Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Siyo siri kuwa hizi njama zilizofanywa na hawa wasimamizi wa majimbo, ambao ni makada waaminifu wa CCM, kuwaengua kihuni wagombea wa vyama vya upinzani, kwa wingi na baadaye Tume ya uchaguzi kuwarejesha, kutakuwa kumewaongezea umaarufu mkubwa hao wagombea wa upinzani
Ni lazima hivi sasa wananchi watakuwa na hamu mno ya kuwasikiliza hao "wahanga" walioenguliwa na hao makada wa CCM na baadaye kurudishwa na Tume ya uchaguzi ya Taifa, kwa ilichokidai kuwa sababu za kuenguliwa kwao hao wagombea wa vyama vya upinzani hayakuwa ya msingi
Hivi unaweza anza jiuliza ni "makosa" gani waliyoyafanya wakati wakijaza fomu hao wagombea wa upinzani hadi waenguliwe kwa maelfu nchi nzima, wakati hakuna hata mgombea hata mmoja wa CCM aliyeunguliwa?
Hivi hawa wagombea wa CCM "waliibia" majibu ya kujaza hizo fomu kwa usahihi wa asilimia 100, hadi waonekane "malaika" na hao wasimamizi wa uchaguzi maDED na wapitishwe kwa asilimia 100?
Hao wasimamizi wa uchaguzi maDED, ambao ni makada wakubwa wa CCM, ndiyo waliopewa jukumu nyeti la kuwa "fair" la kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki.
Hakika kama ni mtihani wameshindwa vibaya na kama siyo bosi wao Jiwe ndiye "aliyewaagiza" kufanya madudu yote haya, wangejikuta wamefukuzwa kazi Mara moja!
Kwa Bahati mbaya walifanya "rewind" ya kile walichofanya kwenye ule uchaguzi uliopita ambao ulivurugika wa serikali za mitaa, ambao "walilazimisha" wagombea wao wa CCM kuwa wameshinda na kutulazimisha kuwa ndiyo viongozi waliochaguliwa na wananchi kwa asilimia 99.9!
Sasa ndiyo tunaweza kuamini maneno yaliyotamkwa na Jiwe kwa wakurugenzi hao nanukuu "wewe Mkurugenzi ninakulipa mshahara mnono, gari la kifahari la kutembelea na nyumba nzuri ya kuishi, halafu nisikie kwenye eneo lako, umemtangaza mpinzani kashinda, ujihesabu kuwa umejifukuzisha kazi" mwisho wa kunukuu
Hivi sasa ndiyo tutatambua hivi vitendo vya hawa makada wa CCM ambao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi namna vilvyo "backfire"
Hivi nyinyi maccm mnategemea hizo "cheche" atakazouunguruma nazo Maalim Seif huko Zanzibar baada ya kuenguliwa na baadaye kuejeshwa na Tume vitakuwaje?
Hivi unategemea na huyu "kibonge" Jacob mgombea wa ubunge wa Ubungo, hivyo vigongo atakavyoshuka navyo vitamuweka salama Dkt Mkumbo ambaye aliamini anateleza kiulaini kama vile yuko kule mteremko wa kule Kitonga?
Wahenga walinena kuwa mwisho wa ubaya ni aibu!
Kwa hiyo nyinyi maccm ndiyo mliolikoroga wenyewe, kwa hiyo hivi sasa muwe wapole na kulinywa!