CCM: Liundi taja mamluki tuliowapandikiza upinzani

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
CCM: Liundi taja mamluki tuliowapandikiza upinzani

2009-01-01 13:44:58
Na Simon Mhina

Chama cha Mapinduzi CCM kimejibu shutuma dhidi yake zilizotolewa hivi karibuni na msajili wa kwanza wa vyama vya siasa, George Liundi kwamba kimepandikiza mamluki katika vyama vya upinzani, na kumtaka awataje kwa majina mamluki hao kama anataka aaminike.

Akizungumza na Nipashe, Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Kapteni John Chiligati, alisema amestushwa na madai hayo, ambayo kwa kiasi kikubwa yanashangaza.

``Liundi amesema kwamba akisutwa atataja majina ya mamluki waliopandikizwa upinzani na CCM, hilo limetufurahisha. Na sisi bila kuchelewa tumeanza kumsuta.

Tunamtaka atutajie hayo majina ya wapinzani feki tuliowapandikiza kwenye vyama vya siasa nchini,`` alisema Chiligati.

Alisema CCM ni chama imara ambacho hakitegemei kupata nguvu wala msaada wowote kwa mamluki, kwa vile tangu kianzishwe Watanzania wameonekana kukiunga mkono pasipo na shaka yoyote.

Alipoulizwa kwamba CCM itakuwa tayari kuwajibika iwapo Liundi atataja majina hayo, Katibu huyo alisema hawezi kuyataja kwa vile sio jambo la kweli.

Alihoji ni kwa vipi awafumbie macho`mamluki` kwenye vyama vya upinzani wakati wote, wakati yeye alidai kwamba alifanya kazi yake kwa mujibu wa sheria, bila kuyumbishwa na mtu?

Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema hali inayoonyesha ni kwamba hivi sasa Liundi anayo matatizo makubwa ndiyo yamemsukuma kutoa madai hayo ya uongo.

Alipoulizwa kwamba anafahamu matatizo yanayomkabili Liundi, alisema: ``Anayo matatizo ya kiubinadamu.``

Alisema iwapo Liundi hatotaja majina ya wanasiasa mamluki ndani ya upinzani, watachukulia madai hayo ya Liundi kwamba ni matokeo ya matatizo hayo aliyonayo.

``Yeye amesema akisutwa atawataja, sasa kaandike kwamba tumemsuta kweli kweli, ili awataje,`` alisema Chiligati, ambaye katika siku za karibuni amekuwa akijibu kila kauli inayotolewa kukikosoa chama tawala.

Huko nyuma aliyekuwa mwepesi kujibu alikuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba.

Hivi karibuni, Liundi alikaririwa na gazeti hili katika mahojiano maalum akisema kuwa anawajua mamluki wote waliopandikizwa na CCM kwenye vyama vya upinzani kwa lengo la kuvihujumu.

Liundi alienda mbali zaidi akasema kutokana na CCM kuhofu upinzani, kuna wakati viongozi walichanganyikiwa wakala njama za kuvunja mfumo wa vyama vingi nchini.

Alisema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyezima jaribio hilo baada ya yeye (Liundi) kwenda nyumbani kwake kumlalamikia kuhusu mpango huo.

SOURCE: Nipashe
 
wale wana-chadema waliokusanyika dar wakati wa kampeni Tarime na kupingana na Dr.Slaa kwenye sakata la mke wa Wangwe ni mamluki. tambwe hiza alikuwa mamluki ndani ya CUF na ngawaiya alikuwa TLP
 
Kwa jinsi ninavyomfahamu Mzee Liundi nadhani watu ambao wamejitokeza kumsaidia kwa madai ya kumtoa kwenye hali mbaya ikiwa ni pamoja na kukaa 'uswazi' huenda wanamshauri vibaya au wanafanya hivyo kwa kuangalia maslahi yao binafsi na wala siyo ya huyu Mzee.

Kama kweli kauli zilizoripotiwa na kwenye vyombo vya habari ni za kwake kweli basi ana kila hali ya kuuomba umma wa watanzania msamaha kwa kutumia vibaya madaraka ya ofisi yake. Ni huyuhuyu mzee mara tu alipomaliza muda wake wa utumishi serikalini aliomba ubunge kupitia CCM, akapigwa chini au ndiyo zile siasa za 'sizitaki mbichi hizi'.

Mzee Liundi kama alivyo Mangula ni vema wakatambua kuwa ufisadi walioufanya huko nyuma sasa unawatafuna wakae chiini watubu makosa yao kwa kutowatendea haki watanzania badala ya kutafuta cheap popularity.

Lakini akumbuke kuwa at the end of the day he's going to be responsible kwa kauli na vitendo vyake kama ambavyo anavyoishi sasa kwani ni matokeo ya kuwajibika kwa vitendo vyake mwenyewe.
 
