati kuelekea dodoma. Pia zamani wenye pesa walikuwa wanawakodishia mabasi maalum wajumbe kutoka mikoa mbali mbali kwenda dodoma kupiga kura kwa maelekezo maalum. Tofauti na zamani, chini ya utaratibu mpya, sasa wajumbe hawa wanaenda Dodoma kuchagua majina 20 tu (kumi bara, kumi visiwani), sio 80 kama zamani, ambapo mtu mwenye hela unaandaa boksi lako lililojaa mamilioni na kuanza kupita kila gesti wanamolala wajumbe hawa na kuwagawia pesa. Kwa system hii mpya, wajumbe hawa wanachagua watu 20 tu kati ya jumla ya kama 80; wengine 60 watatokana na mikutano mikuu ya wilaya. Sasa changamoto kwa viongozi wanaonunua wapiga kura ni kwamba sasa inabidi waanze mchakato wa kwenda kwenye kila wilaya (zipo kariba wilaya 130 Tanzania) na kuhonga wajumbe. Hii itakuwa ngumu kwa sababu kadhaa kwanza ikiwa kwamba viongozi wa aina hii wataonekana kirahisi na TAKUKURU kwa mfano haita ingia akilini kiongozi wa ngazi za juu au wapambe wao, kuonekana kwa mfano wilaya ya Newala au manyoni nyakati za uchaguzi wa wajumbe wa NEC. wanatafuta nini? Lakini pia itakuwa vigumu kwa viongozi wa aina hii kujigawa nchi nzima ikiwa kura huko wilayani zinapigwa siku moja. Ilikuwa rahisi kwa dodoma kwani mchezo mzima ulikuwa unamalizikia pale pale.

Kwa kifupi, mpango huu utaathiri sana mikakati ya wanaowania Urais kupitia tiketi ya CCM 2015.

Mchambuzi kwa nini tusifanye na primaries tu za wagombea Urais wetu? huoni kama hii itaimarisha zaidi chama na kukipa taswira mpya, ari mpya haswa pale wanachama wanapothaminiwa tena na dhamana kama hizi..nafikiri hii inawezekana kwa sababu watu wameamka sasa hivi na wana ccm wengi wanao uwezo wa kuendesha hizi primaries vizuri tu bila ya matatizo yeyote. Hizi board room style meeting za kuchaguz mgombea urais zimepitwa na wakati na inabidi ccm kama chama kikongwe kiwaachie hawa wapinzani waendeleee na huo utaratibu CCM iwe primaries tu kila ngazi.
 
CCM please change, watanzania wanalilia chama cha jembe na nyundo!!
Najua ni ngumu kuwatosa mamilionea wanaowazunguka, wanaotaka muwe puppets wao, hebu jitoeni acheni visingizio,
chonde chonde, mtafikishwa mahali mtauza watu mali zikiisha, chonde chonde punguzeni tamaa
Mkuu hawawezi kubadilika: maandiko lazima yatimie "mene mene tekeli na peresi CCM" dalili za utawala uliofitinika baadhi hizi hapa:
- Watawala hawaelewani tena na watawaliwa,
- Watawala wana pambana/kudhulumiana wenyewe kwa wenyewe= Mkyembe, mndosya na wengine walitoweka ghafla kwa ajali za kupangwa,
Dhuluma imekithiri,
Ufisadi umekithiri
Watu wadogo/maskini=kope za macho za mungu zinalalamika.
Manabii waliotumwa na mungu wanauwa.
Tafakari tena maneno ya Laana: "MENEMENE TEKELI NA PERESI CCM" UTAWALA WAKO CCM UMEFINITIKA.
Walio ndani kimbieni hasira ya Mungu haraka!!! ONYO
 
Unajua hawa jamaa wanajifanya hawaioni hiyo kauli ya baba wa taifa iliyopo nyuma yao.
 
