CCM kuuza shule zake za WAZAZI kwa Serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kuuza shule zake za WAZAZI kwa Serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 13, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Daily News

  ALL secondary schools owned and run by the parents wing of the ruling party (WAZAZI) will be returned to the government, the National Assembly was told here yesterday. The Deputy Minister for Home Affairs, Ambassador Hamisi Kagasheki, said that the Ministry of Education and Vocational Training was working out modalities of repossessing the schools.

  He said this in response to a question from Ms Lucy Owenya (Special Seats-CHADEMA) who wanted to know government's efforts to make public the report by the Scotland Yard regarding fire which gutted Shauritanga Secondary School in Kilimanjaro Region in which 40 students perished some 15 years ago.

  The legislator noted that there were some students whose bodies could not be identified and were buried in a mass grave near the school. She wanted to know when the government would run the school as ward secondary school as promised by the then minister for education, Professor Philemon Sarungi.

  The Deputy Minister for Home Affairs said all WAZAZI secondary schools, including Shauritanga, would be possessed by the government. On the number of deaths at the school, Ambassador Kagasheki said a total of 40 people, including 37 students, four of them died in hospital later and two unidentified people were buried.

  He said since then, nobody had ever reported that a relative or a student from the school was still missing after the inferno 15 years ago. He advised that anyone wishing to see the Scotland Yard report regarding the Shauritanga inferno was free to contact the Ministry of Home Affairs. He said police regulations do not allow such reports to be made public.

  My Take:

  The so called "working out modalities" simply means the gvt and CCM are negotiating how much are the school worthy. CCM will be compensated handsomely right before the next elections. Otherwise, why would CCM release all of its schools free of charge to the Government as if inatoa sadaka kwa madhambi yake?
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Serikali ni ya CCM, sasa si wana nagotiate among themselves? Hapo hakuwezi kuwa na majadiliano yoyote. They will just simply decide how much to pay and it will be payed. Jamani these people are so innovative when it comes to stealing. Laiti wangetumia "kipaji" hicho kubuni mikakati ya kuiongezea serikali kipati mbona tungekua mbali?
   
 3. M

  Makfuhi Senior Member

  #3
  Jul 13, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hizo shule hazikujengwa kwa fedha za CCM. Shule nyingine wao ni mameneja tu kama shauritanga. wanachotakiwa kulipwa labda ni cost of management basi. Tuwe macho hapa.
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Mkuu hata zingekuwa zimejegwa na pesa zao bado kungekuwa na walakini. CCM iuzie kitu serikali ya CCM? Hilo tu wabunge na wananchi tunapaswa kujiuliza. Sema wabunge wengi nao CCM hiyo hiyo
  .
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hiyo njia mpya kupata mchango wa pesa uchaguzi mtasikia hy bei kuuziana,utasikia bil120 hapo ndipo utachoka,maana muda ndio huu kupiga cha juu kilinde chama kwenye uchaguzi.....kweli issue ingekuwa kulipa management cost na compensations tu labda na madeni fulani fulani ila wakihusisha majengo hilo deal.....kubwa na nono pande zote na wapambe pia.
   
 6. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwanafalsafa1

  CCM ni wezi hizo shule na mali zote za CCM zilikuwa za Watz WOTE lakini kwa ubabe in 1992 baada ya kuamua kuzipora kama wanataka kuziuza then tuwabane watuonyeshe documents how they were acquired na mengineyo hata majengo yote ya umoja wa vijana na wazazi including viwanja vya michezo proper vilitakiwa vichukuliwe na serikali kama walivyofanya kule Russia na CCM kwa mujibu wa mabadiliko madogo though sexed by ccm in 1992 haikupaswa kutumia jina la zamani na wangeanza upya hapo pangechimbika I tell you!!

  WASILETE ZA KULETA HAPA. Let me tell you kwa mustakabali huo Chadema kama nao wasingekuwa matawi ya CCM pamoja na vyama vyote vya kisanii vinavyojiita vya upinzani walitakiwa wahamasishe wananchi na kufungua kesi ya kikatiba ya kuainisha kwamba CCM ni haramu kwa hiyo haiwezi kuendelae kutesa period!! That is according to the conditions ya kuanzisha vyama vya siasa mwaka 1992!!

