CCM kupatana, kutengana au kuendelea kuchunguzana?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Dalili zote kutoka Dodoma zinaonesha kuwa hatimaye mgogoro wa kiuongozi uliokikumba chama cha mapinduzi kwa takribani mwaka mmoja sasa utamalizwa kwa kutafuta njia ya upatanisho kati ya makundi yake mawili ambayo yamekuwa katika barabara ya kugongana kufuatia shutma za nani ni mwadilifu na nani ni fisadi.

Vyanzo mbalimbali kutoka Dodoma vinadokeza kuwa ripoti ya mzee Mwinyi iliyoundwa kutafuta chanzo na kutoa mapendekezo ya kutatua mgogoro huo inaonesha kuwa kwa hali iliyopo sasa itakuwa vigumu mno kwa chama hicho kutimuana au kupeana adhabu ambazo zitakifanya kionekane dhaifu. Kikubwa ambacho kinaonekana kubadilisha kabisa mwelekeo wa mapendekezo hayo ni kuundwa kwa Chama cha Jamii ambacho kinasubiri usajili wa muda ili kiweze kuanza kazi zake. Kuanzishwa kwa CCJ (kama nitakavyoonesha katika makala yangu mojawapo wiki hii) kunawatatiza viongozi wakuu wa CCM kwani kuanzia tetesi za uwepo wake juhudi nyingi zimekuwa zikifanyika kujua hasa ni "vigogo" gani wako nyuma ya chama hicho. Kutokana na kutokuwa na ushahidi wa nani anahusika au nani hausiki adhabu ambazo zinaweza kutolewa katika kikao hicho zaidi ni "onyo" na "karipio" kali lakini adhabu za kusimamishwa uongozi au hata kufukuzwa kutoka katika chama zinaonekana kukataliwa na wengi kwani itaonekana kuwapa faida baadhi ya watu kwenye chama hicho.

Kambi hizo ambazo zimekuwa zikigongana hasa kwa kutumia vyombo vya habari na kwenye majukwaa ya kisiasa ikiwemo Bungeni zilizaliwa mara baada ya ripoti ya Kamati teule ya Bunge iliyochunguza kampuni ya Richmond kuja na mapendekezo makali ambayo yalichangia kuanguka kwa aibu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa pamoja na mawaziri wengine wawili kitu ambacho kilisababisha kuvunjika kwa baraza la mawaziri wa Serikali ya Rais Kikwete.

Tukio la kujiuzulu Lowassa liligawa Bunge, wana CCM na Watanzania katika kambi zilizotofautiana kama Lowassa na wenzake walionewa au walistahili kuwajibishwa kutokana na tukio hilo. Wale ambao walionekana kumtetea Lowassa na wenzake mara moja wakaanza kuhusishwa na "watetezi wa ufisadi" huku kambi iliyosifia ripoti ile ya Richmond kuanza kuonekana ni "Wapiganaji wa ufisadi" Kwa mwaka mzima dalili za kambi hizo kupatana zilionekana kutoweka hasa kile amabacho kimetajwa kuwa ni jaribio la kumvua uanachama Spika wa Jamhuri ya Muungano na mmoja wa kambi kufanyika.

Spika Sitta alisalimika kuchukuliwa hatua na chama chake baada ya pendekezo la kuundwa ka Kamati ya Mzee Mwinyi, Mzee Pius Msekwa na Mzee Kinana kuundwa ili kutafuta chanzo cha migogoro ndani ya chama hicho, kupendekeza namna ya kutatua migongano ndani ya wabunge na jinsi ya kupendekeza namna jinsi Bunge litaweza kufanya kazi zake bila kusababisha migogoro kama hii. Juhudi za chini kwa chini za kuzipatanisha kambi hizo mbili hadi hivi sasa zimeshindikana na chanzo chetu kimoja kimetudokeza kuwa wananchi wasishangae kuona ni kina Mwakyembe na wenzake ndio wanapewa lawama za namna fulani kwa kuharibu sifa za wanachama wengine kwa kuwaita "mafisadi".

