CCM kushinda urais mwaka 2015, CHADEMA kutawala bunge! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kushinda urais mwaka 2015, CHADEMA kutawala bunge!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MTENDAHAKI, Oct 3, 2012.

 1. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Pamoja na vuguvugu la nguvu mpya linaloonyeshwa na chadema, cuf na nccr mageuzi ni wazi kuwa chama tawala ccm kina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2015.

  Hata hivyo chadema ina nafasi kubwa sana ya kuwa na wabunge wengi kuliko ccm, hali hii inaifanya cdm kuwa chama cha pili ambacho kinaweza kushika dola!nafasi kubwa ya kushinda urais bado inabaki kwa ccm kwani chama hiki kina watu mahiri wengi wanaokubalika sana kwa wananchi kuliko chadema ambayo ina watu wachache mahiri wanaoweza kugombe kwa nafasi hiyo na kukubalika!

  Yawezekana ccm ikaonekana kama imepoteza muelekeo lakini vipi ikiwa mh. Dr. John pombe magufuli akisimamishwa kugombea urais kwa tiketi ya ccm ni nani kutoka upinzani anaeweza kumzuia?kwa tathmini tuliyofanya inaonyesha magufuli ni mgombea wa kufikirika wa ccm anaeweza kukiokoa kisipoteze uongozi wa nchi.

  Ndiye mtu pekee mwenye nguvu kwa wananchi ambaye anaonekana kutokuwa na kundi linaloeweka ndani ya ccm, lakini zaidi ni kuwa wananchi wanamuona kama mtu anaeweza kusimamia sheria bila upendeleo. Kama akigombea na kupitishwa ni wazi kuwa ccm itapata kura nyingi hata kwenye majimbo ambayo wapinzani watashinda ubunge!

  Angalizo ni kuwa kama ccm itamsimamisha mamvi basi cdm itashinda kwa kishindo uchaguzi wa mwaka 2015 hata kama watamsimamisha aliyekuwa meya wa mwanza mh manyerere kugombea urais! Pamoja na huyo ccm haitaweza kupata ushindi kama wagombea kama sita, sumaye na membe watagombea, hali inaonyesha kuwa upinzania wa kwanza kwa wagombea hawa kama ilivyo kwa lowasa utatoka ndani ya ccm hivyo kuathiri juhudi zao kwa wananchi!hata hivyo tathmini ianonyesha watu kuvutiwa kwa kiasi fulani na dr. Mwakyembe ingawa pia wanasema ni mapema mno kwake kushika wadhifa wa urais kwani bado hana uzoefu wa kutosha wa uongozi katika ulingo wa kisiasa.

  Vilevile tathmini ya uwezekano wa mh shamsi vuai nahodha kuwa rais unaonyesha kuwa mtarajiwa huyo kwa kiwango kikubwa hana ushawishi na mvuto kwa wananchi wengi kutokana na kuonekana ni mpole na hatoweza kuwakemea mapapa ndani ya ccm.

  Wakati hali ikiwa hivyo kwa ccm, upande wa chadema unaonyesha kuwa na wagombea wote wenye nguvu ya kushinda urais kama ccm haitomsimamisha magufuli, ambao nwanongozwa na dr slaa, zito, mbowe na mnyika. Kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa wilaya nyingi zinaonyesha kuchoshwa na wabunge wa ccm wanaosinzia bungeni na kuunga mkono hoja pindi wanapokurupushwa kutoka usingizini!

  Upepo wa kisiasa unaonyesha zaidi ya wabunge kumi machachari wa sasa kutoka ccm hawatogombea tena ubunge kupitia ccm bali watahamia chadema na kushinda tena ubunge na wabunge zaidi ya ishirini wa ccm watapoteza majimbo yao!baada ya kumaliza utafiti huu nitauweka jamvini hapa mwanzoni mwa mwaka 2015!

  karibuni kwa maoni
   
 2. K

  Kalundebageshi Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu aliyesababisha Dr Kafumu kuvuliwa ubunge na Mahakama?
   
 3. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  aliahidi daraja na kweli akalipeleka Igunga!Yaani yeye akisema kinachofuata ni utekelezaji na hicho ndo wananchi wanampendea!
   
 4. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hizi kama ndoto, wapinzani bado sana, kwa sera zipi jamani? CCM wanawasikilizia tu na ma-M4C, V8M na sijui madudu gani, lakini mwisho wa siku ni chali tu.
   
