CCM kutoa tamko kuhusu wabunge wa Chadema

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko Dodoma na kusema CCM inapingana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taraibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz15jr5bjbS
 
Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64

Hii ilitarajiwa na Chadema wamejitakia wenyewe.
Kama ni ushauri tuliwapa, wakaamua kuwa kichwa ngumu na kumfuata Slaa.
Unatarajia nini kuongozwa na Mbowe na Slaa?
Note that Hon. Zito was not part of that fiasco.
 
KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,457
8,295
Hii ilitarajiwa na Chadema wamejitakia wenyewe.
Kama ni ushauri tuliwapa, wakaamua kuwa kichwa ngumu na kumfuata Slaa.
Unatarajia nini kuongozwa na Mbowe na Slaa?
Note that Hon. Zito was not part of that fiasco.
Upeowako ndo ukomo wako hatukulaumu!!!
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko Dodoma na kusema CCM inapingana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taraibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waliotarajia CCM wataunga mkono hatua hii ni majuha peke yao.

Hii inawatikisa bana, unatarajia wataelewa???

Halafu huyu anaeongea ni waziri au ni mbuni tu wa CCM? ana mamlaka gani ya kutoa wabunge kama anavyodai

Akafie mbele na asizingue watu. CHADEMA MWENDO MDUNDO, MPAKA MAJAMBAZI WAKATIKE VIUNO
 
Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,916
Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko Dodoma na kusema CCM inapingana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taraibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz15jr5bjbS
Ningependa kujua kwamba ccm wana madaraka gani zaidi ya CHADEMA? Wakati umefika wa kuelewa kuwa zile siasa za kuburuzana na kutoleana vitisho, zimepitwa na wakati. Ili demokrasia iweze kukua, tunahitaji vitendo zaidi kama walivyofanya CHADEMA pale ambapo misingi ya demokrasia imekuwa ikipindishwa au kutofuatwa kabisa.
 
nzitunga

Senior Member
Oct 31, 2010
193
52
Sidhani kama CCM watafika popote katika swala hili. CHADEMA wametii dhamira yao kwamba hawakubaliani na namna tume ilivyodili na matokeo ya urais. Na hili si swala lililo anzia hapa TZ. Huko Russia mambo yalikuwa hivihivi: soma link hii: BBC NEWS | Europe | Russian MPs make election protest

CHADEMA ina wanasheria wa kutosha ambao kama wangeona ni hatari kwao wangetumia njia nyingine ya ku-protest. CCM wakitaka shari hii lihishe ni kukubali ihundwe tume huru itakayochunguza matokeo ya uchaguzi wa uraisi. Na baadaye tuwe na tume huru ya uchaguzi. Tuwaondoe walioteuliwa na raisi katika kusimamia mchakato wa kumpata raisi na wabunge wake. To deal with walking out is like dealing with results and leaving the cause.
Najua JK na CCM kwa ujumla wamejisikia vibaya sana. And that is the good start for CHADEMA.
 
nyondoloja

Senior Member
Nov 10, 2010
189
52
sizanikamatumehuru yakuchunguzamatokeo yauraisi kamawatakubarikuiunda kamakwerikunauozo? siwataumbuka kwasasa tumehuruyauchaguziiundwekushirikisha vywama vywote
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
9,447
6,020
Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko Dodoma na kusema CCM inapingana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taraibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz15jr5bjbS

kanuni za bunge zinaruhusu chama kupeleka tamko au petition bungeni? naomba kusaidiwa hapo
 
The Infamous

JF-Expert Member
May 11, 2009
731
121
sehemu yoyote ile ambayo ina mamlaka na kanuni zake huwezi peleka TAMKO, ila kunaweza kukawa na remedy ya kupeleka petition kwa kutokuridhika na kitu flani...
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,883
Naona kuna matambo mengi huko CCM wacha ningoje matokeo ya action zao na nione Bunge kama kweli hii ni sehemu ya kazi yao.Chadema hawa kuchaguliwa na CCM wala JK wamechaguliwa na wananchi wa maeneo yao sasa ushauri wa Chiligati nauona butu hapa na hakuna litakalo endelea sema JK na CCM hawakutegemea na wamekumbwa na aibu mbele ya Dunia waliyo taka kuonyesha kwamba Nchi iko shwari hata baada ya kusigana katika matokeo ya Uchaguzi .Kiburi cha NEC ndiyo matokeo yake haya .
 
Mtembezi

Member
Oct 28, 2010
43
0
chiligati ni nani ndani ya bunge.
bunge linaongozwa na kanuni za bunge na sio kanuni za ccm
chadema hawajavunja kanuni za bunge wala katiba ya JMT
 
GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,319
306
kanuni za bunge zinaruhusu chama kupeleka tamko au petition bungeni? naomba kusaidiwa hapo

Mbunge au Wabunge wanaweza kupeleka Azimio Bungeni juu ya hili na kujadiliwa na kisha kupigiwa kura. Na inahitajika kupata uungwaji mkono wa 2/3 ya wabunge wote. Sasa kwa vile CCM ni wengi wanaweza kulifanya hili na wanayo hiyo 2/3 , halina ubishi na linawezekana. Na Azimio la Bunge halipingwi mahakamani wana JF
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom