CCM Lumumba kwachafuka, Vigogo wa UVCCM watimuliwa kwa ufisadi

kilaza mjanja

JF-Expert Member
Jun 2, 2016
654
1,143
Huko Lumumba hakukaliki, Wamefukuzana na kusimamisha muda huu, Mapunda, Seki na mafisi mengine yamefukuzwa kabisa kwakuiba milioni 200.


*Dondoo za Yaliyojiri Kikao cha Baraza Kuu* ......

> Seki Kasuga amesimamishwa Ujumbe wa Baraza na Kamati ya Utekelezaji.

> Mchumi wa Taifa ndugu Omar Sleiman nae amesimamishwa.

*Hawa wote wanapisha uchuguzi wa kuuza viwanja vya Igumbilo-Iringa

> Aliyewahi kuwa Kaimu Katibu wa UV Mkoa wa Iringa Ndugu Nyaongo amefukuzwa pamoja na PS wa Mkoa.
> Kamati ya Utekelezaji Mkoa wa Iringa yote imevunjwa.

> Baraza Kuu limekiomba Chama kimchukulie hatua kali na zinazostahiki Sixtus Mapunda kwa kushiriki uuzwaji wa mashamba hayo na kufuja pesa za Jumuiya.

> Baraza Kuu pia limeiomba Chama kupitia Katibu Mkuu kimchukulie hatua za kinidhamu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa ndugu Hassan Mtenga maana ameshiriki katika sakata hili la uuzwaji wa Mashamba.

> Pia aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa ambaye kwa sasa yupo Chama nae wameomba hatua za nidhamu zichukuliwe dhidi yake.

> Jumla ya fedha 200M zimeliwa kwenye uuzwaji wa mashamba ya Igumbilo.
Huku Sixtus Mapunda akichukua zaidi ya Milioni 80 na Seki 40.

> Kwa mara ya kwanza Kikao cha Baraza Kuu zikiwepo posho na malazi vimegharamiwa na JUMUIYA chini ya Comrade Shaka A. Shaka.

> Kikao cha Baraza Kuu kimemalizika na watakutana mwezi wa 10 kwenye Baraza Maalum.


Magu atawaua mwaka huu ccm na mitoto yao UVCCM

=========

UVCCM Taifa imewafukuza kazi aliyekuwa Kaimu Katibu UVCCM Iringa Ally Nyawenga na Sekretari Pendo Kinyunyu, pia Kamati ya Utekelezaji yote Mkoa yavunjwa.

Baraza Kuu la Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa limeibua ufisadi mkubwa ndani ya jumuiya hiyo, hatua iliyosababisha kuwafukuza kazi, kuwasimamisha na kuwashtaki baadhi ya vijana wake kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana ili wachukuliwe hatua za kinidhamu na vikao husika.

Walioshtakiwa ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Mjini, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga na Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Elisha Mwampashi. Waliofukuzwa ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Alli Nyawenga na Katibu Muhtasi wa ofisi ya UVCCM Mkoa wa Iringa, Upendo Kinyunyu.

Waliosimamishwa ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kutokea Mkoa wa Iringa, Seki Kasuga na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha wa UVCCM Taifa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mjini Zanzibar, Omari Selemani.

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Shaka alisema jana kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha baraza kuu kilichoketi juzi na kushirikisha wajumbe 145 kati ya 167 wa baraza hilo.

“Baraza Kuu limepokea taarifa ya uchunguzi wa shamba la UVCCM namba 454 MBYLR lenye ekari 210 lililopo Igumbilo Wilaya ya Iringa Vijijini,” amesema na kuongeza:

“Shamba hilo liliuzwa kwa Suhail Thakore kinyume cha utaratibu, baada ya upimaji wa viwanja, viliuzwa kwa watu mbalimbali na kuwahusisha viongozi wenye dhamana ndani ya jumuiya yetu.”

Amesema kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo iliwashirikisha wajumbe wanne ambao ni Mariamu Chaurembo (Mwenyekiti), Juma Homela (Katibu) Ally Nassor na Amir Mkalipa.
 
CDM pokeeni zigo hilo tayari kazi ishaanza ya kusafisha
Sio mahali pa majizi mliwalea sasa watumbueni hukohuko CDM inapokea watu safi walioonewa na Magamba na wakatubu na kubatizwa upya na kukubali falsafa zake
 
Wao walidhani Magu anawasomesha namba wapinzani pekee?

Sasa keshawageuzia kibao, amewatangazia 'kiama' viongozi wa Chama chake ambao anaona hawaendi naye sambamba....

Hivi sasa naamini wanaccm wengi wataanza kuisupport 'kimoyomoyo' operesheni Ukuta........
 
Wizi wanaanzia mbali sana!Kutoka vijana hadi wazeeke,nchi hii si wataimaliza?
JPM safisha chama kuanzia watoto/chipukizi/vijana uje umalizie wazee wa ccM,wabaki wachache upige nao kazi
 
Sasa Habari Yako Haijitoshelezi
Rudi Tena Kwa Habari Iliyoshiba
Ccm ,Itakwenda Kwisha Majizi Yote Makubwa Ni Ccm
 
Back
Top Bottom