CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, May 27, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Source Tanzania Daima

  BAADA ya suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini kupigwa danadana, sasa Waislamu wametaka suala hilo liingizwe kwenye Katiba mpya.

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliweka suala la uanzishwaji wa mahakama hiyo katika ilani yake ya uchaguzi mwaka 2005/2010 na kuahidi kushughulikia.

  Hata hivyo, suala hilo halikushughulikiwa na katika ilani yake ya mwaka 2010 hakikuliweka suala hilo.

  Mwaka jana akizungumza katika Baraza la Iddi mjini Dodoma, Rais Kikwete alinukiwa akisema serikali haitaanzisha mahakama hiyo na badala yake Waislamu wenyewe ndio waianzishe.

  Hoja hiyo ilipingwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na kutoa kauli kuwa watatumia maandamano ya usiku na mchana, kushinikiza kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

  Akizungumza katika mahafali ya nne ya wahitimu wa Kiislamu katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya jumuiya na taasisi za Kiislamu nchini kukaa na kukubaliana jambo hilo liingizwe katika katiba ili liweze kufanikiwa.

  Kutokana na hali hiyo, aliwahamasisha Waislamu nchini kujitokeza kwa wingi katika Tume ya Katiba inayoongozwa na Jaji mstaafu, Joseph Warioba na kutoa maoni yao kuhusu jambo hilo, ili hatimaye liweze kuingizwa katika Katiba mpya.

  “Nchi yetu imo katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba mpya. Katiba ni dira na ngome inayolinda haki na kuweka misingi ya maendeleo kwa wananchi. Tukio hili ni kubwa, ambapo kila jamii hupigania haki zake za msingi kuzingatiwa.

  “Katiba iliyopo ambayo Waislamu hawakushiriki, imechangia kwa kiasi kikubwa kuwaathiri kiimani, kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa maana hiyo mchakato huu ni fursa muhimu kwa Waislamu kuhakikisha haki zao za msingi zinaingizwa ndani ya Katiba mpya,” alisema.

  Alisema katika jambo hilo wanataka katiba isajili mahakama hiyo, mashauri ya ndoa, talaka, watoto, vifo, mirathi, wosia, wakfu na biashara yasikilizwe na kadhi na bila kutafutwa ridhaa ya mtu au warithi pamoja na mahakama hiyo kuwapa msaada wa nguvu za dola.

  Alisema kwa kuwa suala hilo limechukua muda mrefu ni vema sasa utekelezwaji wake uwekwe kwa mujibu wa katiba.

  “Wakati umefika kwa Waislamu kupigania na kwenda kutoa maoni katika tume ya katiba, ili tuweze kupata Mahakama ya Kadhi. Waislamu wamekuwa wakipuuzwa katika masuala mbalimbali kutokana na kutowekwa katika katiba lakini sasa umefika wakati wa kupeleka maoni na si kuendelea kulalamika,” alisema.

  Aidha, Sheikh Ponda alisema jumuiya hiyo ambayo ni jukwaa la Waislamu la kuratibu mchakato wa Katiba nchini, masuala mengine ambayo Waislamu wanayapigania yaonekane kwenye katiba mpya, ni kuingizwa katika katiba mpya siku ya Ijumaa kutambulikuwa kuwa ni siku ya ibada ambayo itawasaidia Waislamu kupata fursa ya kwenda kuabudu kwa uhuru zaidi.

  “Pia tunataka katiba itambue uwepo wa Mwenyezi Mungu, itoe uhuru wa kuabudu, kwani katiba iliyopo haijatoa uhuru huo na ndiyo maana Waislamu wanazuiliwa ibada pamoja na kuvaa hijabu vyuoni, majeshini na asasi za serikali.

  Alisema kuwa pia wanataka katiba itoe usawa katika elimu kwa maana ya katiba kutamka uwakilishi sawa kwa Wakristo na Waislamu katika Baraza la Mitihani la Taifa.

  “Kabla na baada ya uhuru chombo hiki kimeendelea kutawaliwa na Wakristo na kusababisha upendeleo mkubwa katika uteuzi na usahihishaji wa mitihani, kuwe na uteuzi wa maofisa elimu wakuu wa shule,” alisema.

  Aidha, alisema wanataka sheria ya ugaidi ifutwe, kuwapo kwa uwakilishi wa dini bungeni, pamoja na baraza la madiwani na mawaziri kuwa na uwakilishi wa dini.

  “Pia tunataka katiba iruhusu vyama vya siasa vya kidini, Waislamu na Wakristo wapokezane urais, serikali ya Tanganyika irejeshwe, kuwapo kwa muungano wa serikali tatu, urais wa muungano uwe wa awamu pamoja na kuwapo kwa serikali ya majimbo,” alisema.