INAOGOPESHA!!!!!!!!!! Mh !!!
Mbona shutuma za wale waliopewa dhima kubwa kwa Taifa mbele ya wateule zimepamba moto. Aidha upo ukweli wa shutuma hizi au upo udhaifu wa kuteuliwa watu wanaopewa dhima za Taifa. Iwapo ubinaadamu wao kama tunapoambiwa na Chiligati ndio unaowapelekea kutowa shutuma hizo baada ya kukosa fupa basi hatuko makini kuchaguwa watu wa kupewa dhima. Iwapo kuna ukweli kwa wanayoyasema na wakaamua kuyasema baada ya kukosa fupa pia lipo tatizo la kutokuwa na waadilifu kwenye safu zetu.

Hata hivyo shutuma zinazojirejea rejea mara nyingi huwa na ukweli ndani yake hivyo CCM mnani? Mnatutendea yepi sisi wananchi wenzenu? Mnapogombana kidogo tu mambo yanafichuka tofauti na wapinzani uchafu wao unawazuru wenyewe kwa wenyewe uchafu wenu CCM unatuumiza kwani nyie ndio wateule wetu katika kuiongoza nchi.
 
Hii kauli ya Liundi haifai iishe hivihivi, jamaa alikuwa msajili wa vyama, na akaona hao Mamluki wanapandikizwa akawa kimya, sasa ndio anakenua kuhusu mamluki. Huenda yeye ndio mamluki...
 
``Liundi amesema kwamba akisutwa atataja majina ya mamluki waliopandikizwa upinzani na CCM, hilo limetufurahisha. Na sisi bila kuchelewa tumeanza kumsuta.

Tunamtaka atutajie hayo majina ya wapinzani feki tuliowapandikiza kwenye vyama vya siasa nchini,`` alisema Chiligati.

Alisema CCM ni chama imara ambacho hakitegemei kupata nguvu wala msaada wowote kwa mamluki, kwa vile tangu kianzishwe Watanzania wameonekana kukiunga mkono pasipo na shaka yoyote.

Alipoulizwa kwamba CCM itakuwa tayari kuwajibika iwapo Liundi atataja majina hayo, Katibu huyo alisema hawezi kuyataja kwa vile sio jambo la kweli.

Alihoji ni kwa vipi awafumbie macho`mamluki` kwenye vyama vya upinzani wakati wote, wakati yeye alidai kwamba alifanya kazi yake kwa mujibu wa sheria, bila kuyumbishwa na mtu?

Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema hali inayoonyesha ni kwamba hivi sasa Liundi anayo matatizo makubwa ndiyo yamemsukuma kutoa madai hayo ya uongo.

Alipoulizwa kwamba anafahamu matatizo yanayomkabili Liundi, alisema: ``Anayo matatizo ya kiubinadamu.``

Alisema iwapo Liundi hatotaja majina ya wanasiasa mamluki ndani ya upinzani, watachukulia madai hayo ya Liundi kwamba ni matokeo ya matatizo hayo aliyonayo.

``Yeye amesema akisutwa atawataja, sasa kaandike kwamba tumemsuta kweli kweli, ili awataje,`` alisema Chiligati, ambaye katika siku za karibuni amekuwa akijibu kila kauli inayotolewa kukikosoa chama tawala.

Huko nyuma aliyekuwa mwepesi kujibu alikuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba.

Hivi karibuni, Liundi alikaririwa na gazeti hili katika mahojiano maalum akisema kuwa anawajua mamluki wote waliopandikizwa na CCM kwenye vyama vya upinzani kwa lengo la kuvihujumu.

Liundi alienda mbali zaidi akasema kutokana na CCM kuhofu upinzani, kuna wakati viongozi walichanganyikiwa wakala njama za kuvunja mfumo wa vyama vingi nchini.

Alisema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyezima jaribio hilo baada ya yeye (Liundi) kwenda nyumbani kwake kumlalamikia kuhusu mpango huo.
Hii issue iliishia wapi? Kuna waandishi walimchochea zaidi Liundi?
 
Hii issue iliishia wapi? Kuna waandishi walimchochea zaidi Liundi?

Mara ya Mwisho ilikuwa kama ifuatavyo; sijui baada ya taarifa hii mambo yaleindeleaje.

Liundi ataja mamluki

2009-01-26 10:50:49
Na Simon Mhina

Aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, George Liundi ameamua kuwataja mamluki waliojipenyeza katika vyama vya upinzani kidiplomasia.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum yaliyofanyika `nyumbani kwake` Mabibo, Dar es Salaam, mstaafu huyo alisema alishangaa kusikia kwamba kuna watu wanamsuta, wakati mamluki wote wanajulikana kwa sura na kwa majina.

``Suala la mamluki waliopo upinzani kwangu mimi sioni kama ni jambo jipya, mamluki wote wanajulikana. Kwa mfano wanaotaka kujua mamluki ni kina nani, wanapaswa waende wakawaulize watu waliokuwa upinzani hususan Chama cha NCCR-Mageuzi, kwamba ilikuwaje wakarudi CCM? Wakaulize waliokuwa vinara wa CUF, imekuwaje ghafla wamebadili msimamo? Kitu gani hasa kimetokea? Jibu ambalo watatoa, watajulikana mamluki ni kina nani,`` alisema Liundi.