  Hii janja ya kuuza kisicho chako ni ubatili beyond all proportions nina wasiwasi hata ile Rescue Package anyoiita stimulant JMK aka Matonya anazotaka kuwapa Mabenki karibu 1.9 trilioni yaweza chotwa kumsaidia kuchaguliwa na watz wajinga 2010 nyie hamwajui CCM kama navyowajua!!! Changieni na nyie don't wait to be spoon fed!!!
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkereme,
  Umesema kweli ndugu mimi nakumbuka shule za wazazi michango ilikuwa ukipeleka ngo'ombe wako mnadani unakatwa mchango wa shule irrespective una mtoto au hauna, au wewe ni CCM au huna chama. Kwa hiyo CCM warudishe shule kwa Watanzania si wauze siyo za chama ni watu wote...wasitake ku-fool sisi!!
   
 8. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2009
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hakuna shule yeyote ile ya jumuiya ya WAZAZI - CCM. Hizi shule zilijengwa na wazazi wa maeneo husina. Wengi walichangia kwa kukatwa sehemu ya mauzo ya mazao, mathalani Kilimanjaro wote tulikatwa sehemu ya mauzo ya kahawa. Haya yalikuwa ni makubaliano ndani ya vyama nya msingi vya ushirika CCM haihusiki. Shule nyingine zilijengwa kabla ya uwepo wa CCM pamoja na jumuiya yake ya WAZAZI. Hizi shule ni za watanzania, period!
   
 9. M

  Mageta Opanga Member

  #9
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kupenda hesabu , sababu moja ni hivyo invyoaandikwa!
  Halafu baada ya miaka kumi na tano bado tu niwaulize Scotland Yard?

  Mimi nawajua 'WAZAZI' wengi waliokuwa CCM, na hata siku moja sijawahi sikia wana shule! Hata minong'ono!

  Leo hii wanauza shule?
  Naomba nielimishwe
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Huu uchaguzi unafurumua kila aina za mbinu ili kupata posho za kampeni!!
   
 11. M

  Makfuhi Senior Member

  #11
  Jul 13, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Shauritanga kama ilivyokuwa shule ilijengwa kwa nguvu za wananchi kwa kuhamasishwa na kanisa. nakumbuka kinamama walikuwa wakibeba mchanga na kinababa mawe n.k. wakati wa kusajili ilibidi kuwa na meneja ili isajiliwe na TAPA ikaombwa kuwa meneja. Nashangaa meneja anataka kuuza shule ya watu.
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Na mie nakumbuka wakati tunaanzisha shule ya Sekondari Irambo, tulikatwa pesa kutoka ktk mauzo ya Pareto. Kwa maana hiyo ni yetu wazazi, haiwezi kuuzwa bila sisi wachangiaji kushirikishwa!

  Duh!

  Sawa, nakubali kulikuwa na mfumo huu miaka hiyo

  Ni sawa!
  Ninavyokumbuka, kabla ya 'WAZAZI' kulikuwa na Tanganyika Parents Association (TAPA) enzi za Mwalimu na TANU, baada ya CCM kuzaliwa, TAPA ikageuzwa kuwa WAZAZI. Kimsingi sisiemu hawatatenda haki kuwauzia Watanzania shule zao!


  Kumbuka enzi za chama kushika hatamu, ndo enzi hizi walijimilikisha mali za Watanzania, kwa sababu chama ndio ilikuwa serikali na kinyume chake!
  Yaani wamejimilikisha kila kitu, viwanja vya michezo, maeneo ya wazi n.k., bila kujali kwamba wengine tulijitolea maeneo haya kwa moyo wotekwa maendeleo ya taifa. Leo hii wanauza bila kutushirikisha wachangiaji. Ni wizi.
   
 13. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bwana Mkeremi CCM iliwahi kushatakiwa na someone Shubi Balonzi na mahakama ikamtema kwa kusema kuwa hakuwa na kitu kinaitwa 'locus stand'. Hawa jamaa ni wezi wakubwa na wana mbinu nyingi sana. Tutawaweza tu pale watanzania wote watakapoacha ukondoo aliousema Mtikila.
   
 14. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,749
  Trophy Points: 280
  A friend of mine early this year suggested that CCM will have to find an alternative to Kagoda na EPA. I think selling all its schools may be just the right alternative. Lakini hebu tusemezane kuhusu hili. Hizi zinazoitwa shule za CCM si zile zile zilizojenjwa kwa nguvu za wapiga kura wote bila kujali itikadi za kisiasa. Could someone please enlighten me on that?
   