  Sheikh Ponda kuwa masuala mengine wanayotaka kuwamo katika Katiba mpya ni mgombea binafsi, matokeo ya urais kupingwa mahakamani, rais kutounda tume ya uchaguzi, adhabu ya kifo iwekwe ndani ya katiba, misamaha ya kodi na mikataba ya kanisa na serikali ifutwe na kikosi cha kupambana na rushwa kuundwa upya na kuingizwa kwenye katiba.

  Concern;

  Jamani sijafafanuliwa vzr juu ya haya.

  Sheria ya ugaisi ifutwe kuna nini nyuma yake?
  Haki ya kusoma hivi hawa watu mmekatazwa na nani kusoma? Mponda elimu yako ni darasa la ngapi na kwa nini?
  Utawala wa kupikezana kwa manufaa ya nani?
  Uhuru wa kuabudu nani kawanyima?
  Sheria ya biashara kwa ...... sijaelewa kivp
   
 2. H

  Honey K JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dosama,
  SASA HAPA THREAD YAKO NA STORI MBONA HAVINA UHUSIANO???!!! IKO WAPI SEHEMU YA STORI INAYOONYESHA CCM KURUHUSU MAHAKAMA YA KADHI KWENYE KATIBA??!!!!!!!!UNAPOTUMWA, AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO KABLA YA KUPELEKA ULICHOTUMWA!
   
 3. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hizi ni pumba tupu, kichwa na maelezo totauti, Shekhe Ponda na CCM inakujaje?
   
 4. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Dah! Haya mapendekezo ya huyu shehk ponda kama yana uchochezi fulani hivi? Polis wa intelejensia hebu fanyeni kazi yenu kama mlivyofanya kwa Nassary,
  ha ha ha ha
   
 5. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  vingine vyote tumeshavisikia sana na tumevizoea lakini hili la kuvaa hijabu majeshini kwa kweli limepitiliza...sasa wawe wanavaa kofia ya jeshi juu ya hijabu au wavae hijabu tu?
   
 6. M

  Mtanganyika mweusi Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ilani ya Chama Chako inasemaje?
   
 7. M

  Mtanganyika mweusi Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ndo napangojea
   
 8. E

  Eberhard JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,024
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Baraza la mitihani linawapendelea wakristo kivipi? Linawatungia mitihani myepesi?
   
 9. E

  Eberhard JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,024
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Yaani hapa ni maslai ya dini na ugaidi tu? Wananchi wengine takataka. Mbona hakusema wapagani nao wapewe madaraka? Uislamu unachokochoko? Yaani hawapendi amani kabisa.
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  NAPE,NAPE NAPE.hivi wewe ni kiongozi au mtawala?
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  mzee wa kukopi na kupaste! Eti vua gamba vaa uzalendo
   
 12. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wakiambiwa waende shule hawataki, Sheikh Ponda kama akili huna tumia hata busara. Mnataka kugeuza nchi hii kuwa battlefield ya waislamu na wakristo, na wasio na dini waende wapi?
   
 13. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kenya wameifutilia mbali hiyo kadhi, ktk katiba yao mpya hakuna hiyo kitu!.
   
 14. M

  Mtanganyika mweusi Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona nasikia ipo
   
 15. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tunaposema waislam wanajidhalilisha ndo kama hivi.
   
 16. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Kama mnaipenda shule inakuwaje mkawaozeshe mabinti zenu ndoa za utotoni eti kisa shule haimsaidii badala yake mle wali na pilau?ama hilo mmelazimishwa na wakristo pia?

  mbona ukiachilia mbali ijumaa huko mashuleni na vyuoni mmepewa mda wa kuabudu sawa na ratiba zinaonesha?
   
 17. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hii nji haina dini, wasipende kuiga vitu havina mshiko kwa taifa.

  Wakatoliki nao wana mahakama ya dini so nao tuwaweke kwenye katiba?

  Ndiyo maana rais aliwajibu wakazianzishe wenyewe na ziishie huko huko!
   
 18. e

  evoddy JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tanzainia itaendelea kuwa nchi isiyokuwa na dini lakini watu wake wataendelea na dini zao wanazoabudu,katiba haitamchagulia mtanzania yeyote yule mahali pa kuabudu.

  Nipotayari hata kufa kwa kupigania hili la kutaka kuwepo ndani ya katiba maswala yanayoiongelea dini furani eti waumini wake wawekwe kwenye katiba hili nitalipinga ikibidi hata kufa kwa kuitetea tanzania yangu

  haitakaa itokee idara yoyote ya serikali iongozwe kwa misingi ya dini furani huu ni usaliti

  hawa viongozi wa kiislamu wanamatatizo sana ubaguzi imekuwa jadi yao na hili ni kwa sababu hawakwenda shule .
   
 19. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Eberhard Why did God create fools like you???
   
 20. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Bangoo nani kakudanganya kenya ipo saana tu ! kwani kinachokuuma nini..? wakati wewe haitokuhusu..?
   
Loading...