CCM kuweni waangalifu, Chama kimetekwa na serikali?

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,853
13,137
Kwa kanuni za msingi kabisa chama maana yake ni matakwa ya wanachama.
Iwe kiitikadi, kimaslahi au hata kimatarajio.

CCM imeanza kupoteza kwa kasi misingi hii ambayo inajengwa kwa ushawishi wa wanachama.
Hii ni hatari.

Katika kampeni tunazoziona Mwenyekiti wa chama hana tofauti na rais wa dola.
Analindwa, tena kwa mitutu wazi wazi, na vyombo vya dola.
Mwenyekiti walinzi wake wa serikali wamevaa nguo za chama.
Magari yote ya msafara, tunajua ni ya serikali, sasa yanatumika moja kwa moja na chama.
Kuna mmoja akadiriki kusema ma V8 ya chama ndio mafanikio ya chama.

Idara za maadhimisho kitaifa, idara ya serikali, kutumika moja kwa moja na chama.
Sasa mtu anajiuliza chama kimeishia wapi na dola imeanzia wapi.
Increasingly inaonekana kwamba sasa tunaipigia kura serikali.

Bashiru ana kazi kubwa ya kupambanua kwamba nyomi zinazoonekana si lazima ziwe za wafuasi wa chama, bali wananchi waliokusanywa na serikali vijijini ili kuishangilia serikali.
Mioyoni mwao kuna vitu tofauti kabisa.

Mwalimu aliwahi kusema Tujisahihishe.
Nami nilikuwa operation hiyo ya JKT, 1977.
 
Kwa hiyo ulitakja Raisi wa JMTZ asafiri bila ya Ulinzi wa Serikali? Unataka kuniambia Raisi wa USA D.Trump akienda kwenye Kampeni Florida au popote pale analindwa na kutumia magari ya Chama cha Republican na siyo beast lake la Serikali?

Ninyi watu ni wa ajabu sana, hivyo hata Katiba ya JMTZ mnaijua kweli? Hivi shida yenu ni nini, ni intelligence yenu haitoshi kuelewa mambo na kutatua matatizo au vipi?
 
tunajua we ni kichaa ila usionyeshe wazi kiasi hicho
 
tunajua we ni kichaa ila usionyeshe wazi kiasi hicho

Ni wapi nimeonyesha ukichaa? Ulitaka Raisi wa JMTZ alindwe na CCM? Ni wapi imeandikwa hivyo kwenye Katiba yetu kwamba Raisi wetu atalindwa na Chama chake?
 
Kwa kanuni za msingi kabisa chama maana yake ni matakwa ya wanachama.
Iwe kiitikadi, kimaslahi au hata kimatarajio.

CCM kimeanza kupoteza kwa kasi misingi hii ambayo inajengwa kwa ushawishi wa wanachama.
Hii ni hatari.

Katika kampeni tunazoziona Mwenyekiti wa chama hana tofauti na rais wa dola.
Analindwa, tena kwa mitutu wazi wazi, na vyombo vya dola.
Mwenyekiti walinzi wake wa serikali wamevaa nguo za chama.
Magari yote ya msafara, tunajua ni ya serikali, sasa yanatumika moja kwa moja na chama.
Kuna mjinga mmoja akadiriki kusema ma V8 ya chama ndio mafanikio ya chama.

Idara za maadhimisho kitaifa, idara ya serikalu, kutumika moja kwa moja na chama.
Sasa mtu anajiuliza chama kimeishia wapi na dila imeanzia wapi.
Increasingly inaonejana kana kwamba sasa tunaipigia kura serikali.

Bashiru ana jazi kubwa kupambanua kwambanyomi zinszoonekana si lazima ziwe za wafuasi wa chama, bali wananchi waluokusanywa na serikali vijijini ili kuishangilia serikali.
Mioyoni mwao kuna vitu tofauti kabisa.
Mwalimu aliwahi kusema Tujisahihishe.
Nami nilikuwa operation hiyo ya JKT, 1977.
ongea sawaswa usigeuze maneno.. kiuhalisia FISIEM ndio kimeinyakua madaraka pamoja na sirikale yenyewe.
 
Back
Top Bottom