MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Ukisikia kutapatapa kwa mtu ni pale ambapo mtu huyu huamua kutumia ama kusingizia mtu mwingine kwa kumtaja jina lake ili mradi tu yeye apumue pindi anapobanwa na Mpinzani wake.
Kinachoonekana kwa sasa ni tabia ya wawabunge wa CCM kujaribu kulitumia jina la aliyekua waziri mkuu Mh Edward Lowassa kwa kisingizio kua upinzani umefunikwa mdomo kukemea ufisadi kwa vile wamempokea fisadi! Bila hata haya hata wale wenye Elimu na uelewa mzuri wa siasa nao kwa kufilisika kisiasa na wameamua kuungana na wapotevu hawa katika kulitumua jina la waziri huyu mustaafu kama ngao ya kujikinga na hoja za upinzani.
Nafikiri hii ni kujidanganya kwa sababu ya wanaCCM kukosa kuelewa kwamba;
1.Hakuna hata siku moja wakati wa mabunge yaliyopita ilitokea mbunge yeyote aliyesimama akamtaja Lowassa moja kwa moja kama fisadi.
2. Hakuna hata mtu mmoja ambaye mpaka Leo hii ametokea kuthibitisha ufisadi wa Lowassa kwa namna yeyote ile.
3.Kujaribu kutumia jina la mtu kujihami ambaye wakati ulipokua naye hujawahi kumsema hata siku moja ni majungu ama unafki.
4.Hata siku moja katika uongo na kweli haviwezi kukaa pamoja, hujitenga.
5.Kazi ya upinzani ni kuikosoa serikali kwa hiyo kutumia jina Lowassa kuzima upinzani haiwezekani.
6.Lowassa akiwa Chadema amefisadi nini?
7.Tokea ajiuzulu mwaka 2008 ufisadi uliisha uliongezeka?
8.Katika majipu yaliyotumbuliwa majipu mbona Jina Lowassa halimo katika majipu hayo?
9.Upinzani una watu makini wanaoelewa nini wanakifanya kwa taratibu, kanuni na sheria! Kwahiyo kuzima hoja zao kizembe hivyo haiwezekani.
10.Kutaja jina la mtu ambaye hayupo kumhusisha na ukweli unaogusha maslahi ya taifa bila kuthibitisha kuhusika kwake kama wengine ni kuongopea umma na ni ujinga.
11.Watanzania wa sasa sio wa miaka ya nyuma, wanajua mbivu na mbichi.