 5. Tisha-TOTO

  Tisha-TOTO JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 1,173
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Ni dhahiri thread hii imehanikizwa na minyukano ya makundi yaliyomo ndani ya CCM. Na kwenye thread yako hii ni dhahiri unamfagilia mtu wako!

  Hatudanganyiki!!!
   
 6. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,955
  Likes Received: 6,714
  Trophy Points: 280
  Wewe mtabiri uliyechukua mikoba ya sheikh Yahya, ngoja nikuulize maswali machache.

  Huyo mgombea wako Pombe Magufuli, unayempigia debe, si ndiyo huyo aliyewakebehi watu wa Kigamboni kuwa ambaye hana nauli ya kulipia pantoni, apige mbizi hadi ng'ambo ya bahari? Si ndiye huyo huyo alienda Igunga na kuwaambia wananchi wa huko kuwa wasipomchagua mgombea wa CCM hawatajengewa daraja la Mbutu, akielewa kuwa anachokifanya ni kinyume cha sheria za nchi, ambazo zimeruhusu mfumo wa vyama vingi?

  Kwa maswali hayo mawili tu, unaweza kutambua upeo wa huyo mtu, unayempigia debe awe ndiye kiongozi mkuu wa nchi!!
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu MTENDAHAKI,..umetoa maoni mazuri lakini sijaona ni kwa vipi umeeleza jinsi hiyo CCM inavyoweza kushinda huo urais hapo 2015, lakini kwa kuwa ulijikita katika maelwzo ya CCM,ningependa kusema;

  Mkuu hao wabunge unaowasena watahama(which is expected)..ni kuhama si kwa ajili ya Ubunge wao tu hata reputation pia, especiallt wakihusishwa kuwa na Chama vibaya, ni dhahiri wazee wa CCM wanakubali kuna UOVU mkubwa ndani ya chama(mf. Mzee Malecela, Pius Msekwa n.k kupitia vyombo vya habari) lakini HAWATAKI kushighulikia uovu huo.

  Mkuu, sisi wananchi(regardless of political differences) tunachohitaki kuona ni uwajibishwaji wa waovu, wenye kuharivu vyama(CCM,CHADEMA,NCCR,TLP, nk).

  Tunachohitaji kuona ni THAT EXTRA MILE beyond what they "think" we want...We dont need for them to ADMIT and think that's it,..b'se even though they wouldnt yet we know the fishy things in CCM..We(citizens) want FULL MEASURE for the deeds, but if that's so hard they should wait for REPERCUSSION of this by 2015.
   
 8. G

  Galaticos Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  haina mashiko.....analysis is not convincing..
   
 9. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  mkuu ahsante kwa uchambuzi wako. siasa za chama tawala kwa sasa hazielekei huko kwa magufuri. ninamaana yeyote anayependa haki hawezi kuwa kiongozi bora ndani ya ssm. kinachoendelea sasa ndani ya ssm na setikali yake ni ubabe wa liwalo na liwe. expected candidate wao ni EL na Chenge as a result hawa wstathubutu kutwaa madaraka kwa ngunvu. let's waint and see.
   
 10. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Bora mumchague lyatonga mrema, kuliko huyo mtu! Naona maamuzi yake mengi ni ya kutafuta sifa bila akili hata chembe!
   
 11. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hahaaa....daraja la mbutu ni hadithi labda nyumba za serikali alioimnunulia small house ....halafu akili yako ndogo unaposema makufuli ni safi hana tofauti na jk na mkapa wote ni wale wale ...ungekuw una gari la mzigo ndio ungejuwa ...ukizidisha uzito faini dola 2000 lazima dola ....2015 cdm kote kote ccm is dead wapo tu kwa vile wapo

   
 12. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Naheshimu mawazo yako pia Tisha-Toto lakini jaribu kupita mtaani kwako halafu uliza vp watu wanaonaje kama magufuli akigombea urais hala uje unijibu humu
   
 13. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Hilo linaeleweka mkuu hippocratessocrates lakini watakula jeuri yao!huku mtaani huyo EL wanamwona wizi tu hata kama watu wanataka ushahidi wa kumpeleka mahakamani, ushahidi ano mwakyembe!
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mtendahaki kamwambie hivi mh magufuli;

