CCM Kwa Faida Yenu Igeni Ngoma Za Wasukuma Za Bagika Na Bagaru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Kwa Faida Yenu Igeni Ngoma Za Wasukuma Za Bagika Na Bagaru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Apr 2, 2012.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika tunakwo kwenda kwa sasa CCM ningewashauri sana KUIGA MFANO WA NGOMA MBILI MAALUFU SANA KWENYE MIKOA YA KANDA YA ZIWA [Mwanza,Shinyanga na Tabora] maalufu kwa jina la BAGIKA NA BAGALU.

  Kwa watu wa makabila ya wasukuma, wanyamwezi na wasumbwa wanazijua ngoma hizo ambazo zina asili moja nzuri sana inayoleta msisimko kwa wapenzi na washriki wake kwa uchezaji wake,mbinu na mikakati yote yenye kila dalili za kuleta ushindani kati ya ngoma hizo mbili yani BAGIKA NA BAGALU.

  Dunia uendeshwa na uvumbuzi wa nadhalia [theory] ambazo zimetokana na matendo tofauti tofauti kama vile jinsi wadudu kama siafu [Lughaa ya Wasukuma na Wanyamwezi maalufu kama sungusungu] wanavyofanya kazi,utalatibu wake ule umeweza kutumika na binadamu kujipatia maendeleo kwa kufuata mtililiko mzima wa kazi husika unavyofanywa na siafu hao.Vivyo hivyo kuna mifumo kama matumizi ya conveyer belt nayo yametengeneza mfumo wa kufanya kazi na kugeuka kuwa kanuni ya binadamu kuitumia kama njia yake ya kumuongoza kufanya kazi kimaamuzi ya kikanuni.Ilikuwa ni kwa mfano wa siafu [sungusungu] ndipo wazee wajadi wa makabila ya Wasukuma,Wanyamwezi na Wasumbwa waliibuni jeshi la ulinzi la kienyeji lenye sura na muonekano wa kimatendo kama siafu [sungusungu au maalufu kwa lugha ya vijana Wasalangata].

  Nimetafakari sana kuwa tunakokwenda CCM kama chama kikongwe watake wasitake hawana budi kujifunza kwa kuangalia wazee wa makabila ya Wasukuma,Wanyamwezi na Wasumbwa wanavyoweza kuwa na ngoma hizo maalufu kwa makabila hayo zinavyochezwa na kuwa simba na yanga kwenye soka la Tanzania huku wachezaji hao wakiwa na urafiki na maelewano bila kujali tofauti zao za mapenzi ya ngoma zao.

  CCM na dhama hizi za siasa zinazoangukia ushindani na chama kikuu cha upinzani cha CDM ambacho kinaonekana kuwavuta vijana yawabidi kutafuta njia bora za kukubalika kucheza ngoma ya Bakika na Bagalu watake wasitake [Kwa Wasukuma wanajua watu maalufu katika makundi hayo ambao ni SAWAKA MWANAGANDILA NA TAGALA].Hawa watu wawili Sawaka na Tagala walipokuwa wanakutana kwenye ngoma hakika utapenda kuona michuano ya hali ya juu,ufundi,maarifa na burudani kali kali zenye kusisimua.Hatimae ya yote mwisho wa ngoma kati ya watu hawa wawili Sawaka na Tagala lazima mmoja awe mshindi kama ni ngombe kumi au gari atachukua yeye na team yake.

  Vivyo hivyo CCM, wanapaswa kutambua kuwa ile ngoma waliokuwa wanatawala na kuicheza kwa mdundo wanaotaka wao, kwa maarifa, mbinu,mizengwe na changamoto kadha wa kadha ambazo walizijua wao pekee yao sasa hawazichezi pekee yao na kuwa NGOMA IMEPATA MCHEZAJI WA PILI wamepata MPINZANI wa dhati tena mwenye nguvu ya vijana wenye damu zinazochemka vibaya sana na mfano wake ni Arumeru kaskazini na wako tayari kuicheza ngoma hiyo kwa masafa malefu.

  Kwa lugha nyingine yaweza kuwa Sawaka ni CCM na Tagala ni CDM,kwa wenyeji wa Mwanza,Shinyanga na Tabora wanajua shughuri ya watu hawa walipokuwa wakikutana.Hawa ni Team mbili tu yani mmoja ni Mgika na mwingine ni Mgalu. vituko, miujiza, uchezaji,dudanganyifu,mizengwe,uchakachuaji,na mengineyo yote kuwavuta watazamaji kujaa kwenye ngoma moja na kuacha nyingine ni ubunifu wa hali ya juu sana.

  Cha msingi CCM wanapaswa kutambua sasa kuwa CDM sio watoto tena hata kama wao ndio waliofungua milango ya vyama vya siasa na kuwa wao ndio wamekuza na kulea siasa za vyama vingi na diplomasia ya maneno, leo hii mtoto wa demokrasia anakaribia kugraduate hivyo hawana budi kujiandaa kuishi nae kama mtu mzima mwenzao mwenye ufahamu mkubwa wa mazingira na nyakati zijazo kuliko mzazi.

  Hivyo kwa CCM kuiga mfumo wa ngoma za jadi za Wasukuma na Wanyamwezi watapata jawabu la kuona ni jinsi gani wataendana na ngoma [Tanzania] huku wakishindani kushinda ngoma hiyo wakiwa na mpinzani wake CDM.Ubabe mizengwe na ujanja ujanja wa KICCM sasa umekwisha umebaki ujanja na maarifa ya kuwakamata Umma na hasa vijana wa kizazi kipya wakubali kutoa support na kuwapa imani kuwa wao CCM ni zaidi ya CDM,na wakati huo CDM nao wakipambana kuonyesha wao ni zaidi ya CCM.
   
Loading...