Ccm kutokua na hoja tutashuhudia na kusikia mengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm kutokua na hoja tutashuhudia na kusikia mengi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Japhari Shabani (RIP), Sep 12, 2010.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Habari za Kitaifa

  CCM yamkana Shehe Yahya
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 12th September 2010 @ 08:16 Imesomwa na watu: 579; Jumla ya maoni: 0

  MWENYEKITI wa Kampeni wa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema chama hicho na mgombea wake havihusiki na taarifa za kuongezewa nguvu za ulinzi usioonekana kama inavyoelezwa na Mnajimu Sheikh Yahya Hussein.

  Kinana alisema jana kwamba, Rais Kikwete ni muumini mzuri wa dini ya Kiislamu aliyelelewa katika misingi ya dini, anaamini afya njema au maradhi, vyote huletwa na Mwenyezi Mungu na vivyo hivyo katika suala la ulinzi wa afya ya mwanadamu.

  Alisema Sheikh Yahya ni Mnajimu, anao uhuru wa kusema vitu anavyoviona, lakini Rais
  Kikwete wala CCM visihusishwe na mambo hayo.

  Alisema mbali na ulinzi wa Mungu, Rais Kikwete ana kikosi madhubuti cha walinzi waliofundwa vyema kuhakikisha usalama wa Rais.

  Kauli ya Kinana imefuatia taarifa za baadhi ya vyombo vya habari kuwanukuu wanasiasa
  na kiongozi mmoja wa dini wakimtaka Rais Kikwete atoe tamko kuhusu madai ya Sheikh
  Yahya ya kumpatia ulinzi usioonekana.

  Sheikh Yahya alikaririwa akisema atatoa ulinzi usioonekana kwa macho ili kumkinga Rais Kikwete, ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi kesho.

  Hata hivyo, jana Sheikh Yahya alitoa ufafanuzi wake juu ya taarifa aliyoitoa awali akisema
  ilitafsiriwa vibaya na baadhi ya watu na kusisitiza kila mtu ana jini wake na kusema jini wa
  mgombea wa Chadema, Dk. Slaa anaitwa Subiyani.

  “Mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina nilikuwa
  nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na
  sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waislamu na Wakristu na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao,” alisema.

  Akifafanua zaidi, alisema hata Mfalme Solomon alikuwa na Jeshi la Majini na aliwatumia
  katika ujenzi na vita.

  “Kwa hiyo nawataka viongozi wa kidini na kisiasa wasihusishe mambo haya na uchawi haya ni mambo ya kawaida na yanafanyika ulimwenguni kote hata hao viongozi wa kidini nao
  wanawatumia majini katika kazi zao,” alisema.
   
 2. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kibaya kama "MTU ANAPOPOTEZA HEKIMA NA UELEVU NA KUBAKIZA KAULI"Mtu huyu anakua kama mzuka hafahamu anachokifanya wala kukizungumza.Hali hii imejitokeza na inaendelea kujitokeza kwa viongozi wa CCM hawana hoja, hawana aibu.Sasa wanakimbili katika uchawi na ushirikina,siasa za maji taka,kukimbia midahalo(Utashiriki vipi kwenye midahalo wakati huna hoja?CCM kushiriki katika midahalo kwa viongozi walio nao na nchi walikuifikisha nikuvua nguo hadharani.MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
Loading...