  "Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuri shikamoo! kazi uliyonituma nimeikubali kwa moyo mkunjufu na kama nilivyokuahidi nimeifanya kwa uwezo na akili zote alizonijalia manani. Nimekwenda ulikonituma lakini sikuwakuta wenyeji wangu, nimewasubiri kwa muda mrefu hatimaye wakarejea. Lakini kwa mastaajabu yangu naamini na yako pia hawakunikaribisha na hawakutaka hata kunisikiliza. Hivyo nimerejea mikono mitupu, tujipange upya mzee. Naahidi kuendelea kushirikiana nawe katika mipango yako mingine siku za usoni. Asante kwa kuniamini"
   
 15. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Galaticos Nashukuru kwa mchango wako pia,sukushawishi hapa, hivyo ndivyo watu asilimia 95 niliokutana nao wanavyosema mpaka sasa!
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Binafsi huwa nashangaa sana kuona vijana wako wanajikita kwenye mijadala ya nani awe Rais na kuacha kabisa kujadili matatizo madogomadogo katika mitaa yao midogomidogo yanayohitaji jitihada ndogondogo za makundi madogomadogo kuyatatua.
   
 17. K

  KGARE Senior Member

  #17
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mim naona katika swala la Kigamboni sio tatizo, ila hayo ya daraja la Mbutu alipotea kwa sababu aliingia ki-ccm zaidi akajisahau, maana CCM ndio huwa wanajisahau kutenganisha serikali na chama katika kila kitu. Hadi Rais akienda kuzindua au kufanya shughuli za serikali unamkuta bado anafagilia CCM badala ya kufagilia wananchi kuwezesha tukio au maendeleo hayo. Hilo ndio tatizo!

  Bila kuwa biased kichama, kuhusu Magufuri kuwa kiongozi wa juu ngazi ya Urais naona hatafaa. Yeye ni mtendaji na anapaswa aendelee kutumika namna hiyo hiyo tu. Haijalishi chama gani kitachukua nchi lakini huyu bwana anapaswa kupewa kazi ya kusimamia mambo fulani. Ana kipaji cha kusimamia project zozote za serikali. Kwa tabia yake Magufuri ni Authoritative, Arrogant and Asiyeshaurika kirahisi, sasa akiwa Rais hata akiboronga atawasumbua wanaompinga.

  CCM huko mimi bado sijui watamleta nani atakayefaa maana so far, Lowasa, Membe, Sitta, Mwakyembe wote hawana uwezo wa kulifikisha taifa tunapotaka. Labda aje mwingine. Wameonesha udhaifu mkubwa sana kusimamia maswala ya nchi na wamekaa kimya makusudi hata wakati tuliotegemea wangesaidia nchi kwa nafasi walizokuwa nazo na taarifa walizokuwa nazo. Tabia hii ni yao, haitabadilika wakiwa ma-rais, hawataweza kubadilisha mfumo mbaya wa KUONGOZA nchi uliozoeleka katika mfumo wa CCM !
   
 18. i

  iseesa JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi PhD ya Makufuli aliisotea sawia au alipewa kwa sababu za kisiasa? Muda wa utafiti aliupata wapi? Ni nani alikuwa msimamizi wake? Mkandala Mkuu wa chuo UDSM siyo "mlamba-miguu" wa MAGAMBA na "homeboy" wake, hivyo alimuogopa? Anayejua naomba anijuze.
   
 19. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kumuogopa kunawezekana walimuogopa lakini katika mazingiria yafuatayo:
  1. Walimpa supervisors (internal) wote makada wa ccm
  2. Wakamtafutia external eximiners wanaojua hawawezi kumfelisha
  3. Curators wake walikuwa watumishi wa maabara za chuo
  4. Alifanyiwa analysis na wataalamu ambao wapo chuoni na hulipwa kwa kazi hiyo
  5. Most inputs za discussion zilitoka kwa supervisors wa ndani (akitegemea kuteuliwa baadae kifadhila)
  6. PhD Mchezo kameza tu vitu alivyoandikiwa kwani kwa hilo naamini ana kipaji na ni jembe kweli
  All in all bado angalau ali-attempt kusoma kuliko waliopewa za bure!
   
 20. d

  dewj Member

  #20
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  just keep on dreaming:A S embarassed:
   
Loading...