CCM kutumia nguvu kubwa uchaguzi mdogo Igunga,je ni dalili njema kwao 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kutumia nguvu kubwa uchaguzi mdogo Igunga,je ni dalili njema kwao 2015?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by mkute, Oct 8, 2011.

 1. mkute

  mkute Member

  #1
  Oct 8, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Katika uchaguzi uliopita jimbo la igunga mkoani Tabora,tulishuhudia ushindani mkali toka mwanzo wa kampeni mpaka siku matokeo yanatangazwa ambapo aliekuwa mgombea wa ccm alitangazwa mshindi kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.
  Kikubwa tulichokiona ni jinsi chama kilichokuwa kinatetea kuendelea kulishikilia jimbo hilo mara baada ya aliekuwa mbunge wa jimbo hilo fisadi Rostam kujiuzulu kwa kisingizio cha kuachana na siasa uchwara za ccm.Kwanza tukashuhudia jopo zima la viongozi wa serikali ya ccm wakihamia Igunga,pili viongozi wote waandamizi wa ccm mpaka wastaafu walifika Igunga kuinusuru ccm,tatu vyombo vya dola viliahidi kutoiangusha ccm,nne tumeshuhudia gharama kubwa sana iliyotumika takribani shilingi bilioni mbili za kitanzania,na tano kutumika kwa baadhi ya taasisi za dini [BAKWATA] ktk kampeni hizo kuisaidia ccm ili iweze kushinda.
  Pamoja na nguvu zote hizo kutumika matokeo walioyapata ni mshangao mkubwa ukilinganisha na nguvu waliotumia,maana ninavyojua mimi kadri mtaji unapotumika mkubwazaidi, huzaa faida kubwa zaidi, lkn sivyo ilivyokuwa ccm walitumia nguvu kubwa wakapata kura kidogo.
  Swali langu kwao kama jimbo dogo tu nguvu zote hapo, je 2015 nchi nzima itakuwaje watagawanyika vipi ili kuidhibiti chadema inayokuja kwa kasi kama mbogo aliejeruhiwa ikizidi kudhihirisha jinsi nguvu ya umma inavyofanya kazi. Ni nani watampeleka Mwanza,Arusha,Mbeya,Shinyanga,Kilimanjaro,Iringa,Mara,Bukoba,Kigoma.....?ili awasaidie kupiga kampeni kama ilivyokuwa Igunga?
   
 2. dhahabuinang'aa

  dhahabuinang'aa Senior Member

  #2
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni dalili njema kuisajili hii No T 2015 CDM

  ni ukweli usiofichika ni wakati muafaka kwa CHADEMA kushika Dola.
  kwani watu wameshaamua kwa dhati kuking'oa kikundi kidogo cha mafisadi {sisiyem}
  na kuikabidhi dola kwa uongozi bora wenye upeo wa kiuongozi.
  tuone kama na 2015 watamwaga tsh ngapi?
  si wamezoea kuhonga itakula kwao
  na pia waache kuibaka Demokrasia!
  naichukia ccm maisha yangu yote!

  puuuuuuuuuuuuuuu! kafie mbali ccm
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  CCM inaweza kuepuka woga wa kuachwa nje ya madaraka 2015 kwa kufanya yafuatayo:
  1. Chama ni watu, jina ni utambulisho tu. Sasa kwa kuwa CCM wameona hawakubaliki wanaweza kuwatumia watu muhimu na kujitoa CCM kuhamia CDM na kuacha dummies ndani ya CCM kwa wale elected officials tu ili wasipoteze nafasi zao kwa mujibu wa katiba.
  2. Wakati haya yanaendelea mchakato wa kupata katiba iliyohuru uwe unaendelea ili 2015 uchaguzi uamue mshindi bila zengwe wala chakachuzi.
  3. Baada ya kuvunjwa bunge wanachama wawe huru kugombea kwa vyama wanavyovitaka au binafsi.
  Baada ya uchaguzi wa 2015 CDM itashinda na nchi kuwa na uongozi mpya ambao una watu waliotoka CCM ili kuhakikisha kuwa waliopo CCM hawafanyiziwi kama wanavyoogopa. Wakifanya hivi watakuwa wamekibadili Jina chama Tawala kutoka CCM kwenda CHADEMA na huku ndiko kujivua gamba halisi hasa.
   
 4. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii ni propoganda isikuwa na msingi. Jopo gani la serikali lililo hamia Igunga? Kama nimawaziri alikuwepo Wasira katika nafasi yake Kama mjumbe wa Kamati kuu ya ccm. Magufuli amekuja Igunga siku mbili za mwisho. Hilo ndilo linaittwa jopo la serikali ! Wrengine waliobaki ni wajumbe wa sekretarite na wabunge kadhaa. Chadema alikuwapo Mwenyekiti Katibu mkuu wabunge zaidi ya robo tatu. Bila kusahau madiwani wao wengi. Mbali na viongozi, waliletwa vijana 2000 wakiwemo wahalifu sugu. Wote hawa walisambaa jumbo Zima.swali ni chama gani
   
 5. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii ni propoganda isikuwa na msingi. Jopo gani la serikali lililo hamia Igunga? Kama nimawaziri alikuwepo Wasira katika nafasi yake Kama mjumbe wa Kamati kuu ya ccm. Magufuli amekuja Igunga siku mbili za mwisho. Hilo ndilo linaittwa jopo la serikali ! Wrengine waliobaki ni wajumbe wa sekretarite na wabunge kadhaa. Chadema alikuwapo Mwenyekiti Katibu mkuu wabunge zaidi ya robo tatu. Bila kusahau madiwani wao wengi. Mbali na viongozi, waliletwa vijana 2000 wakiwemo wahalifu sugu. Wote hawa walisambaa jimbo Zima.swali ni chama
  gani. Kilipeleka nguvu zaidi, ni ccm au chadema? Hebu wa kweli. Kuhusu 2015 tuuwachie wakati kwa nini tuandikie mate na wino upo?
   
 6. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Dalili ya mvua ni mawingu.
   
 7. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Raisi mstaafu ni nembo ya taifa anawakilisha maslahi ya watanzania wote na ndo maana anaendelea kuhudumiwa na serikali kwahiyo nilitegemea mtu kama huyu kuweka maslahi ya taifa kwanza kabla ya chama chake sasa kilichotokea Igunga ni kuona viongozi ambao hawapo kukulinda taifa hili kwanini ni kwa sababu mambo chama cha mabunduki kilichofanya ni kuhatarisha amani ya nchi wanayoihubiri kwa kuingiza udini,kutumia rasilimali za serikali,kutoa rushwa, kutoa ahadi za kiserilikali, kupiga watu, propaganda chafu ya magaidi/tindikali/kuchoma moto/kutangaza mgombea wa chadema amejitoa wakati si kweli, na polisi kupendelea uovu wa ccm na tume ya uchaguzi kushindwa kumuondoa mgombea wa ccm kwa kukiuka maadili ya kampeni namaanisha kununua shahada, kutumia/kutisha kwa silaha. Utaona kwamba ccm hakuna cha kujisifia zaidi ya kuogopa nchi inakopelekwa na wao wenyewe.
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha kukodi helkopta na kuleta robo tatu wa wabunge na top brass yote ya chama na hata kukodi mawakala kutoka nje ya Igunga siyo kutumia nguvu kubwa, kwa standard na finacial resources za Chadema? Kwa kulinganisha na ukubwa wa chama chao, ukubwa wa idadi ya viongozi wao na ukubwa wa mapato, hicho walichotumia ni asilimia ngapi.
   
Loading...