Ccm kuweni makini, vueni gamba kwa kutofautisha la nyoka na la kobe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm kuweni makini, vueni gamba kwa kutofautisha la nyoka na la kobe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Nov 22, 2011.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama cha mapinduzi kipo katika wakati mgumu lakini wa muhimu sana. Maamuzi yatakayofanywa Dodoma yanaweza kukibeba na au hata kukiua.
  Kama gamba ni la wanyama wa aina ya nyoka au kinyonga basi likivuliwa basi chama kitakuwa kimenufaika kwani kitakuwa kina mwonekano mpya. Lakini ni muhimu kupima kama magamba yamegeuka kuwa ya kobe. Hapa uangalifu mkubwa uchukuliwe kwani ukivua gamba la kobe utakuwa umemuua kobe mwenyewe.

  Gamba la kobe ni pale jambo limeachwa na kuwa jambo sugu au la kawaida kwa kila ngazi. Na kama hali ni hiyo ukilivua hilo utaleta kifo. Dawa ya hapo ni kuwaacha kobe wawe na mayai mapya na mayai hayo ndiyo yawe msaada wetu.
  Hii ina maana ni kuruhusu mabadiliko makubwa katika ngazi zote muhimu. Angalao chama kiihimize serikali kufanya mabadiliko katika sekta za muhimu. Yaani pawepo na mabadiliko makubwa.
  Watu wakichoka wanafikia mahali wanachohitaji ni mabadiliko na hawajali ni ya madhara gani au uzuri gani. Mradi yawe mabadiliko. Nilisikia kule Moshi walikuwa wakisema kuliko kumchagua mgombea wa CCM wako tayari kumchagua mzee hata kama akitaka akalale bungeni.
  Kama kuvua magamba ni ya kobe na yameenea ngazi zote basi kuondoa wachache sio suluhisho. Ni muhimu kuleta mabadiliko katika uongozi wa maeneo nyeti, TAKUKURU, POLISI, TUME YA UCHAGUZI NK. Ni muhimu kuzingatia maoni ya wananchi juu ya mambo ya muhimu kama katiba nk. Watu wamechoka. NI MUHIMU KUTHIBISHA KUWA HAKI INATAWALA. TUJITAHIDI KUEPUKA DOUBLE STANDARD NK. KAMA MAGAMBA NI YA KOBE TUKIVUA TUJUE TUNASABABISHA KIFO. LABDA TUWASIHI VIONGOZI WENGI WAZEE WAACHIE VIJANA NAFASI KAMA MAYAI MAPYA YA KOBE.
   
 2. P

  Papushka Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushauri mzuri lakini umeenda kwa watu wasio sahihi, wakati usio sahihi na mahali pasipo sahihi..
   
 3. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilidhani ni wakati sahihi mkuu, wako katika kikao.
   
 4. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni afadhali kuvua hata hilo gamba la kobe huku ukijua kuwa kifo kitatokea lakini kama lilikuwa gamba hatari basi kobe atakufa lakini mvua gamba atabaki na heshima.
   
Loading...