CCM: Mafisadi waanikwe, warudishe fedha

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
670
ccm nayo haiko nyuma kulaani ufisadi

CCM: Mafisadi waanikwe, warudishe fedha

*Yataka Rais Kikwete asisakamwe na wanasiasa
*Yaonya dhidi ya EPA kutumika kuleta mfarakano

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka fedha zote zilizochotwa na mafisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zirejeshwe sambamba na wahusika hao kubainishwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Taarifa ya CCM iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati, imelaani taarifa zilizotolewa na gazeti moja (si Majira) hivi karibuni, zikimhusisha Rais Jakaya Kikwete na kashfa ya ufisadi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), kwa kilichoelezwa kuwa ameshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, gazeti hilo lilimkariri Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, akisema Rais Kikwete anafanya uhuni kwa kutoamuru watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani.

CCM ilisema kashfa ya EPA imeanza kutumiwa kwa malengo ya kisiasa, ili kudhoofisha kazi nzuri inayofanywa na Rais Kikwete katika kushughulikia ufisadi na mafisadi, ili aonekane hajafanya jambo lolote la maana.

Ilifafanua, kwamba Rais Kikwete ndiye aliyeamuru akaunti ya EPA ikaguliwe na wakaguzi kutoka nje ya nchi, kampuni ya Ernst and Young na kuutangazia umma matokeo ya ukaguzi huo na kuchukua hatua kadhaa za kuifanyia kazi taarifa hiyo, kwa maslahi ya nchi, ikiwamo kuteua timu ya kuchunguza kampuni zilizotajwa kwenye uchunguzi huo.

"Mheshimiwa Rais aliagiza Tume ihakikishe kwanza fedha hizo zinarudi na pili wahusika wanachukuliwa hatua. Tume ilipewa muda wa miezi sita kumaliza hali hiyo. Hatua zote hizi Mheshimiwa Rais alizichukua akitetea maslahi ya nchi yetu na watu wake. Anastahili pongezi si lawama," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

CCM ilidai kuwa shutuma hizo ni hila za kisiasa zilizolenga kutumia kashfa ya EPA kuchafua jina la Rais Kikwete na kuwataka wananchi kukataa njama hizo zinazoendeshwa na baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani.

"Rais ameonesha ujasiri mkubwa katika kushughulikia suala la EPA na atalihitimisha suala hili kwa ujasiri huo huo. Wananchi tumuunge mkono na tumpe nafasi akamilishe kazi hii," ilisisitiza taarifa hiyo.

Imewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kukosoana kwa lugha ya staha na uungwana si dharau na kejeli na kutaka viongozi wote wanaoendesha siasa za aina hiyo, wabezwe na kupuuzwa.

Imewahakikishia wananchi kwamba Timu ya Rais iliyoundwa kushughulikia suala la EPA ikimaliza uchunguzi na kumpatia ripoti, atachukua hatua stahiki dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na kashfa hiyo.

"Wananchi wote wanaombwa wawe na subira na waendelee kushirikiana na Tume ya Rais hadi kazi ikamilike. Lengo la Rais ni kwamba fedha zote zilizochotwa kinyume cha sheria zirejeshwe na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria," ilisema.

Aidha, CCM iliwaonya wanasiasa wanaotaka kuleta mfarakano baina ya wananchi na Rais kwa kutumia kashfa ya EPA, waache mara moja mchezo huo mchafu na kumwomba radhi Rais Kikwete kwani hastahili kupakwa matope kwa jambo analolisimamia kwa ujasiri mkubwa.

source majira
 
ccm nayo haiko nyuma kulaani ufisadi

CCM: Mafisadi waanikwe, warudishe fedha

*Yataka Rais Kikwete asisakamwe na wanasiasa
*Yaonya dhidi ya EPA kutumika kuleta mfarakano

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka fedha zote zilizochotwa na mafisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zirejeshwe sambamba na wahusika hao kubainishwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Taarifa ya CCM iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati, imelaani taarifa zilizotolewa na gazeti moja (si Majira) hivi karibuni, zikimhusisha Rais Jakaya Kikwete na kashfa ya ufisadi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), kwa kilichoelezwa kuwa ameshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, gazeti hilo lilimkariri Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, akisema Rais Kikwete anafanya uhuni kwa kutoamuru watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani.

source majira
Huyu ndie aliyekimbia skuli?
Kheeeee heeeeee heeeee ...Eeeeh!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom