Uchaguzi 2020 CCM kumtumia Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete mikoa ya Kusini Wananchi waonesha furaha

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi, tulileta ushauri hapa JF sisi wana CCM tunaojitambua ni hatua gani za kufanya mikoa ya Kusini mwa Tanzania hasa Lindi na Mtwara. Tulishauri mikoa hiyo atumike Mama Salma Kikwete kuweka mambo sawa kuhusu korosho. Tulishauri Majaliwa waziri mkuu asitumike huko kabisa.

Uamuzi wa CCM kumtumia Mama Salma Kikwete ambaye ni mzaliwa wa huko na kumuongeza Rais Mstaafu Kikwete kuzindua kampeni ni karata kubwa sana.

Tulishauri kwenye uzi huu Uchaguzi 2020 - CCM inapaswa kuchukua hatua na kujibu hoja: Je, Maisha ya wananchi yameboreka kwa miaka mitano iliyopita?

Hivyo basi, nampongeza Kikwete kwa kuanza kuhubiri maendeleo ya watu na sio vitu huko Lindi kwenye uzinduzi wa kampeni, watu wengi wana hali ngumu kimaisha.

Kikwete amejaribu kwa uwezo wake leo huko Lindi kupooza machungu ya gesi na korosho kwa njia ya kidiplomasia zaidi na kwa kutumia lugha laini ya ushemeji shemeji kwani ameoa huko Lindi.

Siasa za kuongelea maisha ya watu hasa Bima za Afya, Ajira ndio hatua kuu ya kujibu na kubomoa hoja za Tundu Lissu. Kwa maisha yalivyo mioyoni mwa watu bila kuwahubiria uchumi binafsi ni dhahiri CCM tutachakazwa sana kwenye kura. Ushahidi wa maisha magumu ni watu jinsi hata furaha hawana, shamra shamra za ngoma na sherehe za kuchangiana kwa mapesa sasa hali ni hovyo.

Napongeza chama changu kwa kuzingatia ushauri hapa JF, tutaendelea kushauri kwa nguvu na uwezo wetu ili CCM ishinde.
 
Kwani Kikwete si ndiye aliyepeleka jeshi Mtwara kwa ajili ya gesi ya Msimbati? Jiwe, akawanyang'anya korosho zao. Unadhani kuchekewa huko ndio kumesafisha mioyo yao wakati walitendwa na hao hao? Wenyeji wa kusini wanahitaji mfariji na mfariji hawezi kuwa mtesi wao.

Mtu anapeleka korosho yake ghalani anaambiwa arudishe iko chini ya kiwango. Huo usumbufu unadhani ni mdogo? Subirini mpewe na nyie haki yenu. Kama vipi mkawapige shangazi zao ili wawape kura zote.
 
Kwani Kikwete si ndiye aliyepeleka jeshi Mtwara kwa ajili ya gesi ya Msimbati? Jiwe, akawanyang'anya korosho zao. Unadhani kuchekewa huko ndio kumesafisha mioyo yao wakati walitendwa na hao hao? Wenyeji wa kusini wanahitaji mfariji na mfariji hawezi kuwa mtesi wao...
Meko akienda tena Mtwara atakutana na ule moshi safari hii ukiwa mzito zaidi
 
Kuna hali mbaya sana, Milo yao ya shida umasikini umewaingia mpaka moyoni kumkuta mwanaume kavaa dera kwasababu sio ajabu.
 
Kwani Kikwete si ndiye aliyepeleka jeshi Mtwara kwa ajili ya gesi ya Msimbati? Jiwe, akawanyang'anya korosho zao. Unadhani kuchekewa huko ndio kumesafisha mioyo yao wakati walitendwa na hao hao? Wenyeji wa kusini wanahitaji mfariji na mfariji hawezi kuwa mtesi wao...

Mkuu hiki chama na viongozi wake ni bure kabisa! Huyo Kikwete na CCM yake si alikua rais kwa miaka kumi,aliwafanyia nini hao wana Lindi na Mtwara? Hakuna cha ajabu hapo!
 
Napenda namna Jakaya alivyofanya siasa za kistaarabu. Alikuwa na wajibu wa kuslezea kitakachofanyika kwa miaka 5 na siyo mengine.

Jakaya na mama Salma siyo wageni kwenye historia ya Taifa hili, kwa mema yao na madhaifu pia.

Wananchi wa Mikoa ya Kusini wanayo haki ya kumchagua wanayeona anawafaa kwa mhula unaokuja, wasipoingiliwa katika maamuzi yao itapendeza zaidi.
 
Hawana mvuto wowote watakalisha malio chini kujinyenyekeza Mpaka watachoka , watu wamewachoka , si apige magoti kabisa
IMG_20200909_135554.jpg
 
Sawa mkuu
Basi tunawaomba mrudishe fao la kujitoa sisi wanyonge tutakufanya na kuziacha pesa kwa serikali hizo hizo zitafanyia maendeleo ya jamii badala ya maendeleo ya mmoja mmoja
 
KIKWETE,JIWE na CCM wote kwa pamoja wameua uchumi wa hiyo mikoa,huyu kikwete alipeleka vikosi watu wakaona wasiyowahi kuyasikia na akawaacha wakiwa duni zaidi.

Jiwe tokea ameingia hadi anaomba tena hajawahi (utamka neno "GESI",zaidi akachukua na "KOROSHO" na kula fedha ya "MBEGU"hakutaka hata utafiti wa mbegu bora ufanyike,akasema atawatandika wamama wa huko.

Chama chake kiko kimua mpaka leo hii.
 
Back
Top Bottom