CCM kuweni makini na mtumie intelijensia yaliyotokea Jimbo la Sengerema

budagala

Member
Jun 11, 2015
54
112
Kuna mtia nia mmoja ni Darasa la Saba ,ana tamaa sana ya madaraka na hatosheki. Alikuwa CHADEMA baadaye akawasaliti na kurudi CCM ili agombee tena ubunge. Anautafuta ubunge muda mrefu sana na hata hatujui ajenda yake hasa ni ipi.

Amewekeza pesa nyingi sababu yeye ni tajiri kwa kutoa vizawadi vya TV kila kijiji na kuhonga wajumbe ili wamchague.

Na kwa kweli amefanikiwa kumshinda hata Mbunge anayemaliza muda wake ambaye nae inasemekana anatuhumiwa kutoa rushwa kwa wajumbe.

Kuna tetesi kuwa wawili hao wamekuwa wakitambiana kuwa kila mmoja ana pesa kuliko mwenzie.

Kinachonikera ni huyo tajiri mmoja kuanza kununua watu kwenye mitandao na kuanzisha mada za kumsifia eti yeye darasa la saba kawashinda wasomi.

Hiyo ni fallacial argument na anatafuta appeal for pitty kwa jamii imuonee huruma yeye darasa la saba dhidi ya wasomi ili kamati kuu irufishe jina lake.

Ukweli ni kuwa washindi wote hao wananuka rushwa na endapo mmoja atapitishwa watakigawa chama.

Ushauri wangu kwa CCM, ni kuwapiga chini wote na kutafuta vijana smart na wazalendo ambao hawakutoa pesa wakaambulia kura moja au mbili.

Muda wa kuwa na wabunge darasa la saba umeisha. Wawekeze tu kwenye miradi yao.

Tanzania inahitaji kuwekeza kwa vijana wazawa hasa wenye shule ambao watachunguzwa vizuri tabia na uzalendo wao kabla ya kupelekwa bungeni.

Napendekeza vijana wengi wakipelekwa bungeni hata mishahara yao na posho pia ipunguzwe sababu hawatakuwa na mambo mengi
 
wamchague.Na kwa kweli amefanikiwa kumshinda hata Mbunge anayemaliza muda wake ambaye nae inasemekana anatuhumiwa kutoa rushwa kwa wajumbe
Rushwa ilitolewa na kila mtia nia. Lkn alieshindwa alizidiwa dau. Hata wewe msomi ulieleta madai haya ulitoa rushwa ila rushwa yako ilikuwa dhaifu.
 
Amekariri kuomba miongozo na kuwapiga wenye vichwa vya maana taarifa
 
Acha kulalama tafuta pesa nawewe ununue wajumbe.

Wajumbe hawana mishahara sasa watafaudika na nini??Ndiyo wakati wao huu.
 
KWA UCHACHE HIVI NDIVYO MTIRIRIKO WA MATOKEO YA KURA ZA MAONI ULIVYOKUWA JIMBO LA SENGEREMA.


1. Hamis Tabasamu (Darasa la saba)
2. William Ngereja (Master in Law)
3. Philemon Tano (Master in HRM)
4. Joshua Shimiyu (Master in HRM)
5. Lawrence Masha (Master in Law)
6. Yohana Kasenga (Shahada ya elimu)
7. Ndakama Salang’anya (BA Econom)
8. Kelvin Natto (BA in Law)
9. Tumaini Limbe (Shahada ya Kilimo na Mifugo)
10. Yunge Maige (Bachelor ya Uhasibu)
11. Mlyambelele Levi Ng'weli (Sheria + Post Graduate Diploma in Legal Practice)
12. Veronica K. Mugoyela (shahada ya Uzamivu fani ya Pharmacy)
13.William J.Tega PGD (Economic Diplomacy)
14. Eng. Suleman Daudi Arthur Nkalango (Ph.D In Information and Telecommunication Engineering)
15. Evarist Clement Matulanya (Shahada ya Ualimu)

16.Dotto Joseph Ndemella (Master of Arts in Economics)
17.Dr Godwin Silas Macheku (Adv.dipl (SRHR),MD(doctor of medicine),MMED (masters of medicine-obgy))
18. Onesmo Yegella Ntoneji (Masters in Procurement and supply chain management. PGD in Air Transport Management, (Airport operations))
 
Sawa mjumbe.
usomi pekee hauotoshi na uzalendo pamoja na kuwajibikaji.
wasomi wetu waliopiga kitabu Harvard ndo wamekua mafisadi wakubwa na kuingiza serikali kwenye mikataba mibovu ya wizi wa rasilimali za nchi.
 
Jitafakari kwanza ww unayedhani madaraka yana kutosheka maana hujui maana ya madaraka na sifa zake. .
 
Sasa kwani ni siri au ni uongo anaposema yy ni drs la saba na kawashinda wasomi?. Wenyewe mnakiri yy ni darasa la saba na hao wengine elimu zao mnazijua pia. Ameongopa wapi mpaka useme anafanya kampeni mitanfaoni kujisifia kwa ushindi wake wa drs la saba dhidi ya wasomi?

Kama we ni mmoja wa washindwa au rafiki wa mshindwa, kuwa mpole tu. Drs la 7 kawashinda vby!!!
 
Niambie wewe ulipata kura ngapi kwanza then nimchakachue huyu wa Lasaba. Unaonekana kijana smart na mzalendo kwelkwel
 
Sasa kwani ni siri au ni uongo anaposema yy ni drs la saba na kawashinda wasomi?. Wenyewe mnakiri yy ni darasa la saba na hao wengine elimu zao mnazijua pia. Ameongopa wapi mpaka useme anafanya kampeni mitanfaoni kujisifia kwa ushindi wake wa drs la saba dhidi ya wasomi??!!

Kama we ni mmoja wa washindwa au rafiki wa mshindwa, kuwa mpole tu. Drs la 7 kawashinda vby!!!
STD 7 Oyeeee kudadadeki wanaongezeka kwenda kugonga Meza.
 
  • Thanks
Reactions: Mu7
Back
Top Bottom