CCM Lumumba-fungu la kikosi cha propaganda mitandaoni lazua minung'uniko.

Unajua bwana hawa jamaa nawaonea huruma sana,

Sometimes wanatumia pesa zao binafsi kuingia cafe au hata kununua bundle airtime without prompt refund.

Sasa ukiongeza na arguments zao zinazopingana na nafsi zao, kisha ukamalizia na madongo wanayoyapata hapa Jf, kweli Lumumba hawajafanya fair hata kidogo, wawape tu chao.
 
Wengi wamepotea Kama Tume ya Katiba , Mafilili, Rejao, Ribosome na wengine wanabeep na kupotea siku hizi nasikia hata zile bundle za bure nape kawanyima
Ni kweli Mkuu Rejao umepotea hapa jukwaani kwa sababu ya masuala ya posho? Ebu njoo ubhaelezee
 
Last edited by a moderator:
Wanalalamika hawalipwi inavyostahili kulingana na kazi wanayo ifanya ambayo huwa wanafanya mpaka usiku wa manane ikizingatiwa fungu limeongezeka katika bajeti mpya.

Naanza kuamini Rejao yupo kwenye mgomo!
 
Last edited by a moderator:
FF jamani sio kwamba kapotea ni kaolewa mitaa ya vingunguti kwa mnyamani na ustadhi wa madrasa kakatazwa na mmewe kwenda kushinda lumumba

Dah! Mshikaji we nomaaa!!! Kama FBI?!!! Ulijuaje? Anyway, asante kwa taarifa na tunashukuru dada yetu kupata stara.
 
Kuna hii kitu ilishaletwaga hapa watu wakadhani tunatania[SUP]1[/SUP]:

Mazungumzo kati ya NAPE na Rtz kwenye simu

Criiiii Criiii Criiii Criiii
Ritz:
Dah! Mheshimiwa anapiga simu. Naam Mkuu!

Nape:
Habari yako Comrade?

Ritz:
Salama tu Mheshimiwa

NAPE:
Kazi niliyowapa inaendaendaje?

Ritz:
Inaendelea vizuri tu Kamanda

NAPE:
Jana nilipita JF nikakakuta thread nyingi ni Pro-CDM

Ritz:
Ni kweli Kamanda. Tunaendelea kupambana si unajua mwanzo mgumu

NAPE:
Alafu hivi Malaria Sugu yupo? Sioni kabisa thread na coment zake siku hizi!

Ritz:
Afadhali umeuliza Mkuu. Usema kweli Rejao, Faiza Foxy na Malaria Sugu wananitegea sana. Na ndiyo maana thread za Pro-CDM zinaongezeka kwa sababu kazi inanizidi kimo

NAPE:
Waambie sitaki mchezo. Chama kinawalipa alafu kazi hawafanyi! Waambie ntawashtaki kwa Katibu Mkuu

Ritz:
Sawa Kamanda. Sasa Vipi kuhusu mishahara yetu ya mwezi uliopita na mwezi huu?

NAPE:
Wa mwezi uliopita mtalipwa mwezi huu ila wa mwezi huu msubiri kwanza. Si mnajua chama kina Crisis ya fedha. Ruzuku yenyewe si mnajua ni Shilingi 800 Million tu!

Ritz:
Sawa Kamanda. Kitu kingine Mkuu tufanyieni utaratibu mtununulie Laptop maana kazi ya kuingia kwenye Internet Café kufanya kazi ya Chama ni ngumu sana. Kwanza ni gharama na pia tunakuwa at risk kugundulika kwa Wananchi

NAPE:
Hilo ntalifanyia kazi. Kitu kingine?

Ritz:
Hamna Kamanda!

NAPE:
Sawa basi emu ingia sasa hivi JF Jukwaa la Siasa naona kuna thread inamuhusu Hamad Rashid, Regia Mtema na Godbless Lema. Emu kazicrash crash!

Ritz:
Sawa Mkuu!

NAPE:
Haya kazi njema Mpiganaji!

[SUP]1[/SUP] https://www.jamiiforums.com/jokes-u...zungumzo-kati-ya-nape-na-rtz-kwenye-simu.html
 
Kweli CCM inawatesa sana PRO-CDM kila siku mnazua mambo yasiyo na mashiko , ila bado wananchi hawawasikilizi, mkajifanya na JF ni yenu ila bado mkashindwa, mkanunua na kuanzisha magazeti km Tanzania Daima napo mkashindwa, mmefanya maandamano kila sehemu mkashindwa na hela zikawaishia mmeamua sasa kutulia, sasa msaidiwaje watu km nyie ????

Bingwa wa "rivasi"!!!
 
Hapa Jf wapo wa Chadema na CCM utawaona tu kwenye mijadala inayoendelea..... kila chama kimewalipa na kuwatuma wa kwake kama ni kweli wapo.

Hata hivyo tusiwachanganye wafuasi/mashabiki na waliotumwa.


Kweli humu janvini wapo wafuasi wa Chadema na pia wa CCm na hata CUF pia, lakini tuofauti kati yao ni kwamba wale wa M4C wako wengi na wanajitolea bila malipo; wanaongozwa na mapenzi ya chama chao lakini hawa wa magamba wako kazini hivyo wasipolipwa hawafanyi kazi!! Analogy hii iko pia kwa vyama hivi viwili vikubwa vinapofanya mikutano ya hadhara; M4C wanapofanya mikutano yao wananchi hawapelekwi mikutanoni na mabasi wanakwenda wenyewe lakini hawa magamba wanapofanya mikutano ya hadhara ni lazima wawafuate wanachama wao na mabasi na hela juu ama sivyo hawaendi mikutanoni!!
 
Hapa Jf wapo wa Chadema na CCM utawaona tu kwenye mijadala inayoendelea..... kila chama kimewalipa na kuwatuma wa kwake kama ni kweli wapo.

Hata hivyo tusiwachanganye wafuasi/mashabiki na waliotumwa.

Kama wewe umetumwa na ukibisha nitamwaga mtama hapa kwenye kuku uone aibu .
 
walikwenda kunywa chai ikulu...... Prof safari hasikiki chadema kulikoni??? Hata kesi zao mahakamani simuoni kama anashughulika wakati ni mwanasheria

prof safari ndiye anayedili na kesi ya kafumu kule igunga nasikia hali mbaya kwa kafumu
 
kama kweli kundi hilo lipo hakuna anayetupa habari zake naona tu kila mtu anajifanya kulijua bila kueleza liko wapi na linaundwa na akina nani..... Ni ishara ya habari za kutunga.

kwani nawe hujapata fungu nini? Maana naonaumepunguza propaganda hapa jf!
 
Hivi huyu jamaa Mwita25 au atiwm25 lienda wapi? huyu jamaa alikata tamaa mapema sana!!! FF naye wapi?

huyu mwita25 alikuwa balaaa na english yake ya kutoa kwenye vitabu na dictionary za biology na kemia
 
Alaa kumbe ndiyo yale magamba yaliyokuwa yanatetea wauaji bila hoja!! kweli dunia imejaa wapumbavu!!
 
Back
Top Bottom