Mchambuzi,
Don't you feel haya mabadiliko yamekuja too little too late? Siamini kuwa chama hiki kinaweza kujinasua kutoka shimo kilimojichimbia. Nakumbuka kuanzia 1995 Mwalimu Nyerere alizungumzia ukosefu wa dira ndani ya CCM, na tatizo la rushwa. Lakini hakuna aliyemsikiliza. Ikatokea kwamba the more corrupt you are the more accepted within CCM. Hawa wameoza. Sidhani kuwa wanaweza kujinasua.

Wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa wa CCM uliopita ambapo mfanyabiashara tajiri mwenye elimu ya darasa la saba Jah People alimshinda Katibu Mkuu wa zamani wa CCM Phillip Mangula, matokeo yale yalimshangaza kila mtu mwenye akili timamu kwani Jah People bila kuhonga fedha nyingi na takukuru kufumba macho hakuwa na kigezo chochote cha kumshinda katibu mkuu mstaafu. Katika hotuba yake ya kushukuru wananchama, Mangula aliwatahadhalisha wanaccm kuwa chama kilikuwa na muelekeo mbaya ambapo uongozi wake ulikuwaunanunuliwa kana kwamba waombaji wako mnadani ambapo anayetoa fedha nyingi ndio anayenunua bidhaa!! Aliwatahadhalisha kuwa mwenendo huo usipothibitiwa ulikuwa hatari kwa mustakabali wa chama na nchi nzima. Inaelekea utabili wake umedhihilika!
 
Mambo magumu wakati CCm inakamata viti vya ubunge. Igunga,Uzini, na bado arumeru sasa.
 
Mkuu,
Hii ni makala ya lini? Mapuri alikuwa katibu mwenezi miaka ya nyuma sana, wakati wa Mkapa, baadae akapelekwa China kuwa Balozi. be what it may, nakubaliana na wewe kuhusu CCM kukosa dira na kuendesha siasa za kujichanganya. Huyu mwandisha anaongelea azimio la arusha kwa maana ipi wakati azimio linalotawala sasa ni lile la zanzibar? Na kuhusu masuala ya kugawa utajiri kwa wananchi, kuinua kilimo, mambo haya wakiyatamka majukwaani kwa kweli watajitafutia kupigwa mawe, kweli kabisa kwasababu katika mazingira ya leo ya CCM na jinsi inavyoendesha uchumi wa nchi hii na kupelekea watanzania wengi kuwa watumwa na mafukara katika nchi yao iliyojaa kila aina ya rasilimali, maneno mengi uliyoya highlight rangi nyekundu ni maneno yanayotia hasira na uchungu sana, kwani ni kama kusanifu tu maskini wa nchi hii. Nimeshtuka sana kuona huyo Mapuri akijitahidi kutetea kitu ambacho hakipo. Sijui viongozi wa CCM huwa wanaingiwa na wazimu gani. Hata Nape miezi kadhaa iliyopita alijibu maneno kama hayo hayo kwenye mdahalo alipoulizwa CCM inafuata itikadi gani. Binafsi nilishtuka na sikuelewa kabisa mtu mwenye upeo kama wake anasukumwa na nini kutetea itikadi ya ujamaa wa Marx-Lenin, nyakati hizi.
Mkuu wangu kama ujuavyo Msingi wa chama hauwezi kubomelewa pasipo kwanza kuibomoa nyumba nzima, na maadam CCM wanaendelea kujenga ghorofa juu ya msingi wa Ujamaa na Kujitegemea, tafsiri yake haiwezi kubadilika na ndicho alichokifanya Mapuri. Kwa madai yake ni kwamba Dira hii ya chama haijabadilika baada ya Azimio la Zanzibar na hii pia ndio DIRA ya TAIFA, vyama vya Upinzani pia wanakubaliana - kitu kama hicho....mmnnnnnh!
Unaweza kumsoma vizuri ktk site ya chama na bandiko hilo lipo hadi leo:- Bofya

Lowassa kama mtu haogopwi hatishi na haogopwi hata n nzi tu.
Fedha yake Lowassa ndiyo inayoogopwa na hata kusujudiwa.
Ile kashfa ya Richmond Wizi wa Bank Kuu na Madudu engine ndani ya serikali yana mkono wa Lowassa.

