CCM kuondokewa na Mawaziri wakuu wawili ni jambo la aibu sana

Dalili za M/Rais kuhamia upinzani.? Au naota mimi. Kwanza ulishawahi kujiuliza kilichowaleta upinzani hao Mawaziri Wakuu zaidi ya uroho wa madaraka? Nadhani sasa hivi wao ndo wanaona aibu kuliko CCM. Maana kuna mmoja katoka Uwaziri Mkuu hadi Uenyekiti wa Kanda. Mwingine kashindwa kutetea jimbo kwenye ngome yake.
Hoja yako ni dhaifu na ya kizembe sana !
 
Mkuu, kwa nafasi yako humu JF ni aibu kujibu hivi. Ulitakiwa kuonyesha uzembe na udhaifu wa hoja yangu.
kama hukuona udhaifu wa hoja yako basi hutakiwi kuwemo jf , mnataka kila siku tuwafundishe tu , hukuona video inayomuonyesha Majaliwa akiimba " Tuna imani na Lowassa " ? unadhani kwani aliimba ?
 
Kila nikitafakari nashindwa kuelewa, chama kilicho madarakani kupuuzwa na watu wawili waliokuwa Mawaziri wakuu wa nchi na kukiacha wakati wa uchaguzi, ilikuwa fedheha kubwa sana yenye ukakasi ndani yake, na iliyoacha maswali mengi mno!

Swali la kujiuliza ni je, kama hawa waliokuwa na madaraka ya juu namna ile waliondoka, wewe mchumia tumbo, unasubiri nini? Jiulize ni watu wangapi mashuhuri waliobaki CCM kiukweli kabisa hivi leo?

Hivi wewe unaijua CCM kuliko Kingunge?
Chadema bhana 😂 bila shaka ukiona huu uzi unatamani ufutwe 😂

Chadema ndio wanapaswa kuona aibu kuchukua mamluki na bado mkafeli na bado tena mkakimbiwa na hao mliowachukua 😂
 
Back
Top Bottom