Tetesi: CCM kwachafuka, sasa wachunguzana, hakuna kuaminiana

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
SIRI (CONFIDENTIAL).

Chama cha mapinduzi CCM kumeibuka hali ya taharuki, wamekuwa wakifanyiana ushushushu kila kona, na kwa kila mjumbe wa halmashauri kuu, mkutano mkuu na kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa, na hivi sasa ngazi husika hazipati usingizi, zinashughulikia hilo, ili kuepukana na baadhi ya wajumbe kususia mikutano na vikao vinavyoendelea huko Dodoma.

Zimeundwa Kamati za siri, kwaajili ya kuwafuatilia, kuwabaini na kuwachunguza wanachama na makada ambao wameonekana kutofautiana na kundi lingine ndani ya chama hicho, ikumbukwekuwa mpaka hivi sasa ndani ya chama cha mapinduzi kumeibuka makundi mawili imara, yasiyokubaliana kabisa katika masuala ya msingi na yaliyoshikilia uhai wa chama hicho.

Kundi moja ni lile linalounga mkono kila jambo linalofanywa na kuamuliwa na Mhe. Magufuli, na kundi lingine ni lile linalo hoji kila hatua inayopigwa kwa upande wa chama na serikali, kutokukubaliana na maamuzi ya pupa, uminywaji wa sauti za watu kwenye chama na serikali, maamuzi kutoka upande mmoja yasiyozingatia usawa, na imebainika kuwa sababu za Mhe. Kikwete kuamua kwa hasira kuuacha uenyekiti ni kile kilichosemekana kuwa kuna mtu ambaye ana madaraka serikalini lakini amekuwa akisukuma hoja zake ndani ya chama na kuunda genge lake, yaani kukiteka chama na kuamua kukiendesha bila mpangilio, ilhali hana uongozi wowote ndani ya chama hicho, na hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa kijiji.

Kamati hizo za siri pia zimekuwa na jukumu la kuwabaini wajumbe waliokusudia kususia mikutano hiyo, na endapo watapanga kuzungumza na vyombo vya habari, basi wazuiliwe na wakabiliwe vikali, ikiwezekane wakamatwe na wafungiwe kwenye afisi ndogo, hapo hapo mjini Dodoma, mpaka shughuli nzima ya Chama itakapokamilika.

Aliniambia kada mmoja na kiongozi wa chama hicho kwa njia ya VoIP (Voice over IP) na hakupenda kutajwa jina lake kuwa: kamba ya kuunda kamati hizo za siri, tulikuwa na mkakati wa kuwaita wanachama mmoja mmoja tangu wiki mbili zilizopita, tukakaa nao katika sekretarieti, na kuwaonya, tuliwaambia ni marufuku kufanya wala kusema lolote kinyume na maelekezo, na hakuna kuzungumza masuala ya chama, anayepaswa kuyazungumza ni Msemaji wa chama tu"

Pia, moja ya agenda zinazosadikika kwenda kuzungumzwa, katika vikao vya siri, ili kuwa na mwongozo sahihi katika mkutano mkuu, ni ukimya wa Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, imellamikiwa kuwa bado kuna kundi kubwa linalounga mkono CHADEMA/UKAWA kwa siri siri, jambo ambalo sio afya kwa CCM, na namna ya kuwadhibiti wapinzani, hususan CHADEMA/UKAWA wasipate fursa ya kuongea na wananchi, lakini hilo lisiwaathiri CCM katika kufanya siasa na mikutano ya kisiasa kwa mgongo wa serikali. Pia, kumjadili Maalim Seif, na namna ya kumdhibiti asifanye kile alichokikusudia, kinachomnyima usingizi Dr. Shein na serikali yake.

BAVICHA bado ni kitendawili kwao, na wameshindwa kukitegua. Kuna taarifa zinazowachanganya, wanaambiwa kuwa BAVICHA wapo kamili na watauzuia mkutano, wengine wanawaambia hawatakuwepo kwani wameambiwa na Mwenyekiti wao wasiende Dodoma... lakini kutokana na Kinachooneshwa na Jeshi la polisi kile kilichoitwa maandalizi ya kuwakabili BAVICHA, kimeibua hoja, na CCM ngazi ya Taifa imechukua hatua ya kujitafakari kwa kuona kuwa BAVICHA imeungwa mono na vijana wengi kuliko UVCCM, imewafanya kuamini kuwa vijana wa CCM UVCCM ni mizigo inayosubiri kupewa vyeo, hakuna wanalolifanya zaidi ya kujipendekeza, hivyo unaandaliwa mkakati maalum wa kuhakikisha uongozi wa UVCCM unaangushwa mara moja.

Hayo ni machache, mengine nitawajulisha muda mchache ujao, mnyetishaji wangu kadiri atakavyokuwa anaendelea kunipa nyeti hizi za chini ya kapeti, kwa umakini mkubwa.
 
Tupatie na yale yaliyojadiliwa kwenye kikao cha bavicha Regency mikocheni, ambapo Lowasa alikuwepo.
 
Kama kupasuka CCM ingepasuka July 12 2015. Jengeni Vyama vyenu mkisubiri CCM ipasuke ndio mkamate Dola ni sawa na kusubiri Boti ya Znz Ubungo bus terminal
Ni kweli mkuu, misingi ya ccm ni imara na inahitajika muda sana kuweza kuiondoa, wanatoka watu, wanaingia watu..
 