Lowassa ndiye aliye kuwa akikusanya malipo yote ya Richmond na Baadaye Dowans.
Lowassa ndiye kiongozi wa kwanzawa ngazi ya juu ndani ya serikali ya CCM kuibamamilioni ya fedha huu akilindwa na Polisi, Jeshi, Usalama wa Taifa,Ikulu na Takukuru.

Lowassaa anataka U rais wa Tanzania hata gharama yake ikiwa ni kuibinafsisha serikali.

Fedha aliyoikomba kutoka hazina ya Taifa sasa anapita nayo kwenye kila Usharika na Kigango na kuwanunua waumini kwa kile akiitacho mchango wa harambee ya kanisa huku yeye binafsi akitoa mamilioni ya fedha za wizi kuwanasa. Wachngaji kupewa mamilioni ya wizi kujikimu.

Makanisa siku zote ni kama shimo la maji taka.

Yanapinga wizi lakini yanpokea fedha kutoka kwa wezi kama Lowassa.
Makanisa;
Yanapinga wauaji na majambazi lakini jambazi akitoa mchango mnene unapokelewa unapigwa busu na kubarikiwa kwa nguvu zote.

Yanapinga ulevi umalaya na uasherati lakini yanapokea fedha kutoka kwenye madangulo na club za pombe. Yanahubiri Amani Haki na Upendo lakini siku zote yanafungamanana madikteta waujaji na wavunjaji wa haki za binadamu,wene mdangulo na biashara za malaya.wchungaji ni malaya namba moja na wazinzi wakubwa. hutembea na wake za watu wachumba wa watu wazi wazi.

Yanapinga ushoga lakini wachungaji wengi ni mashoga(Mabasha) wanatembea na watu wa jinsia yao, wanatembea na vijana wadogo, wanabaka vijana wadogo kinyume na maumbile yao.

Ndiyo maana baada ya mapinduzi ya nchi nyingi Maaskafu mashemazi na wachungaaji wengi hujikuta wakiingia mitimi kuponya nafsi zao kwa sababu ya kushiriki kwao katika uovu.

Lowassa amaechagua kanisa katika kueneza sumu yake ili ingie Ikulu.

Ole wako Edward Lowassa siku inakuja ambayo utatamani kwamba hukuzaliwa kabisa.
Magugu unayo yapanda utayavuna na kuyaweka gharani hata punje ya mwisho.

"Lowassa bado ana nguvu sana ndani ya PCCB na Jeshi la Polisi, na ndio maana issues zote zinazomgusa Lowassa au vijana wake wa UVCCM, polisi na PCCB huwa wako makini sana katika kuzi-handle. Bado CCM yenyewe inamgwaya Lowassa, na sijui ni kwanini inamgwaya na hilo ndio linampa nguvu zaidi.
"

Mkuu sikubaliani na ujumla wa hoja zako kuhusiana na makanisa.

Unaposema makanisa unamaanisha kanisa gani? Au ndio ile methali samaki akioza wote wameoza?

Methali kama hiyo zimepitwa wakati na hazitoi tija kwa muhula tuliopo.

Kama kuna makanisa yanayokubali pesa za wazinzi, majambazi, wala rushwa , haimainishi ni makanisa yote.

Je kuna kipimo gani cha kujua hii ni hela ya mzinzi, jambazi au mla rushwa?

Fikiria kidogo, katika ngazi ya familia au jambo binafsi kama michango ya harusi, elimu au chochote katika familia yako, kuna hela yoyote mmeshawahi kuikataa kwa vile inatoka kwa mwizi, jambazi au mla rushwa? Sidhani itawezekana bila upinzani na kuleta vurugu katika vikao hivyo, hivyo basi la kujua kama pesa ni za fisadi, jambazi, kahaba, hilo aachiwe mwenyewe mtoaji. Unless kama utaweza kuhakikisha kwamba, hela inayotoka hapa ndio ile iliyoibwa sehemu fulani. Mambo haya si rahisi sana kuyatenganisha.

Hivyo basi, kuyahukumu makanisa kwa kupokea michango ya wadhambi si sahihi hata kidogo..... Mpaka pale utakapothibitisha hoja yako.
 
Back
Top Bottom