Mstaafu huyo aliongeza: ``Unakuta mtu alijiunga na upinzani akiwa mtu mzima, ghafla anasema amegundua eti upinzani hauna sera. Ilikuwaje ajiunge na chama ambacho hakina sera? Angejiunga akiwa mtoto pengine tungesema hakuelewa anachokifanya.``

Hata hivyo, alisema si lazima mamluki hao wawe wamepandikizwa kwenye upinzani na CCM.

Alisema wengine walijipenyeza kwenye vyama vya upinzani, na kujifanya vijogoo wa siasa, kwa lengo la kufanya biashara ya ruzuku.

Kuhusu madai ya Katibu Mwenezi wa CCM, John Chiligati ya kumtaka ataje majina ya mamluki hao, Liundi alisema Katibu huyo anataka kukiumbua Chama tawala, hatua ambayo yeye hawezi kushiriki.

Vilevile, alisema kauli hiyo ya Chiligati, ilikuwa na lengo la `kumtega` kwa vile yeye akiwa mtumishi mwandamizi mstaafu wa serikali, hawezi kutoa siri za ofisi.

Liundi alisema kauli yake ambayo ilinukuliwa na gazeti hili hivi karibuni, imemfanya azongwe zongwe na baadhi ya watu.

``Japokuwa msimamo wangu una ukweli, lakini wengine wamekuwa wakiniuliza kwanini kusema mambo haya hivi sasa kuna faida gani? Wanataka ninyamaze nipumzike,`` alisema.

Kuhusu maisha yake, Liundi alisema pamoja na matatizo ya kiubinadamu ambayo yanampata kila mtu, halali njaa na hajioni kama kuna kitu amepungukiwa.

Alisema pamoja na kwamba anaishi Mabibo, lakini si kweli kwamba eneo hilo ni uswahilini.

``Nimesoma taarifa za John Tendwa (Msajili wa sasa) na zile zilizotolewa na Chiligati akidai nina `matatizo`, wasifikiri kwamba nina dhiki sana. Mimi nimeridhika na maisha niliyo nayo, sina sababu ya kumpigia mtu magoti, bali Mwenyezi Mungu,`` alisema.

Alisema ameridhika na maisha aliyo nayo, kwa vile yanatokana na jasho lake na hakuna anayemdai.

  • SOURCE: Nipashe
 
``Suala la mamluki waliopo upinzani kwangu mimi sioni kama ni jambo jipya, mamluki wote wanajulikana. Kwa mfano wanaotaka kujua mamluki ni kina nani, wanapaswa waende wakawaulize watu waliokuwa upinzani hususan Chama cha NCCR-Mageuzi, kwamba ilikuwaje wakarudi CCM? Wakaulize waliokuwa vinara wa CUF, imekuwaje ghafla wamebadili msimamo? Kitu gani hasa kimetokea? Jibu ambalo watatoa, watajulikana mamluki ni kina nani,`` alisema Liundi.
Inawezekana hata Tendwa anawajua mamluki tusubiri tu aondoke tutasikia mengi
 
Tatizo la nchi hii ni kwamba wale ambao hawanufaiki na system iliyopo ndo wanapiga kelele. Kama Liundi ni muwazi atje hayo majina na sio kusingizia kua ataua anatoa siri, kama ni siri kwanini aliyasema hayo kaika media???au anataka popularity?aende CCJ asi kama kweli amechoshwa...
 
Ndg WanaJF,

Tunao wapuuzi wengi ambao wamepewa madaraka wayatumie kwa mujibu wa sheria lakini wanapindisha kwa makusudi kwa manufaa yao binafsi au kundi lao/ chama chao.
Liundi ni mfano mmoja wa watu wa aina hiyo na wanatakiwa walaaniwe sana katika jamii yetu.
Hawa ndio asili ya mmomonyoko wa maadili tunaoulalamikia sasa.
Ni lazima mtu yeyote aliyepewa madaraka katika ofisi ya uma aelewe kwamba anapaswa kufanya kazi kwa haki na kwamba ipo siku ataondoka na ofisi itabaki pale pale.
Kumbukeni Liundi hakutakiwa kuwa mwanchama akiwa msajili, lakini mara alipokabidhi ofisi alitaka ubunge kupitia CCM. Hii ikimaanisha alikuwa mwanachama!
Kwa nini tusimuweke katika list ya watu wasio waadilifu waliowahi kutumikia TZ?
 
Kuna ubaya gani kupandikiza watu kwenye chama pinzani...kila chama lazima kifanye hivo kama inteligencia yake..ikiwa vingine havifanyi basi kalagabaho...mtanedelea kuburuzwa tuu...

CCJ ikiwa nyie viongozi hamjapandikizwa basi fanyeni mpandikize kila mahali ili muwe strong from the beginning..tena mlifanya makosa sana Mpendazoe kujiunga nanyi mapema..angeendelea kubaki hukohuko huku akifanya kazi kama kibaraka wenu...lasivyo mjue huyo pia kapandikizwa kwenu..simmesikia analipwa mshahara wa ubunge mpaka leo
 
Back
Top Bottom