G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Ripoti ya siri ya mwenendo wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 imevuja na aliyeivujisha hajajulikana bado. Inadaiwa kuwa mwaka 2016 Rais Magufuli aliamuru kufanyika kwa uchunguzi ndani ya chama hicho kuhusu mwenendo wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Katika sehemu ya taarifa ya ripoti hiyo inaonyesha kuwa Lowassa alikuwa tishio kwa serikali na alikuwa na kila dalili za kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 (Kama alikuja kushinda au hakushinda hilo hatujui).
Pia kuna sehemu taarifa hiyo inadai wapo baadhi ya viongozi wa upinzani waliopewa kiasi kikubwa cha fedha ili kumhujumu Lowassa. (Dah kumbe sio tu wale walioondoka bali wapo wengine ndani walikuwa wanatoa nyendo zote za mzee kutokana na mgao)
Kumbe Kikwete alikuwa anafanya vikao vya siri na viongozi wa upinzani kumhujumu mzee Lowassa. Inadaiwa wakati wa kampeni waliwahi kufanya kikao kimoja Morogoro.
Aisee inabidi wapinzani wajikomboe kwanza na njaa zao ndipo wawe na dhamira ya kweli ya kufanya siasa za kipinzani.
Hapo Lumumba hapakaliki tunaambiwa Polepole na Bashiru hawaongei na si hivyo tu bali hata Polepole na Kinana waliwahi kusuluhishwa mara mbili na waziri mkuu Kassim Majaliwa. Inadaiwa Bashiru kampiga marufuku asiandamane naye kwenye mikutano yake.