CCM kushindwa kumdhibiti Lowasa ni janga lingine!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kushindwa kumdhibiti Lowasa ni janga lingine!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Losambo, Apr 5, 2012.

 1. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Endapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kitashindwa kumdhibiti kada wake maarufu E. Lowasa ni wazi watakuwa wamekiweka chama chao mashakani sana. Haya yanathibitishwa na tuhuma nyingi sana dhidi yake kama ifuatavyo"

  1.0 Ikimbukwe Sioi Sumari alilazimisha kupita kwa kutumia nguvu ya mtandao wake hali iliyopeleka CCM kushindwa pasipo na sababu za msingi. Wajumbe wengi wanakiri Sioi hakuwa chaguo la CCM bali la Lowasa na alitumia nguvu ya pesa kuhakikisha mgombea huyo anapita.

  Kwa hilo tu, kwa kuwa kuna uthibitisho ndani ya chama, basi kama chama hakikupaswa kufumbia macho. Kwa nini? Athari ya uchaguzi wa Arumeru ni kubwa sana kwa chama kwa watu wenye macho.

  2.0 Tangu na kabla ya hukumu ya G. Lema kulikuwa na tetesi kuwa nguri huyo wa siasa kushinikiza maamuzi kuwa Lema avuliwe ubunge!!! Leo imethibitika kuwa Lema siyo mbunge baada ya mahakama kutengua ubunge wake.

  Hoja ya msingi hapa si kutengua ubunge wa Lema bali;

  (a) Hali ya kisiasa itayokuwepo Arusha hasa endapo uchaguzi utarudiwa. Kama CCM itashindwa basi atakuwa amepelekea chama chake kushindwa mara mbili pasipo sababu za msingi au maslahi yake binafsi kuliko chama!!!!!

  (b) Hali ya kiuchumi ya taifa bado siyo shwari kiasi cha serikali kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya ukata wa fedha. Mfano ulio wazi ni malipo ya walimu ambayo serikali inapiga danadana kila siku, madeni ya watumishi wa umma wengine wakimemo askari ambao ndiyo walinzi wao na wanaowategemea katika shughuli mbali mbali.
  Na siyo hayo tu bali hata upelekwaji wa fedha kwa baadhi ya idara nao umekuwa ni shida kutokana na ukata wa fedha.
  Ikiwa yote hayo hayajaonekana kuwa ni muhimu ila kwa makusudi mtu anaenda kushinikiza hukumu ni kutoionea huruma serikali na wananchi wake ambao ndiyo walipa kodi!!

  Tendwa alisema kurudia ucahguzi jimbo moja tu gharama yake siyo chini ya 19bil!!! Ukipima Tshs 19bil zingeweza kuwa na matumizi mbadala badala ya kuendekeza chaguzi ambazo hukumu zake zimejaa utata.

  3.0 Yeye ndiye muasisi wa makundi ndani ya CCM. Katika kipindi cha hivi karibuni suala la makundi limekuwa midomoni sana mwa wanaCCM na kuonekana kuwaathiri. Nguzo kubwa ya makundi hayo ni Lowasa hasa la kwake ambalo linaonekana kuwa na nguvu ya kupingana na mwenyekiti wake. Hata suala la kujivua gamba ni yeye aliyekwamisha na mwangwi kutaka kumrudia mwenyekiti JK!!

  Hata kama Lowasa atakuwa anasingiziwa yote hayo basi tujiulize kwa nini yeye tu? Kuna haja ya kuwa makini zaidi na mienendo ya mtu kwa maslahi ya chama na taifa.

  Nikiwa mtu ambaye nina machungu na nchi yangu naomba sana CCM imemthibiti kada wake la sivyo CCM itapotea kabla ya wakati wake. Matendo yake kwa chama ni kama mtu anayetoboa mashua tunayosafiria wote.

  Nawasilisha.

  MoDs naomba uzi huu msiunganishe na wa hukumu ya G. Lema.
   
Loading...