CCM lazima itashinda Uchaguzi wa Ubunge Kinondoni

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Mara kwa mara kwenye mikutano ya kampeni za ubunge jimbo la Kinondoni nimekuwa nikimsikia Mbunge wa Mtera, Mhe. Livingstone Lusinde akisema tena kwa kujiapiza kuwa lazima CCM ishinde Ubunge jimbo la Kinondoni.

"Afe Kipa, afe Beki CCM lazima itashinda kiti cha Ubunge Kinondoni. Mtulia ndio Mbunge wa jimbo la Kinondoni" alisema Mhe. Livingstone Lusinde, MB (MNEC).

Nimejaribu kufanya utafiti mdogo wa kisayansi kubaini uhalisia wa kauli ya Lusinde.

Twende sawa. Waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2015 jimbo la uchaguzi la Kinondoni walikuwa jumla ni 267,439.

Baada ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni mwaka 2015 walijitokeza wapigakura 192,556 sawa na 72% ambapo matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:-

CUF walipata kura 70,337; CCM walipata kura 65,964; Huku kura 56,255 zikigawanyika kwa vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi ikiwemo ACT WAZALENDO na wengine.

Ifahamike tu kwa jimbo la Kinondoni CCM ndio chama chenye Wanachama wengi kuliko chama kingine chochote wakifuatiwa kwa mbali sana na Chama cha Wananchi CUF.

Katika kata kumi zinazounda jimbo la Kinondoni CCM ina matawi yapatayo 62 na mashina 1,129 ambayo yana wanachama wa wastani wa takribani 67-73 kwa shina moja. Hivyo kuifanya CCM kuwa na wanachama takribani 75,643 hadi 82417.

Pia tusisahau kuna kura alizozipata Mtulia mwaka 2015 ya zaidi ya kura 70,000. Katika hizi kura Mtulia ana uhakika wa kupata si chini ya kura 60,000.

Kwa mantiki hiyo uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni CCM itashinda kwa kishindo kwa sababu ya wingi wa Wanachama, utendaji bora kabisa wa Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 - 2020 katika eneo hilo pamoja na mipango waliyonayo ya kimaendeleo kwa Kinondoni.

Pia ni kwa sababu CCM ni chama bora chenye umoja, utulivu na utayari wa kutatua matatizo ya Wananchi, udhaifu mkubwa wa washindani wake ambao ni CUF (CUF ya Maalim Seif na CUF ya Lipumba) na Chadema ambayo imegubikwa na wimbi kubwa la hamahama ya viongozi na wanachama wao kutokana na migogoro ya ndani.

Vilevile utitiri wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi huu mdogo vipatavyo 12, kufa kwa ukawa kwani wote wamesimamisha wagombea na ukigeugeu wa Chadema kunaipa CCM njia nyeupe ya kushinda.

Njia ya ushindi kwa Maulid Mtulia kuwa Mbunge wa Kinondoni ni nyeupe. Siasa ni Sayansi.

Na Shilatu E.J
Kinondoni
 
Nilishawahi kusema mwanzoni kabla ya uchaguzi kuwa Mtulia Lazima atadhinda ubunge kwahoja zifuatazo (1) kamakweli amenunuliwa na ccm,watafanya kilaliwezekanalo ili ashinde kamahizo mlizozisikia (2) polepole alishasema kabla ya uchaguzi kuwa "tunasubiri kuapishwa mbunge wetu kwani tayari ameshapita (3)Hao wanaodaiwa kumnunua Mtulia wasingekubali ashindwe na mpinzaniwake kwani watapata fedheha kubwa kutoka kwa wapinzani
 
Hizi ni hisia zako tu Mkuu. Tatizo la chadema ni kudharau wapiga kura.
 
Mikutano mingi ya upinzania wanajaa wahuni wasio na kadi za kupigia kura.Uchaguzi ni mathematics.
 
Mikutano mingi ya upinzania wanajaa wahuni wasio na kadi za kupigia kura.Uchaguzi ni mathematics.
Haya maneno yalitumiwa na akina Mrema miaka ya 1985. Siyo sasa, kwa sasa watu wameelimika na hawadanganywi kipumbavu, wanajua wanachofanya na wanajua wanachofanyiwa.
Hoja nyepesi sana mbele za wenye akili.
 
Back
Top Bottom