CCM Lowassa kawaachia chama chenu, mbona mnakesha kumsema? Mwacheni

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Inashangaza sana kuona viongozi wa CCM badala ya kushughulikia shida na taabu za watanzania ambazo zimesababishwa na viongozi wake, wamekuwa kila kukicha wanamjadili Mh.Edward Lowassa.Hakika haiingii akilini kuona viongozi hao kuendelea kumsema na kumtukana Mh.Lowassa pasipo sababu ya msingi.Hivi wakiulizwa ni kwanini wanamtukana na kumsema Mh.Lowassa watajibu nini?

Hivi wakiulizwa ni kosa gani kubwa Mh.Lowassa amelifanya mpaka atukanwe ni lipi?

Pamoja na Mh. Lowassa kuwaachia chama chao kwanini wanamfuatafuata? Nadhani viongozi wa CCM mnapaswa kuacha kumchafua Mh. Lowassa kumbukeni yeye no binadamu ana mwili kama nyinyi.

Tunampongeza sana Mh.Lowassa kwa kuyavumilia matusi na kebehi zenu hakika Mh.Lowassa ni mtu wa mfano ameweza kuvumilia matusi hata ya watoto wake kina Nape, Makonda, Makongoro Nyerere n.k.

Mungu mpe maisha marefu Mh. Lowassa.
 
Lowassa alikuwa nguzo iliozuwia kuyumba kwa CCM muda wote huo baada ya kifo cha Nyerere. Waliobakia wote watu wa kupayuka na mipasho pia wapo mnawajua. Ndio maana wanamtukana baada ya kuja na mbinu za kuleta maendeleo.
 
CCM wote wanamuota lowassa, si JK, Mangula,si JPM,nasikia JPM anamtafuta mamvi amshauri kuhusu sukari
 
Arudishe mashamba aliyojimilikisha, ranchi, na rasilimali zoote alizojimilikisha wakati akiwa kiongozi hadi tukamkata akakimbia vinginevyo na wewe utulie.
 
arudishe mashamba aliyojimilikisha, ranchi, na rasilimali zoote alizojimilikisha wakati akiwa kiongozi hadi tukamkata akakimbia vinginevyo na wewe utulie..

Hahahhahaahaha Tajiri aishi kama shetani aka masikini? Hii ni ndoto za alinacha mkuu. Wewe endelea kuota tuu mchanamchana utakuja kuzinduka kila kitu kimekwisha.
 
Unaposema viongozi wa CCM wanamfuatafuata na kkumtukana ni viongozi gani hao? au unamaana wachangiaji humu JF ndio viongozi wa CCM? kama wewe ni mashauri mzuri wa Lowassa mshaurini akae kimya, uchaguzi umeisha hizi harakati zake za 2020 amewahi mno. Alituahidi akishindwa uchaguzi atarudi kuchunga ng'ombe au waliisha kugharimia uchaguzi?Ukimchokonoa chui na kijiti madhara yake ndiyo haya, hawakeri CCM pekee hata wanachama wa CHADEMA wanaojua taratibu za kumpata mgombea ndani ya chama inawakera anakigawa chama. Yeye sio Mungu mtu kwamba lazima kila mwaka agombee yeye demokrasia inataka watu kuomba ridhaa ya chama. Itokee ndani ya CHADEMA mtu mwingine naye asimame aseme atahakikisha anagombea 2020 nini matokeo yake.
 
CCM inafanya yale yafanywayo na mke aliyeachwa na mume huku bado anampenda. Wakubali tuu kuwa hayo yameshatokea.
 
  • Thanks
Reactions: Fdt
Hahaahahahhaahhahahahhahaahaha Tajiri aishi kama shetani aka masikini? Hii ni ndoto za alinacha mkuu. Wewe endelea kuota tuu mchanamchana utakuja kuzinduka kila kitu kimekwisha.
Eehh anataka Malaika waishi kama mashetani, lakini hataki watu wajadili ushetani wa kuuzwa nyumba za serikali.
 
CHADEMA imetia fora kwa kuwa chama cha kwanza kisicho madarakani, kujua mgombea wake wa uraisi miaka minne kabla
 
Walisema Lowassa kaisha ila kwa sasa wanakiri Lowassa ni chuma cha pua na kufuli limepiga kutu halifungi wala kufunguka
 

Attachments

  • VID-20160513-WA0012-1.3gp
    580.3 KB · Views: 33
  • VID-20160513-WA0012.3gp
    580.3 KB · Views: 31
Eehh anataka Malaika waishi kama mashetani, lakini hataki watu wajadili ushetani wa kuuzwa nyumba za serikali.
Amewambia kabla ya kuja huku kujadili uuzwaji wa nyumba za serikali, anzeni kujadili na mjumbe wenu wa Kamati kuu, Fredrick Sumaye ndiye alikuwa mtekelezaji wa maagizo ya serikali. Kama mnamuogopa, muulizeni Kubenea, aliwahi kujibiwa na Sumaye swali la uuzwaji wa nyumba za serikali.
 
Lowasa ni mwizi lazima kuandamwa kila kona ili abadilike kabisa kwa tabia yake ya wizi.
 
Back
Top Bottom