Elections 2010 CCM kutumia ubalozi wa JMT kumpongeza rais JK ni sawa?

pepekale

Member
Nov 25, 2010
60
50
wanajamii naomba kupokelewa jamvini,mimi ni mgeni hapa!ndugu zangu wana JF hapa russia kuna tawi la ccm,wameandaa sherehe za kumpongeza rais jk kwa ushindi hafifu aliopata katika ubalozi wetu hapa moscow!sasa ndugu zangu naomba kufahamishwa kama inaruhusiwa ofisi ya serikali kufanya sherehe ya chama fulani?na je kama chadema nao wakiomba ukumbi wa ubalozi wetu watapewa au inakuaje hapa?please msaada tutani wakuu!
 
tulia wewe Pepekale alaah!!!! mbona unataka kutuharibia shughuli! we jmosi njoo ule ubwabwa kwa mzee Mwambi.
 
hizo ndo sera hafifu za hiki chama sasa hivi wote ni wala bata from top mpaka down
 
kibabu mwambi anajaribu kusafisha nyota yake maana kutakuwa na reshuffle ya mabalozi soon!
 
by the way huu mfumo sijui tumerithi kwa wakoloni au kwa machief hata haieleweki kabisa.
watu wakiboronga au wakikataliwa na wananchi huku ndo wanapewa ubalozi!!! huu kweli ni upuuzi wa aina yake. na kunaweza kukawa na reshufle kubwa kwa kuwa demand kwa sasa ni kubwa sana....mawaziri wake zaidi ya kumi wakikosa kupewa ukuu wa mikoa basi watapewa ubalozi. wengine ni wazee wa kustaafu wanapewa ubalozi wakale bata badala ya kuwa active na kusaidia kuleta maendeleo wanaendekeza sherehe za kujipendekeza kwa chama.
tumeona akina mapuri,mwambi,lumbanga(aliyekuwa katibu mkuu kiongozi) na wengine lukuki....
nwayz nchi itajengwa na wazalendo na walanchi wote mwisho wao upo karibu sana.
 
Unashangaa hilo.Wakati wa kampeni za JK huku mikoani kwenye ofisi ya serikali tena ya kitaaluma kabisa bendera ya CCM sambamba na ile ya Tanzania zilikuwa zikipeperushwa pamoja bila woga.Wengine tulipo hoji mantiki ya hili wakasema we nini hiki ndicho chama tawala.Lakini sasa hivi bendera hiyo haipeperushwi tena.Tatizo la wasomi hao wa nje wanajiandalia nafasi za kula.Wamegundua ukitaka kupata ulaji wa haraka kimbilia huko ccm.Hao ni maslahi yanawa fanya wawe watumwa wa fikra.Tatizo kubwa la nchi hii ni kuwa hata wale unaodhania kuwa wamesoma na kuelimika bado hajaelimika.Na usidhani kama wanaelewa.Wengi wanakariri.Hawana uwezo wa kujenga hoja na kutambua dhamana yao katika jamii.Umaskini ni kitu kibaya sana.
 
wanajamii naomba kupokelewa jamvini,mimi ni mgeni hapa!ndugu zangu wana JF hapa russia kuna tawi la ccm,wameandaa sherehe za kumpongeza rais jk kwa ushindi hafifu aliopata katika ubalozi wetu hapa moscow!sasa ndugu zangu naomba kufahamishwa kama inaruhusiwa ofisi ya serikali kufanya sherehe ya chama fulani?na je kama chadema nao wakiomba ukumbi wa ubalozi wetu watapewa au inakuaje hapa?please msaada tutani wakuu!

Ndg Pepe Kale angalia unataka kuzungumza nini hapo....Sidhani kama Balozi Jaka Mwambi kawaalika Watanzania na marafiki wa tanzania waliopo Moscow na Vitongoji vyake kuja kushangilia Ushindi wa Mwenyekiti wa CCM,bali watu hao watakutana hapo kushangilia Ushindi wa Uchaguzi wa Rais,Kwa maana hiyo hata ushindi ungeangukia kwa Dr.Slaa au Prof.Lipumba bado uhalali wa sherehe hiyo ungekuwepo.Pitia tena mualiko wa sherehe hiyo uone maandishi yake...Tunawakaribisha kusherehekea Ushindi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kumalizika salama kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.Balozi anawawakilisha Watanzania wote bila kujali vyama vyao.
 
..haya mambo ya ajabu-ajabu kabisa.

..kuna umuhimu na ulazima gani wa kufanya sherehe baada ya uchaguzi mkuu?

..halafu huyo balozi ni mtumishi wa serikali, si mtumishi wa chama cha siasa.

..sijawahi kuona wala kusikia mahali popote pale, viongozi wa Idara, au mashirika ya serikali, wakifanya sherehe kutokana na kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

..kwa mtizamo wangu, huyu balozi anatumia vibaya nafasi yake, na fedha za umma.
 
ndg pepe kale angalia unataka kuzungumza nini hapo....sidhani kama balozi jaka mwambi kawaalika watanzania na marafiki wa tanzania waliopo moscow na vitongoji vyake kuja kushangilia ushindi wa mwenyekiti wa ccm,bali watu hao watakutana hapo kushangilia ushindi wa uchaguzi wa rais,kwa maana hiyo hata ushindi ungeangukia kwa dr.slaa au prof.lipumba bado uhalali wa sherehe hiyo ungekuwepo.pitia tena mualiko wa sherehe hiyo uone maandishi yake...tunawakaribisha kusherehekea ushindi wa rais wa jamhuri ya muungano na kumalizika salama kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.balozi anawawakilisha watanzania wote bila kujali vyama vyao.


yani mtu anatetea kabisa upuuuziiiiiuuuuuu , wanatumia hela ya nani? Na kwanini moscow tu?
 
Back
Top Bottom