 15. M

  Mageta Opanga Member

  #15
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana Idimi,

  Kuna mengi ya kujiuliza hapa.

  Wana uza shule..hususan Shauritanga kwasababu ya kukimbia kuwajibishwa?

  Shule hizo haziwezi kubinafshishwa, tena?

  Nafikiri swali lilikuwa ni kujuwa kuhusu hiyo ripoti.

  Ni vigumu kuelewa mwandishi alitaka nini haswa.
   
 16. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sio hiyo tu tumain, pia wanafunzi kuanzia shule za msingi tulikuwa tunachangishwa shilingi 2 kwa ajili ya shughuli za ccm. Leo hii ukisema kuwa mali hii ni ya ccm na sio ya Watanzania ni kuwakosea Watanzania fadhila kabisa. Mali zote hizi zinatakiwa zirudishwa serikalini, na kama kuna madeni basi serikali itayarithi, lakini kuiuzia serikali (Watanzania) wakati wao ndio waliozijenga tena kwa kushurutishwa na serikali hiyohiyo ikiwa chini ya ccm sio haki.
   
 17. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Inawezekana, kwa sababu sio kila mmoja yuko tayari kubeba lawama na kuwajibika, hasa viongozi wa Jamhuri hii tukufu. Mfano hai ni wa mawaziri wako wafuatao, ambao katika misingi ya utawala bora na nchi inayofuata utawala wa sheria na haki walistahili kuwajibika kwa kujiuzulu:-

  1. Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi (kuvuja mitihani ya taifa ya kidato cha nne)
  2. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi (kuingilia mchakato wa vitambulisho vya uraia na mapigano yasiyokoma ya Watanzania kule mkoani Mara)
  3. Waziri wa nishati na madini (utiririshaji wa maji ya sumu ktk mito ambayo yameua Watanzania kadhaa mito mkoani Mara )
  4. Waziri wa miundombinu (kufeli kwa shirika letu la reli na la ndege)
  5. Waziri wa maliasili na Utalii (utoaji kimakosa wa vibali vya uwindaji wa wanyama kwa wageni ilhali bunge lilikataza)


  NB. Orodha ni ndefu na hakuna waziri hata mmoja kati ya hao ambaye kawajibika kwa kujiuzulu hadi sasa!

  Na shule zetu hizi tutauziwa hata bila ya waziri yoyote kujiuzulu kamwe, kwa utovu huu wa nidhamu!
   
 18. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hizi shule za wananchi zinataka kutumiwa na CCM kuchota fedha kutoka hazina. Wakimaliza nakuambia hata mdomo hawatafuta. Watafuata viwanja vya michezo na maeneo (ardhi). Hivi vyote walijimilikisha kitapeli kwa mlango wa nyuma kwa sababu serikali yao iliwaachia wachukue wanachotaka. Sasa watavitumia kuchota fedha hazina tena! Sasa sijui 2015 watafanya nini?

  Hizi shule ni za wananchi, hazina tofauti na hizi zinazoitwa shule za kata. Zilijengwa kwa mtindo kama huo huo, sasa sijui hiyo hati miliki hao wazazi wa CCM waliipataje maskini! Hizi shule wenyewe ni wananchi kupitia halmashauri zao za wilaya, miji na manispaa. Maeneo mengi hizi halmashauri ndo zilikuwa zinashughulikia ujenzi hadi kukamilika.

  Huu mzimu unaoitwa jumuiya ya wazazi wa CCM ulikuwa unazuka tu shule ikiisha kamilika. Hawa walitakiwa kuwa waendeshaji wa shule hizo au managers. Baada ya shule kuwashinda inatakiwa wazirudishe kwa waliozijenga (wananchi kupitia halmashauri zao).
   
 19. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Jamani mfa maji kweli haachi kutapatapa, Shule za TAPA leo waziwazi zimekuwa za CCM? Bila aibu na macho meupeeeee! Hebu waziorodheshe tuwaambie shule hizo zilijengwa namna gani,Jambo hili mwanzoni nilikuwa nafikiri ni mzaha wa waandishi kumbe kweli watu wanajiandaa na 2010,
  Hii inanikumbusha kule kenya ya mama Kenyata kuuzia serikali ardhi badala ya kuwarudishia ardhi yao wenyeji, lakini hebu tujiridhishe kidogo, Msishangae huko mbeleni hawa ndugu zetu wakatembea utupu kwani watakuwa wameuza hata nguo zao[​IMG]
   
Loading...