CCM kwa ahadi ndiyo wenyewe, Lowasa alimwahidi mwanafunzi huyu jibu la swali lakini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kwa ahadi ndiyo wenyewe, Lowasa alimwahidi mwanafunzi huyu jibu la swali lakini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 17, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Wakati Bw. Edward Lowasa akiwa Waziri Mkuu aliwahi kuulizwa swali na mwanafunzi wa shule ya msingi huko Mwanza vijijini na hakulijibu bali aliomba muda zaidi wa kulifanyia kazi. Bw. Lowasa baada ya Bunge letu machachari kumtupia virago vyake aliishia hadi leo hajalijibu au hata kumkabidhi mrithi wake Mheshimiwa Pinda kulipatia majibu ili kukidhi ahadi waliompa mwanafunzi mnyonge yule......................

  Majibizano yalikuwa kama ifuatavyo:-

  Mwanafunzi (swali)..........Hivi ni kwani serikali ya CCM imewarundikia watu wachache nafasi nyingi za uongozi wakati nchi hii ina waasomi kwenye taaluma mbalimbali wako tu hawana kazi?

  Mheshimiwa Waziri Mkuu (Jibu)..............Nipe mfano wa swali lako.

  Mwanafunzi..(ufafanuzi)............Huyo Mkuu wa Mkoa ana nyadhifa nyingi sana.

  Mheshimiwa Waziri Mkuu (swali).......Nyadhifa zipi?

  Mwanafunzi.(ufafanuzi)...yeye ni mbunge, mkuu wa mkoa, mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, diwani

  Mheshimiwa Lowasa alijikuna kichwa na kuweweseka na aka-ahidi (jibu).........Ninaomba muda wa kulitafutia jibu swali lako ambalo ni la kimsingi sana.


  Mwanafunzi...........Ninashukuru.


  Hadi leo mwanafunzi huyu hajajibiwa. CCM ni kawaida yao kulaghai raia kama watoto wadogo na baada ya kupata wanachotafuta basi huwatelekeza raia hao hadi uchaguzi mwingine ujao...a use and dump policy is in place for CCM

  CHAGUA DR. SLAA CHAGUA CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli mzee na mtoto alitiwa msukosuko sana
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,090
  Likes Received: 4,038
  Trophy Points: 280
  usikumbushe mzee we acha tu mtoto na babake walipewa jambajamba haijapata tokea kwa ujasiri wake huo
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hivi huwa najiuliza sipati majibu
  kama rais ambaye ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri anafanya nini humo barazani mpaka waende yeye na mawaziri wake kujitathmini kwenye halmashauri kuu ya chama ambapo yeye ni mwenyekiti wake pia? nadhani Kungelikuwa fair kama endapo akitenganisha kofia na kubakia na moja pekee ili kutoa mwanya kwa wengine wenye vipaji vya uongozi kujitokeza.

  CCM ya sasa inaundwa na kikundi cha watu wachache waliojilimbikizia madaraka na vyeo lukuki.
  HAWANA MAANA KABISA HAWA
   
 5. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa kutumbusha. To be specific, ilikuwa ni Ukerewe. TISS walimshughulikia sana, sijui kwa sasa yuko wapi. Yule mtoto ni shujaa mkubwa. Na alikuwa anasoma primary
   
Loading...