SIRI (CONFIDENTIAL).

Chama cha mapinduzi CCM kumeibuka hali ya taharuki, wamekuwa wakifanyiana ushushushu kila kona, na kwa kila mjumbe wa halmashauri kuu, mkutano mkuu na kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa, na hivi sasa ngazi husika hazipati usingizi, zinashughulikia hilo, ili kuepukana na baadhi ya wajumbe kususia mikutano na vikao vinavyoendelea huko Dodoma.

Zimeundwa Kamati za siri, kwaajili ya kuwafuatilia, kuwabaini na kuwachunguza wanachama na makada ambao wameonekana kutofautiana na kundi lingine ndani ya chama hicho, ikumbukwekuwa mpaka hivi sasa ndani ya chama cha mapinduzi kumeibuka makundi mawili imara, yasiyokubaliana kabisa katika masuala ya msingi na yaliyoshikilia uhai wa chama hicho.

Kundi moja ni lile linalounga mkono kila jambo linalofanywa na kuamuliwa na Mhe. Magufuli, na kundi lingine ni lile linalo hoji kila hatua inayopigwa kwa upande wa chama na serikali, kutokukubaliana na maamuzi ya pupa, uminywaji wa sauti za watu kwenye chama na serikali, maamuzi kutoka upande mmoja yasiyozingatia usawa, na imebainika kuwa sababu za Mhe. Kikwete kuamua kwa hasira kuuacha uenyekiti ni kile kilichosemekana kuwa kuna mtu ambaye ana madaraka serikalini lakini amekuwa akisukuma hoja zake ndani ya chama na kuunda genge lake, yaani kukiteka chama na kuamua kukiendesha bila mpangilio, ilhali hana uongozi wowote ndani ya chama hicho, na hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa kijiji.

Kamati hizo za siri pia zimekuwa na jukumu la kuwabaini wajumbe waliokusudia kususia mikutano hiyo, na endapo watapanga kuzungumza na vyombo vya habari, basi wazuiliwe na wakabiliwe vikali, ikiwezekane wakamatwe na wafungiwe kwenye afisi ndogo, hapo hapo mjini Dodoma, mpaka shughuli nzima ya Chama itakapokamilika.

Aliniambia kada mmoja na kiongozi wa chama hicho kwa njia ya VoIP (Voice over IP) na hakupenda kutajwa jina lake kuwa: kamba ya kuunda kamati hizo za siri, tulikuwa na mkakati wa kuwaita wanachama mmoja mmoja tangu wiki mbili zilizopita, tukakaa nao katika sekretarieti, na kuwaonya, tuliwaambia ni marufuku kufanya wala kusema lolote kinyume na maelekezo, na hakuna kuzungumza masuala ya chama, anayepaswa kuyazungumza ni Msemaji wa chama tu"

Pia, moja ya agenda zinazosadikika kwenda kuzungumzwa, katika vikao vya siri, ili kuwa na mwongozo sahihi katika mkutano mkuu, ni ukimya wa Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, imellamikiwa kuwa bado kuna kundi kubwa linalounga mkono CHADEMA/UKAWA kwa siri siri, jambo ambalo sio afya kwa CCM, na namna ya kuwadhibiti wapinzani, hususan CHADEMA/UKAWA wasipate fursa ya kuongea na wananchi, lakini hilo lisiwaathiri CCM katika kufanya siasa na mikutano ya kisiasa kwa mgongo wa serikali. Pia, kumjadili Maalim Seif, na namna ya kumdhibiti asifanye kile alichokikusudia, kinachomnyima usingizi Dr. Shein na serikali yake.

BAVICHA bado ni kitendawili kwao, na wameshindwa kukitegua. Kuna taarifa zinazowachanganya, wanaambiwa kuwa BAVICHA wapo kamili na watauzuia mkutano, wengine wanawaambia hawatakuwepo kwani wameambiwa na Mwenyekiti wao wasiende Dodoma... lakini kutokana na Kinachooneshwa na Jeshi la polisi kile kilichoitwa maandalizi ya kuwakabili BAVICHA, kimeibua hoja, na CCM ngazi ya Taifa imechukua hatua ya kujitafakari kwa kuona kuwa BAVICHA imeungwa mono na vijana wengi kuliko UVCCM, imewafanya kuamini kuwa vijana wa CCM UVCCM ni mizigo inayosubiri kupewa vyeo, hakuna wanalolifanya zaidi ya kujipendekeza, hivyo unaandaliwa mkakati maalum wa kuhakikisha uongozi wa UVCCM unaangushwa mara moja.

Hayo ni machache, mengine nitawajulisha muda mchache ujao, mnyetishaji wangu kadiri atakavyokuwa anaendelea kunipa nyeti hizi za chini ya kapeti, kwa umakini mkubwa.

Wako katika demokrasia na maendeleo
Goodluckies Good/ Goodluck Abel

Hizi ngonjera sisizo NA mbele wala nyuma hazitasaidia kuokoa Upinzani. Hoja zimefilisika sasa Ni kupika majungu tu... Mtasubiri sana....
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom