CCM kupendekeza mfumo tofauti wa uchaguzi: Ebu Tuujadili...

Jean chill

Member
Apr 8, 2011
69
20
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinafikiria kupendekeza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa uchaguzi ambao mbunge au diwani akifa au kujiuzulu hakutahitajika uchaguzi mdogo.

Badala yake katika mfumo huo (proportional representation) unaotumika pia Marekani na Afrika Kusini, chama kilichoshinda katika jimbo husika, kitapewa mamlaka ya kuteua mwanachama wa kurithi nafasi iliyoachwa wazi kwa kutumia orodha ya wanachama wake.

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifafanua utekelezaji wa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wa Aprili mwaka huu na kufafanua kuwa, mfumo huo utasaidia kupunguza usumbufu na gharama za kurudia uchaguzi.

Mbali na mfumo huo, pia kinafikiria kupendekeza kuanzishwa kwa mfumo mwingine wa uteuzi wa wagombea wa vyama ambao Mukama alisema unatumika Ujerumani, ambapo vyama vyote vya siasa vitatakiwa kuteua wagombea wake siku moja.

Alikiri kuwa sababu ya mfumo huo mpya wa uteuzi wa wagombea wa vyama, ni kuzuia tabia ya baadhi ya vyama kusubiri uteuzi wa chama kimoja na kuchukua wagombea wa chama hicho walioachwa, “Huwezi kukaa kusubiri wanaokataliwa na CCM, kwa sasa tunamfumo wa uteuzi sawa na ule wa kupanga magoli (mfumo unaotumiwa na vilabu vya soka kupanga matokeo kumpata mshindi),” alisema Mukama.

Chama hicho pia kwa mujibu wa Mukama, kinafikiria kuwafikisha katika vyombo vya kisheria watu waliokituhumu kuwa kimetumia zaidi ya Sh bilioni 3 katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Mukama ambaye alikataa kutaja fedha zilizotumiwa na chama hicho katika uchaguzi huo, alisema taarifa hizo za kutumia fedha nyingi, zililenga kukifitinisha chama hicho kwa wananchi.

Source: Habari leo
 
CCM should stop this now and right here!!! Wao kutumia pesa nyingi kugharimia chaguzi ndogo has nothing to do with the legitimacy of the democratic process. Ni lazima kila mpiga kura apewe haki ya kuchagua mgombea yeyote halali. Ni lazima kila kiongozi wa uwakilishi wa uma achaguliwe!!!

CCM does not speak for NEC or Political Parties Registrar!!! They don't speak for the Nation. We have the government to do all that. Sipendi kusikia habari za "chama kushika hatamu"
 
Unajua Mukama na fikiria kutumia makalio. Hivi hajuo kama magamba ndo kimekufa, na kama kimekufa mitego yote hiyo si itawaumiza wao? mbona wanashindwa kusoma alama za nyakati. Yaani magamba bado wanafiria wapinzani na wakati huo huo wanajisahau kuwa tayari come 2015 wao ni wapinzani wa kutupwa?
 
They do encompass a point thou.... A fine set of exemplar is the last Igunga political occurrence and it's effects of the whole procedure.
 
Nchi ya Demokrasia ya kweli India, wanafanyaje?

Siiamni Demokrasia ya Africa ya Kusini au Marekani
 
Back
Top Bottom