Ccm kwa sasa wanaendesha nchi kwa maelekezo ya chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm kwa sasa wanaendesha nchi kwa maelekezo ya chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Apr 28, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF na wapenzi wa JF,

  Napenda kusema kuwa CHADEMA kimejidhihirisha kuwa ni Chama Makini ambacho kina maamuzi magumu na mazuri kwa ajili ya maslahi ya Taifa letu. Hakika CHADEMA kwa sasa ndicho Chama kinachoendesha nchi hii kikiwa nje ya Ikulu(Remote control). Hii inatuonyesha picha ya kwamba CHADEMA ndicho kilistahili kuwa pale Ikulu (White House)kama isingelikuwa mambo ya uchakachuaji wa Kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010. Nitaeleza.

  Kuna mambo matatu makubwa sana ambayo CHADEMA wamesababisha yafanyike ndani ya serikali ya CCM nayo ni haya yafuatayo:

  1. Mchakato wa kuundwa kwa Katiba Mpya. Hii ni HOJA ILIYOANZISHWA NA KUUPIGIWA KELELE NA CHADEMA BUNGENI mpaka serikali ya CCM chini ya Rais wake Kiwete wakaelewa somo na kukubaliana na HOJA hiyo ambayo tayari Tume yake inaanza kazi mwezi wa Mei,2012. Kumbuka CCM hawakuwa na hoja hii kwenye ILANI yao ya Uchaguzi ya 2005/2010. Hoja hii Ilipoanza ilipingwa kwa nguvu sana na Serikali wakiwemo Waziri wa Sheria, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri na Wabunge wa CCM! Kiwete aliweza kusoma alama za nyakati ikabidi amwage manyanga na kukubaliana na HOJA YA KUWA NA KATIBA MPYA! Hii ndiyo KAZI ILIYO BORA KABISA ILIYOFANYWA NA CHADEMA kuwapatia Watanzania kitu chema-Katiba Mpya!
  2. Kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri baada ya HOJA YA CHADEMA kupitia Mbunge wake machachari Mhe.Zitto Kabwe baada ya CAG kuanika UOZA WA UFUJAJI WA MABILIONI NDANI YA SERIKALI YA CCM. Hoja ya KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU iliibuliwa na Zitto Kabwe pasipo matarajio ya Wabunge wa CCM na Serikali yao. Hakika wamekutwa ''OFF GUARD''! Pamoja na juhudi za kutaka kuizima hoja hii kwa mizengwe mbalimbali kupitia Spika Makinda, William Lukuvi,Pinda mwenyewe na majority ya Wabunge wa CCM bado ngoma ikabakia palepale. HII NI KAZI NYINGINE NZURI YA CHADEMA.
  3. Hivi karibuni mwanzoni wa mwaka huu wa 2012, Rais Kiwete kama kawaida yake alifanya ziara ya KUTEMBELEA NCHI ZA NJE HUKU AKINDAMANA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA SERIKALI AMBAPO MSAFARA HUO ULIGHARIMU SH.400 MILLIONI FEDHA YA WALIPA KODI. CHADEMA kwa heshima na taadhima ikaiambia Serikali msafara wa Rais kutumia Shs.400 milioni kwa mara moja ni UFISADI NA FUJAJI WA PESA YA WATANZANIA. Kiwete aliporudi alikuta hoja hiyo ikichemka jikoni na kwa maneno yake mwenyewe akasema KUNA HAJA SASA SERIKALI IANGALIE UPYA ZIARA ZINAZOFANYWA NJE YA NCHI ILI KUPUNGUZA GHARAMA. Naamini hili limeshafanyiwa kazi maana hata juzi Kiwete alivyokimbilia BRAZIL kukwepa joto la kisiasa la kutokuwa na IMANI NA PM msafara wake ulikuwa wa watu wachache sana. HIYO NAYO NI KAZI NZURI YA CHADEMA.

  Inavyoelekea huko tuendako hoja na sera za CHADEMA ndizo zitazidi kutamalaki mpaka mwaka 2015 wakti CHADEMA watakapoingia IKULU rasmi.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja CHADEMA kikweli ni wapambanaji ndiyo wanajua uchungu wa nchi hii.
   
 3. n

  nketi JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo nyumba ccm ilikuwa inaendesha nchi kwa maelekezo ya dr.slaa......sasa wamejinyea wanasutana...nchi inaendelea kuangamia
   
 4. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni dhahiri mkuu!!
   
 5. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  JK hakumbuki tena sera wala ilani ya CCM, anachokifanya ni kufuata mwangwi wa M4C!
   
 6. O

  One Man Army JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  viva chadema
   
 7. M

  Makwarukwaru Member

  #7
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  M4c kazini.
   
 8. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #8
  Apr 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Very said kamanda
   
 9. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Chadema wanaongoza nchi kinadharia...lipo wazi
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hata ritz na rejao wanalijua hili na wanalikubali kiaina
   
 11. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,087
  Trophy Points: 280
  Mkuu unamanisha dr. Alikua mtu wa karibu sana na waongoza nchi (enzi hizo akiwa CCM)..? Maana yake ni kwamba alipojitoa CCM walikosa mshauri' hii imeongeza imani yangu kwa dr.. Mungu akurehemu na akuzudishie siku za kuishi zenye wingi wa neema!
   
 12. mwenyenguvu

  mwenyenguvu Senior Member

  #12
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kweli kabisa mkuu
   
 13. S

  SunStrong Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja mkuu!
   
 14. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ndio raha ya hoja makini,waropokaji wote kimya hawana cha kukanusha,mkulu mwenyewe anaikubali CDM nina mashaka kama hatajiunga rasmi before 2015 kuepuka kupelekwa puta akitoka magogoni
   
 15. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,114
  Trophy Points: 280
  Chadema ni kama Ng'ombe asiye na bei sokoni, eti ndo waweze kuongoza nchi wakiwa nje!!!!!!!!!.
  .
  "WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
   
 16. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  I salute
   
 17. h

  hans79 JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Rais wa Mbeya alisema watake wasitake lazima baraza la mawazir lifunjwe,sasa wewe unaandika nn!Pole rudisha akili sehemu yake.
   
 18. m

  mayere Member

  #18
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vidole viwili vipon up kaka...means people's power
   
 19. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watatafuta na ilani ya cdm waitekeleze maana hawawezi kusimamia ya kwao.
   
 20. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280

  M4C ni mziki mzito Mkuu wangu; umefunika mtaa mzima. Viredio uchwara vyote (sera, itikadi, vikao, mikutano, n.k. ya CCM na washirika wao) viko off vikisikiliza mvumo wa mziki huu wa kutisha. Umezoa kila rika - vikongwe hadi vitoto vinavyonyonya vimetekwa na huu mdundiko. Ha ha ha ha ha ha!
   
Loading...