CCM Mambo yazidi kuwa Magumu: Ni kuhusu rasimu ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Mambo yazidi kuwa Magumu: Ni kuhusu rasimu ya katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Feb 12, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Chama kinataka kugawanyika vipande vipande. haya tusubiri yetu macho na masikio!
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  sio kugawanyika hata kingefutika kabisa ingekuwa bora zaidi, chama kimeja mafisadi wanateteana hakuna uwajibikaji, hakitekelezi ahadi zake wakati wa uchaguzi kuna uhalali gani kinaonekana sasa kama sio chaama cha siasa bali genge la wafanyabishara ambao wanashindanisha sera zao za ufisadi!! kupambana na ufisadi sio sera zao ndio maana wameshindwa kuvuana *******..
   
 3. a

  alisam Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hasira za posho zimehamishiwa kwenye katiba.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kumputa mtu mkono unaolekea kinywani sii kazi ndogo vile..walivikwa kofia tatu wengine nne leo mje zichukua kirahisi hivyo... Wabunge wanasema tu lakini wanajua fika kwamba ukiwa huna cheo ndani ya chama CCM basi ubunge wako hauna manufaa, mbunge anaweza kukamatwa akaswekwa ndani lakini sii rahisi kumkamata kiongozi wa chama na hasa CCM huko mikoani. Mwenyekiti wa CCM ana nguvu utafikiri yeye ndiye governor..
   
 5. H

  Haika JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  CCM please change, watanzania wanalilia chama cha jembe na nyundo!!
  Najua ni ngumu kuwatosa mamilionea wanaowazunguka, wanaotaka muwe puppets wao, hebu jitoeni acheni visingizio,
  chonde chonde, mtafikishwa mahali mtauza watu mali zikiisha, chonde chonde punguzeni tamaa
   
 6. t

  tenende JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ..Eeeh Mwenyezi Mungu! Naomba maneno haya yatimie. Kifo cha CCM ni UKOMBOZI kwa taifa!.
  :lol::lol:
   
 7. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CCM isigawanyike, ifutike kama KANU
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijaelewa ugumu wake unakujaje? Tuwe fair hebu fafanua kidogo Mungi.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona Dr. John Pombe Magufuli si mjumbe wa NEC na anaendelea vyema tu?
   
 10. j

  jigoku JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mungi unataarifa rasmi za kikao?kama huna basi tufafanulie,ndio tunaombea sana hata kesho kiamke kimefutika kabisa kwani ikiwa hivyo ndio itakauwa ukombozi wa taifa hili,ila kwa post yako mkuu bado mimi sjapata picha.
   
 11. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Kunaweza kuwa na sababu nyingine za chama kuvunjika vipande vipande lakini sio hili la mabadiliko ya katiba juu ya wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama, hasa NEC kwani hili litakipa chama uhai zaidi hata kama utakuwa ni wa muda mfupi. Tofauti na zamani, wajumbe wa NEC wengi watatokea wilayani. Hii ni mbinu ya kukisogeza chama karibu na wananchi zaidi tofauti na zamani ambapo kila mkoa ulikuwa unatoa mjumbe mmoja tu wa NEC. Pia kulikuwa na tatizo la viongozi kujirundikia vyeo, mfano wabunge kuwa pia wajumbe wa NEC. Hili sasa litakwisha kwani chini ya mapendekezo mapya, wabunge watapigwa technical knock-out huko huko majimboni kwao. Hii itatoa nafasi kwa wanachama wa CCM huko ngazi za chini kuhisi kwamba sasa na wao wana sauti katika ngazi za juu za maamuzi za chama.

