CCM majaribuni tena! Je safari hii chama kitasilimika tena?

Hizi ni story tu za hapa jf hazina madhara yoyote ni changamsha genge tu na zitaishia humu humu mitandaoni
Sio stories, unakumbuka kutekwa kwa msaidizi wa mh zito? Kunamtu hapa aliwapa 24 hr awe amepatikana LA sivyo aliemteka amtaje,nilifikiri porojo,duuuu akapatikana next day,kwao mombasa
 
Watanzania hawaitaki kabisa CCM, Mungu saidia litoke hili joka.

Poleni watumishi maslahi yenu mmekandamizwa miaka 4.
 
Siasa za visasi na kukomoana ndizo zinazomkosesha credits Magufuli, uraisi unataka hekima, mzee Madiba anaheshimika ulimwenguni kwa kuwa aliweza kuwasamehe waliyomtesa na maisha yakaendelea, lakini Mugabe alileta jeuri yakamkuta yaliyomkuta.
 
 
Himaya ya CCM, kama ilivyowahi kutokea kwa himaya mbalimbali zenye nguvu duniani, kuna siku itaanguka, lakini itaanguka sio kwa hila tu za watu fulani! Kama historia yaweza kuwa funzo kwetu, bila shaka, wenye hila wataangukia pua na mitaji yao ya kisiasa kupotea asilimia 100. Anguko la CCM litakuja katika mazingira yasiyokuwa ya hila za kupangwa na mtu yoyote. Wimbi litakaloiangusha CCM ni wimbi mithiri ya lile wimbi la Arab Spring ambalo lilidondosha himaya kadha za North Africa miaka ya karibuni.

Kama Kinana, Makamba, Membe na washirika wao wangekuwa na washauri wanaowatakia mema wangewashauri watunze mitaji yao ya kisiasa na salio lao la heshima ya viongozi wastaafu. Kufanya vinginevyo, ni kutafuta fedheha kama ilivyokuwa kwa wengine wa aina yao waliotangulia (wakiwemo ENL, Mzee Kingunge (RIP), Mwapachu, Sumaye, n.k.), ambao walifanya political miscalculations mithiri ya hizi!
 
Mdharau Mwiba Guu Huota Tende
ccm mapande matatu tayari
Linalounga mkono wakosoaji
Bendera fuata upepo
Linalounga mkono utawala wa sasa.....
Hili na bendera fuata upepo sio muhimu sana.... Yanayopewa kipaumbele kwa karibu ni hayo mengine mawili kila moja likitafuta uungwaji mkono... Ni vita inayotokota chini kwa chini kimya kimya lakini soon itakuwa live
 
ccm mapande matatu tayari
Linalounga mkono wakosoaji
Bendera fuata upepo
Linalounga mkono utawala wa sasa.....
Hili na bendera fuata upepo sio muhimu sana.... Yanayopewa kipaumbele kwa karibu ni hayo mengine mawili kila moja likitafuta uungwaji mkono... Ni vita inayotokota chini kwa chini kimya kimya lakini soon itakuwa live
Utabiri wako mtani kundi lipi kuibuka kidedea?? Maana nasikia kuna viongozi waandamizi awamu iliyopita inatakiwa wakae vizuizini
 
CCM wanajua kutuchezea akili kama haukupasuka katika wakati ule 2012-15 haiwezi, Nachokiona wananchi ndo wanaodanganywa, CCM ni wamoja mtaona mwaka 2020 kwenye mikutano ya kupitisha wagombea wa Urais
ccm mapande matatu tayari
Linalounga mkono wakosoaji
Bendera fuata upepo
Linalounga mkono utawala wa sasa.....
Hili na bendera fuata upepo sio muhimu sana.... Yanayopewa kipaumbele kwa karibu ni hayo mengine mawili kila moja likitafuta uungwaji mkono... Ni vita inayotokota chini kwa chini kimya kimya lakini soon itakuwa live
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom