Ccm maji shingo

Lusambara

Member
Oct 31, 2010
38
9
Kitendo cha CCM, chama ambacho ni kikongwe na ambacho miaka yote kimetawala nchi kutumia HELKOPITA 2 kwa ajili ya kampeni kinadhilirisha kuwa hali si shwari hata kidogo. Wananchi wa Igunga wengi wamechoshwa na hadi hewa za kila wakati hivyo hawana hamu tena ya kuona CCM inaendelea, ambao wako mstari wa mbele kwenye kampeni za CCM ni akinamama na watoto wa shule.

Kwa hali hii, sijui mpaka jumapili mambo yatakuwaje??
 
Walikuwa wanafidi hela binafsi za Rost.... ila kwa sasa hakuna watakachofaidi kwa huyu wa CCM. Kama wana Igunga wana akili na macho na masikio wavifungue.
 
CCM wameona Igunga ni jimbo gumu kulipata ndio maana Wabunge wote na viongozi wakuu wanahaha Igunga! Helikopta mbili inaonyesha hofu kuu waliyo nayo, kwani kama kweli wao ni chama kubwa wasingehangaika hivyo kupoteza fedha nyingi na kuendesha siasa za maji taka!
 
Lazima wachukue jimbo kwa kupitia mbinu yao ya wizi, na kampeni za shuka kwa shuka....!
 
Mhhh! Namimi suala la matumiz ya helkopta 2 yamenistua.vyama kutumia helikopta ni dharau kwa wapiga kura kuwa ni wajinga watakusanyika kushangaa.
 
Siku zote maigizo ni maigizo tu, wanadhani Helkopta 2 ni kuwazidi CHADEMA kumbe sio CHADEMA wanatumia Helkopta kwa kukosa Magari ya kutosha na rasilimali watendaji chache, nimeshaangaa CUF nao wanaleta Helcopta! Sipati Picha baada wa uchaguzi kuna viongozi wa CUF watawekwa rehani kufidia madeni ya Helkopta, kweli iga ufe!
 
ccm inalazimisha wananchi wa igunga tuamini hivyo ile hali maisha bado ni magumu tumeamua kubadili msimamo wacha tujaribu kwanza hawa cdm wao wanaonekana kupigania maslahi ya wananchi kwa vitendo na sio porojo za kujivua gamba unajivua gamba ile hali waliokula pesa ya serilkali wanakuja kutudanganya huku igunga acheni masihala bwana hampati kitu hapa hapa ni Kashindye tu.
 
Safi sana. Chukueni maneno ya Zito kama changamoto kwenu ambapo alisema wabunge wa CDM walikuwa wachache lakini walijitahidi kuwatetea wananchi. Sasa muwaongezee Kashindye wapate nguvu zaidi.
 
mwanzoni walikua wanatumia ungo sasa yule aliekuwa rubani wao ameshatangulia mbele ya haki....
 
CCM CCM CCM...

Chama hiki ni jinamizi la taifa hili... Ni mumiani lanywa damu za wa-TZ!! Ni vile tu wamefanikiwa kutuacha na ujinga wetu ili watutawale vizuri. Natumaini wana-Igunga wametoka tongotongo za usingizi huu!!! Watafanya maamuzi sahihi...
 
Inanikera sana kila nina posikia neno CCM,tena inaudhi mpaka basi.mijitu isyokuwa na aibu,huruma mijitu haina ut,minafiki,mijitu miongo iko CCM inasikitisha sana wamejazana Igunga kuwalaghai wananchi huku wakijua hakuna wanachowafanyia wananchi licha ya wananchi kuendelea kulipa kodi,licha ya madini mengi yaliyoko Tanzania,tena na mengine yako hapo Igunga,pamoja na resources nyingine nyingi,Jinamizi hili la -Taifa -CCM limetuchosha,tena mm huwa nakerwa sana hata yanapokwenda bungeni yako mengi lakini hakuna yanachokifanya zaidi ya kuitikia ndioooo kwa kila jambo,sasa wana Igunga fumbueni macho msipeleke hii mijitu ya Ndioooo kwa kila jambo bungeni.
Jumapili i karibu
 
Wanatumia rasilimali kibao kwa watu masikini kama wale! baada ya uchaguz watakutana tena wakati wa uchaguzi mwingine, si yule mzee wa kijiji kimojawapo alisema hakuwahi kumuona Rostam tokea wamemchagua!
 
Kitendo cha CCM, chama ambacho ni kikongwe na ambacho miaka yote kimetawala nchi kutumia HELKOPITA 2 kwa ajili ya kampeni kinadhilirisha kuwa hali si shwari hata kidogo. Wananchi wa Igunga wengi wamechoshwa na hadi hewa za kila wakati hivyo hawana hamu tena ya kuona CCM inaendelea, ambao wako mstari wa mbele kwenye kampeni za CCM ni akinamama na watoto wa shule.

Kwa hali hii, sijui mpaka jumapili mambo yatakuwaje??

Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. John Tendwa yuko wapi kuhusiana na hili la GHARAMA ZA UCHAGUZI? Why 2 helicopters? What for? Hivi Igunga ina Eneo la Mraba kilomita ngapi mpaka CCM watumie helikopta 2? Haya kama siyo matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi ni kitu gani? Tumeambiwa bajeti ya Uchaguzi mdogo wa Igunga ni kiasi cha Tshs.80 milioni KWA KILA CHAMA. Lakini inavyoonekana wenzetu wa CCM hii 80m watakuwa wameisha izidisha 10 times na wata gota kwenye Bilioni moja na zaidi. Huo ndo ukweli. Kama Tendwa anabisha basi amwagize CAG akague immediately baada ya Uchaguzi!!

Igunga can be anothert EPA for CCM!!
 
Back
Top Bottom