  Wataoathirika na mpango huu mpya ni wale viongozi wenye tabia ya kununua kura - wenye uwezo wa kifedha wa kuwanunua wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa kuwanunulia konyagi na biskuti na kuwapa vibahasha wakati wa safari zao kutokea kanda ya ziwa na treni ya kati kuelekea dodoma. Pia zamani wenye pesa walikuwa wanawakodishia mabasi maalum wajumbe kutoka mikoa mbali mbali kwenda dodoma kupiga kura kwa maelekezo maalum. Tofauti na zamani, chini ya utaratibu mpya, sasa wajumbe hawa wanaenda Dodoma kuchagua majina 20 tu (kumi bara, kumi visiwani), sio 80 kama zamani, ambapo mtu mwenye hela unaandaa boksi lako lililojaa mamilioni na kuanza kupita kila gesti wanamolala wajumbe hawa na kuwagawia pesa. Kwa system hii mpya, wajumbe hawa wanachagua watu 20 tu kati ya jumla ya kama 80; wengine 60 watatokana na mikutano mikuu ya wilaya. Sasa changamoto kwa viongozi wanaonunua wapiga kura ni kwamba sasa inabidi waanze mchakato wa kwenda kwenye kila wilaya (zipo kariba wilaya 130 Tanzania) na kuhonga wajumbe. Hii itakuwa ngumu kwa sababu kadhaa kwanza ikiwa kwamba viongozi wa aina hii wataonekana kirahisi na TAKUKURU kwa mfano haita ingia akilini kiongozi wa ngazi za juu au wapambe wao, kuonekana kwa mfano wilaya ya Newala au manyoni nyakati za uchaguzi wa wajumbe wa NEC. wanatafuta nini? Lakini pia itakuwa vigumu kwa viongozi wa aina hii kujigawa nchi nzima ikiwa kura huko wilayani zinapigwa siku moja. Ilikuwa rahisi kwa dodoma kwani mchezo mzima ulikuwa unamalizikia pale pale.

  Kwa kifupi, mpango huu utaathiri sana mikakati ya wanaowania Urais kupitia tiketi ya CCM 2015.
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mchambuzi,
  Don't you feel haya mabadiliko yamekuja too little too late? Siamini kuwa chama hiki kinaweza kujinasua kutoka shimo kilimojichimbia. Nakumbuka kuanzia 1995 Mwalimu Nyerere alizungumzia ukosefu wa dira ndani ya CCM, na tatizo la rushwa. Lakini hakuna aliyemsikiliza. Ikatokea kwamba the more corrupt you are the more accepted within CCM. Hawa wameoza. Sidhani kuwa wanaweza kujinasua.
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  duh lini kinakufa tuwe huru km libya
   
 14. K

  Keil JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Mchambuzi,

  Naweza kukubaliana na hoja zako, lakini mabadiliko haya ya Katiba sioni kama kinaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa mafisadi ambao wanataka kuingia Ikulu kwa njia yoyote ile.

  Chaguzi za ndani za CCM kwa ngazi za Wilaya na Mikoa, zimekuwa zikiendeshwa kwa mfumo huu huu, na bado mafisadi hao hao walifanikiwa kupanga safu ya uongozi kuanzia ngazi ya Wilaya mpaka Mkoa. Sasa ni kipi kitawashinda leo hii kupata mjumbe wa NEC kwenye ngazi ya wilaya?

  Iwapo kwenye Kura za Maoni watu wanahongwa shilingi elfu 5 au 10, na kutoa kura kwa mgombea, leo hii ndio watashindwa kuwahonga wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ambao wanamchagua mjumbe mmoja wa NEC?

  Mfumo wa Uhongaji ndani ya CCM hauhitaji uwepo wa mhusika mkuu, bali ni swala la mhusika mkuu kutafuta mtu wake na kuhakikisha kwamba anasimamia kila kitu ili kuhakikisha kwamba mgombea wao anashinda.

  Hoja ya TAKUKURU naomba wala usiingize. Jiulize, ni wangapi ambao walishikwa wakihonga kwenye kura za maoni za 2010 kwa upande wa CCM? Je, kesi ngapi zilipelekwa mahakamani? Wapo walioshikwa na ushahidi wa wazi kabisa, lakini waliachwa wakapeta. Kesi pekee ninayoikumbuka ilikuwa ni ya Mwakalebela ambaye alipambana na Mwanamtandao Mama Monica Mbega. Mimi binafsi sina imani na Polisi wala TAKUKURU kwa kuwa wanafanya kazi kwa kuangalia nani anahusika na yuko kundi gani. Unakumbuka kesi ya yule mama wa Moshi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya mkoani Kigoma? Kamanda wa PCCB alijikuta akihamishwa ghafla mara sakata hilo liliporipotiwa, kwanini?

  Lowassa bado ana nguvu sana ndani ya PCCB na Jeshi la Polisi, na ndio maana issues zote zinazomgusa Lowassa au vijana wake wa UVCCM, polisi na PCCB huwa wako makini sana katika kuzi-handle. Bado CCM yenyewe inamgwaya Lowassa, na sijui ni kwanini inamgwaya na hilo ndio linampa nguvu zaidi.