Ni matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kuwa CCM wataamua kutafuta njia za kidiplomasia zaidi kumaliza mgogoro wao kama walivyofanya kwenye suala la Richmond na hasa namna ya kuhakikisha hatimaye Lowassa na Mwakyembe wanakumbatiana, Mengi na Rostam wanakunywa chai pamoja katika hali ya kuonesha hatimaye "umoja na mshikamano" umepatikana ndani ya chama
 
Nchi haiendeshwi kwa kubembelezana, watu wazima ambao ni wezi kama EL, RA na kundi zima la mafisadi wanatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua. Kama hawatafukuzwa kwa uongozi kuogopa au kulindana huo ndio mwanzo na mwisho wa Chama Cha Majambazi.
 
ccm wataendelea kulindana.
Kama mlimwelewa vema alivyoongea Msekwa; wamefanikiwa kuurejesha Umoja wa CCM uliokuwa unasambaratika, je kauli hii itasimama? Wanajivunia kuwa Kamati ya kipekee iliyoweza kufanya jambo kubwa sana kwa chama kabla ya uchaguzi!
 
I wish wangefukuzana ili waunde chama kingine (hata waende huko CCJ) ...nzuri kwa demokrasi yetu..
 
nilijua tu hakuna jipya litakaloamuliwa kwa kuwa viongozi wengi wa CCM wamejaa uoga na ni wagumu kuthubutu kufanya maamuzi magumu vilevile
 
For how long will Watanzania continue to bend over to accomodate CCM mistakes and stupidity?
 
No one can whistle a symphony. It takes an orchestra to play it!You can work miracles by having faith in others.To get the best out of people , choose to think and believe the best about them.
 
Madai yao ni mwaka wa uchaguzi hivyo ni lazima wabebane ili waendeelee kuwa wengi Bungeni.,huu ni uzandiki kwa watanzania wanao wategemea.unafiki mtupu!siasa bwana me anaanza kuichoka bado mapemaaaaaaaaa.
 
Kitu wanachofanya CCM ni kama kumpa mgonjwa wa ukimwi dawa za kurefusha maisha wanajipa matumaini kama wako ANGAZA vile wanafikiri wametibu kumbe ni kinga tu ya uchaguzi ili upite dawa itakapoisha nguvu inabidi warudi tena ANGAZA(tume nyingine) dawa halisi ipo na wanaijua ila waogopa ni chungu kuimeza watafurahia mgojwa wao kumeremeta usoni lakini maradhi yanaendelea kumtafuna.
 
kinachotokea ndani ya ccm ni picha au movie ambayo mwisho wake itakuwa surprise....ni kweli watu wanaongea lugha tofauti kwa msukumu wa manufaa "yao"!....hapa natumia neno yao kwa maana ya ccm au binafsi......hivyo basi lolote linawezekana!
 
Tumechoka sana na mambo kama haya maana kila kikicha kuna ulazima kuona kuwa Tanzania inakuwa katika misingi Imara kabisa na sio katika mambo ya ajabu sana kama haya ua siku hizi
 
Mzee Mwanakijiji, kama nilipoandika kuhusu Bunge lafunika kombe, mwanaharamu apite, CCM nayo huko Dodoma inafunika kombe wanaharamu wapete.

Nilikuwa na source wangu mzuri sana ndani ya CC na NEC, baada ya kujua mimi ni mwana JF, amenikatia line kiaina. Namjaribu tena for the last time, asipotoa updade, basi itakuwa ni kweli, kombe limefunikwa.
 
mpasuko (niwe wa kwanza kutumia neno hilo) uliopo ndani ya CCM ni mkubwa mno kiasi kwamba wanaweza kuishia "kukubaliana kutokubaliana" lakini vile vile bila kufukuzana au kutukanana! wimbi limegeuka... goliathi anayumba
 
For how long will Watanzania continue to bend over to accomodate CCM mistakes and stupidity?

Is it correct to ask;

For how long will opposition parties continue to bend over to accomodate CCM mistakes and stupidity for expenses of Tanzanian tax payer in the so called ruzuku?
 
Back
Top Bottom