CCM Kuondoa Alama ya Nyundo Kwenye Bendera Yao?

Sekenke

Senior Member
Mar 3, 2008
132
29
Chama Cha Mapinduzi hujinadi kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi, japo kwa siku za karibuni ile M imehusishwa na Mafisadi.

Jana wakati Mwenyekiti wa Chama hiki, wakati akiwahutubia wazee wa CCM (kila mmoja alikuwa kavaa jezi za chama) Dar es salaam, alitangaza kuwakana wafanyakazi, hata kuzira kura zao licha ya kwamba kampeni hazijaanza. Kisa? Mgomo ulioandaliwa kisheria miezi kadhaa sasa.

Kwa mantiki hiyo, CCM yawezekana wamepania kuachana na alama ya nyundo kwenye bendera yao, sitashangaa ikiwekwa alama ya fedha (mafisadi) badala yake...

Yote hayo tisa, kumi kesho... siku ya tano tano: 5.5.2010
 
Naombea tusiwe waoga wa mkwara wa boss. Ama kweli tuna Boss wa mipasho km ya Sophia Simba...
 
Naombea tusiwe waoga wa mkwara wa boss. Ama kweli tuna Boss wa mipasho km ya Sophia Simba...

Nadhani siku ambayo watanzania walimpa huyu Mkwere nchi ndo walifanya kosa kubwa, hope jana angekuwa mzee Ben a.k.a Chinga boy angetema biti bila kucheka cheka au angetoa suluhisho la mgogoro uliopo kwa sasa, nilidhani ni ngonjera kumbe ni Head of State anaongea na Wazee ambao ni Ma-layman hawajui maana ya mapato na matumizi. nilishangaa kusikia kuwa anaongea na wazee wa Dar but sura nyingi zilikuwa vijana.
kama kiongozi wa Taifa anafanya yale ya jana je waongozwa watafanya nini.
 
Back
Top Bottom