  Uchaguzi wa ndani wa CCM wa mwaka 2007, kuna watu walikuwa wanatumia jina Kikwete kama kete ya kuchaguliwa, kwamba mimi ndio chaguo la Kikwete so, nipeni kura na walishinda. Kwa jinsi mambo yalivyo ndani ya CCM sasa hivi, usije ukashangaa watu wanaanza kutumia jina la Lowassa ili washinde uchaguzi wa ndani na hao hao ndio ambao watakuja kuiangamiza CCM.

  Kuonyesha ni jinsi gani CCM inamgwaya Lowassa, wale vijana waliokusanyika Dodoma kwenye kikao cha CC na NEC mara baada ya uchaguzi wa Igunga, walichukuliwa hatua gani? Kikwete alikuwa na details zote za mkusanyiko wa vijana kutoka mikoa yote ya Tanzania na kwamba walilipiwa nauli kuja Dodoma, na malazi na gharama nyinginezo za kuwepo kwao Dodoma. Je, Kikwete na CC waliwafanya nini? Wassira na Lukuvi waliishia kumsema Malisa bila kuchukua hatua yoyote.

  Hali hiyo kwa jinsi inavyoendelea kuachwa ndiyo inawapa kiburi Lowassa na kundi lake. So, wale wote ambao hawakuwa kambi ya Lowassa, wataona kwamba huyu ndo mbabe so ukikaa kwenye kundi lake hakuna mtu atakugusa, iwe ni Kamati ya Maadili ya CCM, Jeshi la Polisi, au PCCB. Wale vijana wa Arusha walipofungua matawi na kufanya mikutano yao bila kibali cha Jeshi la Polisi, walifanywa nini?

  Hii ngoma bado ni nzito, tatizo ni kwamba uongozi wa chama hautaki kwenda kwenye kiini cha tatizo ili kuweza kulitatua, wanaendelea kuzunguka tu na mwisho wake ni kwamba kansa inaendelea kusambaa.
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mchambuzi unajua wewe ni kati ya wana CCM wachache unayekemea na kupinga vitendo vya rushwa lakini wana CCM wengi kuanzia ngazi ya chini mpaka juu,rushwa ni sehemu ya maisha yao.
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Aliyezungumzia ukosefu wa dira si nyerere bana ni Kolimba wewe kila kitu nyerere aisee..

  Kweli mabadiliko haya yalitakiwa yaanze enzi za kolimba wameahirisha hadi leo, lakini ni vizuri kwa nchi yetu wacha vyama vya upinzani navyo vikue..ccm ikiwa very powefull ni hatari kwa Taifa..
   
 17. k

  kanjanja Member

  #17
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm haina jipya wala dira
   
 18. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Haya tunashukuru mchambuzi ......
  ila... Sidhani kama kutakuwa na cha kuwashinda Kingmakers..
   
 19. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  CCM ifanye lolote inalotaka ila isiifilisi nchi tu kwa kugawa watu kisiasa na kugawa rasilimali zetu. After all ni chama kama chama kingine. wakicheza vibaya karata zao, hiyo itakuwa pole yao.
   
 20. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Jasusi,
  Kimsingi nakubaliana na wewe. Mbali ya ukosefu wa dira na kukithiri kwa rushwa/ufisadi, CCM pia inakabiliwa na tatizo la wanachama kujihisi kwamba uongozi wa Juu wa chama haupo karibu nao huko ngazi za chini. Mabadiliko haya yatakisaidia sana chama katika hilo kwani kila jimbo sasa litakuwa na Mjumbe wa NEC full time akikusanya maoni ya wanachama na kuyapeleka katika vikao vya juu vya maamuzi - Taifa. Whether mawazo yao yatakuwa yanafanyiwa kazi au lah, ni kitu kingine, lakini kwa kiasi fulani sasa wanachama wengi ngazi za chini watajihisi wanasikilizwa na chama. Lakini upo sahihi kuhusu two much bigger projects kabla ya 2015- ukosefu wa dira na kukithiri kwa rushwa/ufisadi.Sijui CCM itaweza kujinasua katika haya ndani ya kipindi hiki kifupi kilichobakia kabla ya 2015.
   
Loading...