CCM kwafuka watishiana kupelekana mahakamani??

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,191
674
Posted Date::10/8/2007
CCM kwafuka watishiana kupelekana mahakamani
Na Abdallah Nsabi, Maswa

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa, Mkoa wa Shinyanga, Hasani Tindo ametishia kuwafungulia mashtaka baadhi ya vigogo wa chama hicho kwa kumfedhehesha na kumkashifu kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi yake kwa viongozi wa juu wa CCM.


Dhamira hiyo aliitangaza mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Maswa kuhusiana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake na vigogo hao wa wilaya huyo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba.


Tindo alisema kuwa, tuhuma kwamba alizunguka wilaya yote ya Maswa na kuwazuia wajumbe wa halimashauri kuu ya hicho wasihudhulie mkutano wa Makamba uliofanyika Sept 22, ni mbaya na zimempaka matope ndani ya chama hicho.


Alidai kuwa, amekuwa mwadilifu katika kukitumikia chama kwa muda wa miaka 15 sasa bila shutuma au ya kashfa yoyote.


"Shutuma dhidi yangu si za kweli bali ni uzushi na upotoshaji wa kweli uliolenga kuchafua jina langu na kunishushia hadhi mbele ya wanaCCM kwa ujumla, shutuma hizi zimeniathiri kwa kiwango kikubwa sana sijawahi kupata tuhuma kama hizi nitafungua kesi mahakamani kama Hasani Tindo na si mjumbe wa halimashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Maswa ," alisisitiza Tindo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Biafra.


Alisema kuwa shutuma hizo ni nzito kwa kuwa pia, zimchafulia wasifu wake wa vitendo na tabia mbele ya viongozi ya viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na taifa.


Tindo alisema amemwandikia barua mmoja wa vigogo hao, akimtaka athibitishe tuhuma hizo na nyingine alizozisema mbele ya Makamba ndani ya siku saba, akishindwa anampeleka mahakamani .


"Siwezi kutaja kiwango cha fidia, nitakitaja mahamani kesi nitafungua haraka iwezekanavyo baada ya muda niliompa kuisha na ninawasiliana na wanasheria ndio watakaojua watafungua katika mahakama ipi, " alisisitiza.


Vilevile wanachama wengine wanaotuhumiwa kukwamisha mkutano huo, Mbunge wa Maswa, John Shibuda, ameonyesha nia yake ya kuwashitaki viongozi hao na Makamba kwa madai ya kumzulia uongo na kumtangaza hadharani kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga na baadhi ya wilaya.


Kutokana na mvutano huo uliojitokeza, viongozi hao wa wilaya waliitisha kiako cha dharula cha kamati ya siasa wiki iliyopita na kuazimia kuwahoji waandishi wa habari wawili ,akiwemo wa habari hizi sababu za kuripoti mgogoro ndani ya chama hicho.


Hivi karibuni Makamba akiwa ziarani mkoani Shinyanga, Makamba alishindwa kufanya mkutano wa wajumbe wa halimashauri Kuu ya CCM Maswa kutokana na wengi kutohudhuria .


Wakati huo huo; Viongozi wa CCM Wilaya wamekana kauli ya Makamba ya kuwapo mgawanyiko ndani ya chama hicho na kudai watu wanaodai hivyo waongo wasiokitakia mema chama hicho.


Kauli hiyo ilitolewa na katibu wa chama hicho wilayani hapa, Mberito Magova wakati akitoa taarifa kwa wajumbe wa NEC na Mkutano Mkuu taifa wa CCM Mkoa wa Manyara, Dk Mary Nagu na Mkoa wa Mbeya, Profesa Mark Mwandosya.


Kwa upande wake, Mbunge Shibuda alikiri kuwapo kwa mgogoro huo na kutoa vielelezo huku akiungwa mkono na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, wakisema umesababisha kujengeana chuki baina yao.


Kwa upande wake, Mwandosya aliwaomba viongozi na wanachama wa CCM Maswa kuacha tofauti zao na kulaumu uongozi huo kutaka kuwapotosha kuhusiana na mgogoro huo kama ambavyo umekuwa ukiripotiwa katika vyombo vya habari.

source mwananchi
 
Back
Top Bottom